Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

Is it a 'goodluck' to have Jonathan as Commonwealth Chief Electoral Observer in Tanzania?

$
0
0
By Victor Mlunde
Having started out humbly as a zoology professor, Jonathan ‘accidentally’ switched to politics to become Deputy then full Governor of Balyesa State, then Vice-President who would eventually inherit the throne in 2010 after the death of President Y’aradua. Jonathan the ‘peace maker’
Former Nigerian president, Goodluck Jonathan (right) congratulates his February elections challenger and successor, General Muhammadu Buhari (left) after announcement of results.


Although the job of Nigerian president in itself is a great achievement, we would somehow agree that Jonathan’s footprints would not necessarily be visible in his presidency of the most populous and arguably the most strongest economy in Africa rather in setting a rare precedent in the continent that an incumbent desperately seeking extension of his rule can indeed concede defeat, relinquish power peacefully and become a “Godfather” of democracy. 
Switching to his current mandate as the Commonwealth Secretariat Chief Observer to Tanzania general elections, I am of an opinion that Jonathan’s role is pivotal and should not be confined to a mere observer who would just oversee the process and report back to NEC rather his role should extend to utilizing his diplomatic genius to counsel main candidates to accept outcome of polls. 
Despite having distinct political and democratic history, as non-industrial countries in Sub-Saharan Africa, Nigeria and Tanzania have indeed a lot to compare in that they both pursue multiparty political systems. 
Ethno-religious politics 
As is the rest of Africa, Nigeria is renowned for its trademark Muslim North- Christian South political culture that have polarized a country, also known for its ethnic divide. Indeed, Jonathan’s and Buhari’s divided electorate is a typical example. 
In Tanzania, we have recently witnessed some key presidential aspirants seeking votes on religious and ethnic lines too, hoping to benefit from a polarized electorate. 
Security factor 
We are all witnesses to the security tension brought about by the Boko Haram insurgency in Northern Nigeria around the time of elections, reaching its climax with abduction of 200 Chibok girls, pushing the polls for further six weeks. In Tanzania, security tension around Sunday elections has already been elevated by quest to guard votes outside 200-meter parameter from polling stations, a catalyst for clashes between/among party supporters and/ or security forces. 
Moreover, there is a lingering security uncertainty in various potential hotspots which are traditionally violent for instance Arusha, Mbeya - Tunduma, Mwanza and Zanzibar, to mention a few. 
Oil and gas factor 
Like Nigeria, Tanzania elections are set on top of a stiff but covert battle for access to ‘gas billions’ in Southern Tanzania. While Nigerian elections were seen as a rare opportunity for any elected leader to have an upper hand in production sharing agreements with international oil companies (IOCs), Tanzania elections suggest that the new leader will be influential in the newly found gas wealth, set to start flowing in the second half of his first 5-year tenure (2019 or so). Foreseeing this glory, already some local business tycoons and business networks are siding with some candidates to ensure they win State House and state coffers by hook or crook. 
Untested electoral technologies - BVR 
Faced with a challenge of democratizing electoral systems, both Nigeria and Tanzania used Biometric Voters Register in an attempt to make voters roll more inclusive, transparent and credible despite being . If Nigeria could make it, I believe the best efforts employed by the National Electoral Commission (NEC) in adding almost 3 Million voters in the register deserves an applause, although much has to be done to ensure electoral bodies become more independent, ending ‘unhealthy’ perception that they protect the incumbent regimes. 
Pre-electoral pledge for peaceful elections 
There is a lot to learn from former Nigerian president Abdisalam Aboubakar’s approach in forging a pre-election deal which compelled Jonathan and Buhari to accept outcome of elections. Whether that was a gentleman agreement or a legally binding one, at least it shows it can really work. Similarly, presidential contenders in Tanzania should sign such deals in future so as to impose a social and moral guilt on them.


NEC has played a more or less similar role at campaign level by engaging all parties to signing an MoU guaranteeing respect for electoral regulations and code of conduct. To some extent that has worked although key to it is for opposition parties to ensure they uphold democratic standards to the end by urging supporters to leave polling stations after voting.


How important is Jonathan to Tanzania 
In his address to members of diplomatic corps earlier in the week, Jonathan praised Tanzania for not only upholding peace and tranquility, but also for being the symbol of democracy and stability, often exporting the rare commodity to the rest of the continent. 
Indeed, his words should be an eye opener in seeing that as Tanzanians, we should not be complacent about peace but prove the world wrong in that we can emerge from these complex situations united. 
Way forward

Commonwealth is no stranger to brokering peace deals in the region, Zanzibar Muafaka Accord in early 2000s is the best example. As an exemplary African statesman, a diplomatic genius and now Head of Commonwealth Election Observation Mission, Goodluck Jonathan should employ preventive measures to counsel our presidential contenders especially opposition parties to accept the outcome of elections even if it means conceding defeat.  Urging supporters to go back home after voting will help avoid a catalyst for violence, prevent a potential trigger for a post-election conflict and help a seemingly divided country to rise above and move on.

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.


Victor Mlunde  is a Dar es Salaam - based Governance and Development Consultant with expertise in Elections, Democracy, Energy Governance and Conflict Resolution in the Great Lakes region. He can be easily reached through +255 714 289428 or vicmlunde@yahoo.com



MKURUGENZI MKUU MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA (TAA) AHUDHURIA MAHAFALI YA 46 YA SHULE YA SEKONDARI PUGU

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman S. Suleiman (kulia) akipewa maelezo na mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Pugu, Godwin Ogweyo kuhusu utengenezaji wa kadi ambazo hazichafui mazingira alipotembelea maonesho ya shughuli zinazofanywa na wanafunzi hao alipokuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya 46 ya wanafuzi wa kidato cha nne shuleni hapo, Dar es Salaam juzi (Oktoba 22). Kulia kwake ni Mkuu wa Shule hiyo, Jovinus Mutabuzi.
 Wahitimu wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Pugu, Dar es Salaam wakipiga makofi kumkaribisha mgeni rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman S. Suleiman wakati akiwasili ukumbini kuhudhuria sherehe za mahafali ya 46 ya wanafunzi hao, shuleni hapo juzi (Oktoba 22).
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Mhandisi Suleiman S. Suleiman akivishwa skafu na mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Pugu kama heshima ya kuwa mgeni rasmi katika sherehe za mahafali ya 46 ya wanafunzi wa kidato cha nne shuleni hapo, Dar es Salaam juzi (Oktoba 22). Kushoto ni Mkuu wa Shule hiyo, Jovinus Mutabuzi.

INTRODUCING Hamisi Kamanda - "Tulia" (Official Music Video)

Muangalizi Mkuu wa EU kutembelea vituo vya kupiga kura Jijini Dar es Salaam Siku ya Uchaguzi

$
0
0
Muangalizi Mkuu wa Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Umoja wa Ulaya (EU EOM) kwa Tanzania, Judith Sargentini, atakuwa akiangalia uchaguzi, katika vituo vifuatavyo, pamoja na vinginevyo Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Oktoba:

Muda
Jimbo
Kata
Kituo cha kupiga kura
Saa nne –Saa tano asubuhi
Ilala
Kisutu
Shule ya Msingi Kisutu A-1,2,3,4
Mtaa wa Kisutu
Saa tisa na robo – Saa kumi alasiri
Kawe
Msasani
Shule ya Msingi Oyster Bay, C-1,2,3
Barabara ya Haile Selassie

Kutakuwa na fursa za waandishi wa habari kufanya mahojiano na Muangalizi Mkuu kuhusu uangalizi wa awali wa EU EOM siku ya uchaguzi toka nchini kote.
EU EOM kwa Tanzania ndiyo ujumbe mkubwa kabisa wa kimataifa nchini na ambao upo kwa muda mrefu zaidi, kati ya 11 Septemba na 15 Novemba.

EU Chief Observer to visit polling stations in Dar es Salaam on Election Day

Schedule for media

The Chief Observer of the European Union Election Observation Mission (EU EOM) to Tanzania, Judith Sargentini, will be observing at, among others, the following polling stations in Dar es Salaam on 25 October:

Time
Constituency
Ward
Polling station
1000-1100
Ilala
Kisutu
Kisutu Primary School A-1,2,3,4
Kisutu Street
1515-1600
Kawe
Msasani
Oyster Bay Primary School, C-1,2,3
Haile Selassie Road

There will be opportunities for media to interview the Chief Observer on the EU EOM’s preliminary election day observations from around the country.
The EU EOM to Tanzania is the largest international observation mission in the country and is in Tanzania for the longest duration, between 11 September and 15 November.

JK ATEUA MAKATIBU WAKUU WANNE NA MANAIBU KATIBU WAKUU WATANO WAPYA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete usiku wa  Ijumaa, Oktoba 23, 2015, amewateua Makatibu Wakuu wanne wapya wa wizara mbali mbali. 
Aidha, Rais Kikwete amewateua Naibu Makatibu Wakuu wapya watano, amewateua Makatibu Tawala wa Mikoa wawili na pia amewahamisha Naibu Makatibu Wakuu wawili. 
Kwa mujibu wa uteuzi huo, Rais Kikwete amemteua Ndugu Hab Mkwizu kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma; Profesa Elisante Ole Gabriel kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo; Dkt. Yamungu Kayandabila kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na Mhandisi Omari Chambo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini.

 Aidha, kwa mujibu uteuzi huo, Rais Kikwete amemteua Mhandisi Paul M. Masanja kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini; Dkt. Maria Mashingo kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi na  Ndugu Zidikheri M. Mundeme kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.
 Wengine walioteuliwa kuwa Naibu Makatibu Wakuu ni Ndugu Tixon T. Nzunda ambaye anakuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Ndugu Emmanuel Kalobelo ambaye anakuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia. 
Walioteuliwa kuwa Makatibu Tawala wa Mikoa ni Ndugu Eliakim Maswi ambaye anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara na Mhandisi Madeni Kipande ambaye anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi. 
Katibu  Mkuu ambaye anahamishwa ni Bibi Sihaba Nkinga ambaye anakwenda kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Wanawake, Jinsia na Watoto kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.


Naibu Makatibu Wakuu wanaohamishwa ni Ndugu John T. Mngodo ambaye anahamishiwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kutoka Wizara ya Uchukuzi na  Ndugu Mwamini Juma Malemi ambaye anakwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.


Wateuliwa hao wote wataapishwa asubuhi ya leo, Jumamosi, Oktoba 24, 2015, Ikulu mjini Dar es Salaam.





DAWA ZA KULEVYA AINA YA HEROINE NA COCAINE ZATEKETEZWA CHINI YA UANGALIZI MKALI JIJINI DAR

$
0
0

 Sehemu ya Kinu cha Kiwanda Cha Saruji Cha Wazo Hill Jijini  Dar es Salaam  ambako dawa za kulevya zimeteketezwa jana chini ya uangalizi mkali . Akizungumza  na waandishi wa habari mara baada ya kuzichoma moto katika kinu hicho Jaji  wa Mahakama Kuu Edison Mkasimongwa alizitaja aina ya dawa hizo kuwa  ni Heroine mifuko 179 na Cocaine mifuko 81 zenye thamani ya Shilingi Bilioni tano ambapo  zilikuwa na Gram 175,000 ambazo zilikamatwa miaka kadhaa Mbezi Jogoo jijini Dar.
Jaji wa Mahakama Kuu Edison Mkasimongwa(kulia) akihakiki sehemu ya kinu cha kuchomea madawa hayo ya kulevya uku akisindikizwa na Mkurugenzi wa Mashtaka  Biswalo Mganga(kushoto) katika Kiwanda Cha Saruji Cha Wazo Hill Jijini  Dar es Salaam
Hii ndio sehemu ya mfuniko wa kinu kilichotumika kuchomea dawa za kulevya
Majaji kutoka mahakama kuu pamoja na polisi wakifuatilia kwa umakini uteketezaji wa dawa za kulevya
Askari wakifungua maboksi yaliyokuwa yamebeba dawa hizo za kulevya kwa ajili ya kuziteketeza katika kinu cha kiwanda cha Saruji hapa jijini Dar.
Jaji wa Mahakama Kuu Edson Masimongwa(kushoto) akifungua moja ya boksi lililobeba dawa za kulevya kwa ajili ya kuhakiki pamoja na kuziteketeza dawa hizo
Askari akizihakiki dawa za kulevya kwa kuzihesabu ili kuziteketeza ambapo zoezi hili lilifanyika katika Kiwanda Cha Saruji Cha Wazo Hill Jijini  Dar es Salaam jana mchana
Sehemu ya Dawa za kulevya zilizoteketezwa jana katika Kiwanda Cha Saruji Cha Wazo Hill Jijini  Dar es Salaam uku zikisimamiwa na majaji wa mahakama Kuu, jeshi la Polisi pamoja na mamlaka ya kudhibiti Dawa za kulevya hapa nchini
Mfanyakazi kutoka kampuni tya Saruji ya Twiga akiziteketeza dawa uku akisimamiwa na jeshi lapolisi, maofisa wa mahakama pamoja na viongozi wa kudhibiti Dawa za kulevya hapa nchini hapo jana katika kiwanda hicho
Maofisa kutika mahakama pamoja na maofisa kutika mamlaka ya udhibiti wa dawa za kulevya wakifuatilia tukio la kuteketeza dawa hizo

MTOTO HATUMWI DUKANI LEO . NI KATIKA UFUNGAJI WA KAMPENI ZA CCM JIJINI MWANZA.

$
0
0
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Pichani) amesema kuwa maandalizi kwa ajili ya shughuli ya kufunga kampeni za Uchaguzi Mkuu kitaifa kwa upande wa Chama hicho inayotarajiwa kufanyika hii leo katika Uwanja wa CCM Kirumba yamekamilika.

Na:George Binagi-GB Pazzo
Screen kubwa itafungwa nje ya uwanja huo kwa ajili ya wale watakaokosa nafasi ya kuingia uwanjani kwa kuwa shughuli hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa na maelfu ya wakazi wa Jiji la Mwanza na Maeneo jirani.
Mbali na Mgombea Urais wa CCM Dkt.John Pombe Magufuli kuwepo katika mkutano huo, pia Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaemaliza muda wake Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa miongoni mwa viongozi watakaohudhuria katika Mkutano huo wa Ufungaji wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa upande wa CCM 
Wakati Watanzania wakitarajia kushiriki zoezi la Uchaguzi Mkuu siku ya kesho jumapili ya Octoba 25, Chama cha Mapinduzi CCM kimejihakikishia ushindi mnono katika maeneo mbalimbali nchini kuanzia ngazi ya udiwani, Ubunge na Urais.
Shamra shamra kwa makada wa CCM zimepamba moto katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Mwanza katika kuelekea kwenye ufungaji wa kampeni za chama hicho kitaifa unaofanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba.

UCHAMBUZI WA MAGAZETI OKTOBA 24,2015

$
0
0
Magufuli afunika Dar ,Lowassa awanadi viongozi CCM kwenye kampeni ,UKAWA kufunga kampeni jangwani. Tazama uchambuzi wa magazeti. 
Mahakama yapiga marufuku kukaa mita 200,Magufuli afunika,Lowassa asema mwisho wa CCM kesho. Fuatilia uchambuzi wa magazeti ya leo. https://youtu.be/0OygojVUywg
UKAWA wapata pigo,mwisho wa CCM ni kesho asema lowassa, Mahakama yapiga marufuku mita 200.Fuatilia habari kupitia uchambuzi wa magazeti. https://youtu.be/TuyqynV3cuY
Van Gaal na Wenger watofautiana,Yanga yazitega Simba na Azam,Kocha wa Simba byebye.Fuatilia uchambuzi wa magazeti. https://youtu.be/aCc_l0GXYq0


SERIKALI YASAINI MKATABA WA UNUNUZI WA MAGARI NA KAMPUNI YA ASHOK LEYLAND KWA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA, JIJINI DAR

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job Masima (kulia), Makamu wa Rais wa Kampuni ya Kutengeneza Magari ya ASHOK LEYLAND ya nchini India, Bhimasena Rau wakisaini Mkataba wa ununuzi wa magari kwa ajili ya matumizi ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama ambavyo ni Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI. Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, jijini Dar es Salaam. 
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job Masima (kulia), Makamu wa Rais wa Kampuni ya Kutengeneza Magari ya ASHOK LEYLAND ya nchini India, Bhimasena Rau wakipongezana baada ya kusaini Mkataba wa ununuzi wa magari kwa ajili ya matumizi ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama ambavyo ni Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job Masima (katikati aliyevaa tai), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wakumi kulia), Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI, Jumanne Sagini (wanane kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na Viongozi wa Kampuni ya Kutengeneza Magari ya ASHOK LEYLAND ya nchini India. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


SERIKALI ya Tanzania imeingia Mkataba wa ununuzi wa magari kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama nchini na Kampuni ya Motorrama (T) LTD ambayo ni Wakala wa Magari aina ya ASHOK LEYLAND kutoka nchini India. 


Mkataba huo umesaniwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job Masima pamoja na Makamu wa Rais wa Kampuni hiyo ya Utengenezaji wa magari, Bhimasena Rau ukishuhudiwa na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, jijini Dar es Salaam.


Akizungumza mara baada mkataba huo kusainiwa, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja aliishukuru Serikali kwa msaada huo ambao utasaidia kutatua tatizo la uhaba wa magari katika Jeshi la Magereza.


“Utekelezaji wa mpango huu katika Jeshi la Magereza utakuwa na manufaa makubwa kwani utapunguza tatizo la uhaba wa magari kwa ajili ya shughuli za uendeshaji na utawala pamoja na utekelezaji wa jukumu la kuwasafirisha Mahabusu kwenda mahakamani na kurudi magerezani,” alisema Minja.


 Lengo kubwa la ununuzi wa Magari hayo unalenga kuboresha huduma za usafiri pamoja na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama hapa nchini.

TUPIGE KURA, TUPOKEE MATOKEO KWA AMANI NA UTULIVU, KUNA MAISHA BAADA YA UCHAGUZI

$
0
0

Bendera na ramani ya Tanzania
JUMAPILI ya Oktoba 25, 2015, Tanzania inafanya Uchaguzi Mkuu wa madiwani, wabunge pamoja na kumpata Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 Uchaguzi ni nini? Zipo tafsiri mbalimbali lakini mojawapo na iliyo wazi ni kwamba, hii ni njia ya kidemokrasia inayotumiwa na watu katika kuchagua viongozi wa kuwaongoza kwa kipindi fulani kwa mujibu wa Katiba au utaratibu waliojiwekea wenyewe. 

 Huu ni Uchaguzi Mkuu wa Tano kufanyika tangu mfumo wa vyama vingi ulipoanza tena mwaka 1992, lakini ni wa 11 tangu Tanganyika na Zanzibar zilipoungana mwaka 1964.

 Uchaguzi wa mwaka huu una umuhimu wa kipekee kwa sababu kadha wa kadha, mojawapo ikiwa umri wa miaka 23 tangu mfumo wa vyama vingi ulipoanza.

 Huu ni umri mkubwa, na kwa hakika vijana wengi waliojitokeza kujiandikisha safari hii ni wenye umri wa kati ya miaka 18-35, ikimaanisha kwamba wengi wao walizaliwa kuanzia mwaka 1992.

 Hawa wanatengeneza asilimia 57 ya wapigakura wote. Umuhimu mwingine ni kwamba, kulinganisha na uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995, safari hii demokrasia imekua na kupanuka kiasi cha kushuhudia wapigakura 22.75 milioni, idadi ambayo ni kubwa zaidi kuwahi kutokea nchini tangu tupate Uhuru. 

 Kwa upande mwingine, uhuru wa habari umepanuka ukiwamo ukuaji wa sekta ya habari na mawasiliano, hususan mitandao ya kijamii. Haya yote yanatokea kutokana na kuwapo kwa amani na utulivu, sifa ambazo zimeendelea kuitambulisha vyema Tanzania hata katika jumuiya za kimataifa.

 Uchaguzi Mkuu ni gharama kubwa kifedha, rasilimali watu na muda, na kama mambo yatakwenda mrama maana yake nchi itakuwa imeingia hasara kwa kupoteza fedha, lakini pia itaingia kwenye machafuko ambayo yatatowesha amani iliyodumu kwa miaka mingi.

 Madhara ya machafuko au vita – kama tulivyoshuhudia kwa majirani zetu Rwanda na Kenya ni vifo, ulemavu wa kudumu, kutengana na familia, ukimbizi na kuvurugika kwa uchumi, jamii na siasa kwa ujumla. Kwa miaka yote tangu Uhuru, licha ya uchanga na umaskini kama taifa, Watanzania hatujazoea maisha ya vurugu na machafuko na ndiyo maana tuna wajibu wa kuhakikisha uchaguzi huu unapita salama.

 Wajibu wa kulinda amani ya nchi yetu ni wa kila Mtanzania bila kujali rangi, dini, kabila ama nafasi yake katika jamii. Tunaposema hivyo tunamaanisha kwamba, vyombo vya dola vinapaswa kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria na kuhakikisha Watanzania wanapiga kura kwa amani kuchagua viongozi wao kwa utaratibu waliojiwekea. 

 Kimsingi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ndio wasimamizi wa chaguzi zote, hivyo wana dhamana kubwa kuhakikisha kila aliyejiandikisha na kujitokeza siku hiyo anatumia haki yake ya kikatiba kupiga kura bila kubughudhiwa. Ili kuondoa utata huo, NEC pia inapaswa kuhakikisha kunakuwa na uwazi kuanzia hatua ya kupiga kura mpaka wakati wa kutangaza matokeo, ambayo pia yanatakiwa kutolewa kwa wakati ili kuondoa mashaka miongoni mwa wagombea na wananchi kwa ujumla.

 Wanasiasa, hususan wagombea ama wapambe wao, wanapaswa kutoa kauli za kuhamasisha amani na utulivu kwa siku hizi chache zilizosalia kuelekea uchaguzi mkuu, siku ya uchaguzi na baada ya kutangazwa kwa matokeo.

 Wanasiasa wanaaminika kwa wananchi, kwa hiyo kauli yoyote watakayoitoa ama inaweza kujenga au kubomoa amani iliyopo, hivyo kuondoa utulivu na kuisambaratisha Tanzania ya sasa iliyotukuka ulimwenguni kote kama kisiwa cha amani na utulivu.

 Vyombo vya habari navyo vina wajibu mkubwa zaidi kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa usalama na amani na hata baada ya matokeo kutangazwa viendelee kudumisha amani hiyo. Hilo litawezekana tu iwapo vyombo vya habari vitaandika au kutangaza habari kwa kufuata sheria za nchi, miiko na maadili ya taaluma na fani ya uandishi wa habari ikiwa ni pamoja na kutoegemea upande wowote, kuepuka lugha za uchochezi na ushabiki wa kisiasa, kabla na wakati wa kutangaza matokeo.

 Kutokana na umuhimu huo, sisi wamiliki wa mitandao ya kijamii nchini Tanzania (Bloggers) tumejadiliana na kukubaliana kwa pamoja kuhusu hatma na mustakabali wa taifa letu kuhakikisha amani na utulivu vinadumishwa wakati na baada ya uchaguzi huu wa kidemokrasia na kwa kauli moja tumetoa msimamo wetu kuhusu amani ya nchi hii. 

 Kwa ujumla, hakuna anayeweza kujisifu kuwa ana uhalali zaidi wa taifa hili kuliko mwingine, taifa hili ni letu sote, hivyo wajibu wa kulinda na kudumisha amani na usalama wa nchi ni wa kila mmoja. 

 Tunaomba Watanzania wote wenye sifa wajitokeze kupiga kura kwa amani na utulivu, wasubiri matokeo kwa amani na utulivu, wapokee matokeo kwa amani na utulivu, maisha yaendelee kwa amani na utulivu, tusonge mbele kwa amani na utulivu huku tukijua kwamba kuna maisha baada ya uchaguzi, na hilo ndilo muhimu zaidi.

 MUNGU IBARIKI TANZANIA!

MAMA SAMIA NA DK. SHEIN WAFUNGA KAZI MKUTAO WA KUFUNGA KAMPENI ZA CCM ZANZIBAR LEO

$
0
0
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Makamu wa Rais Dk.Mohammed Gharib Bilal akihutubia mkutano wa kufunga kampeni za CCM uliofanyika leo kwenye Viwanja vya Kibanda maiti mjini Zanzibar
 Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi akizungumza kwenye mktano wa kufunga kampeni za CCM uliofanyika leo kwenye Viwanja vya Kibandamaiti mjini Zanzibar
 Dogo Aslay akitumbuiza wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za CCM uliofanyika leo Kibandamaiti mjini Zanzibar.
 Mgomea Mwenza wa Urais kwa tikei ya CCM Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia mkutano wa kufunga kampeni za CCM uliofanyika leo kwenye Viwanja vya Kibanda maiti mjini Zanzibar. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO).

DKT JAKAYA KIKWETE AONGOZA MAELFU YA WANANCHI KUFUNGA KAMPENI ZA DKT MAGUFULI JIJI LA DAR VIWANJA VYA JANGWANI

$
0
0
Mwenyeki wa chama cha Mapinduzi Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimnadi Mgombea Urais wa CCM Dt John Pombe Magufuli,mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Dar na vitongoji vyake kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Jangwani.

Mgombea Urais wa CCM Dkt Jonh Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa jiji la Dar es salam na Vitongoji vyake,katika uwanja wa Jangwani

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM Dkt Jonhn Pombe akihutubia maelfu ya wananchi waliojitokeza kwa wingi katika viwanja vya jangwani,alipokuwa akijinadi na kuwaomba wampigie kura za ndio na hatimae aibuke kinara katika nafasi ya Urais ifikapo Oktoba 25 mwaka huu kwenye uchaguzi Mkuu.
Nyomi uwanja wa Jangwani likiwa tuliiiii.
Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wananchi wa jiji la Dar na viunga vyake wakati wa kufunga kampeni za lala salama za Mgombea Urais wa chama hicho.Dkt Magufuli,uliofanyika viwanja vya Jangwani,jijini Dar.
Sehemu ya umati wa wananchi wakiwa wametulia wakisikiliz Sera za Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akijinadi mbele yao kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika ndani ya viwanja vya Jangwani.
Sehemu ya umati wa watu
Wananchi wa jiji la Dar na vitongoji vyake wakifutilia mkutano wa kampeni wa CCM .
Sehemu ya maelfu ya wananchi wakiwa wamekusanyika katika viwanja vya Jangwani kwenye mkutano wa kampeni za lala salama,ambapo Mwenyekiti wa CCM,Dkt Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa ndiye mgeni rasmi,wakiwemo vingozi mbalimbali wa cma na Taifa kwa ujumla.
Mwenyeiti wa CCM Dkt Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Katibu MKuu wa chama hicho cha CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana wakishangilia jambo wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Dar waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Jangwani jijini Dar.Pichani kulia ni  Mke wa Mwenyekiti wa CCM,Mama Salma Kikwete
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,na Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi,Mama Salma Kikwete akijadiliana jambo na Mke wa Mgombea Urais wa CCM,Mama Janeth Magufuli ,kwenye mkutano wa kampeni za lala salama uliofanyika viwanja vya Jangwani jijini Dar.


BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA OKTOBA 23,2015

MAADHIMISHO YA SIKU YA TAKWIMU DUNIANI YAFANA

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuhutubia kwenye maadhimisho ya Siku ya Takwimu Duniani yaliyofanyika leo katika Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika jijini Dar es Salaam. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni "Takwimu Bora, Maisha Bora".
 Wanafunzi wa Stashada wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika wakiwa wameshikilia bendera za nchi wanachama wanaoshikiana na nchi ya Tanzania kuendesha chuo hicho wakati wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Duniani yaliyofanyika leo katika Chuo hicho kilichopo jijini Dar es Salaam. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni "Takwimu Bora, Maisha Bora".
Baadhi ya washiriki wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa (hayupo pichani) wakati akihutubia kwenye maadhimisho ya Siku ya Takwimu Duniani yaliyofanyika leo katika Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika jijini Dar es Salaam. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni "Takwimu Bora, Maisha Bora". (Picha na Veronica Kazimoto)

Na: Veronica Kazimoto
WATAKWIMU vijana wameaswa kufanya kazi kwa weledi na uadilifu ili kusaidia katika ukusanyaji na upatikanaji wa takwimu bora zitakazosaidia katika kupanga mipango ya maendeleo.
Akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Takwimu Duniani yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa amesema vijana wenye taaluma ya takwimu wana nafasi kubwa katika kuhakikisha kuwa kuna upatikanaji wa takwimu bora nchini.

"Ninyi watakwimu ambao bado ni vijana mna jukumu la kuhakikisha kuwa mnatumia taaluma yenu ya takwimu katika kusaidia upatikanaji wa takwimu sahihi ili zitumike katika kupanga na kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo,” amesema Dkt. Chuwa.

Dkt. Chuwa amesema maadhimisho haya ya Siku ya Takwimu Duniani yana nafasi kubwa katika kutambua umuhimu wa takwimu katika kufanikisha utoaji wa huduma mbalimbali za kijamii na kuboresha maisha ya wananchi.
 
Aidha, amesema kuwa kutokana na dunia kuzindua Mpango Mpya wa Maendeleo Endelevu (SDGs), ofisi yake imejipanga vyema katika kuhakikisha takwimu bora zinapatikana kwa wakati ili zisaidie Taifa katika kutekeleza malengo ya mpango huo.

“Kutokana na umuhimu wa takwimu katika utekelezaji wa malengo 17 na viashiria 169 vya Mpango wa Maendeleo Endelevu, Ofisi ya Taifa ya Takwimu imejipanga vyema katika kuhakikisha takwimu zote muhimu zinapatikana na kusaidia katika utekelezaji wa malengo ya mpango huu,” amesisitiza Dkt. Chuwa.

Siku ya Takwimu Duniani huadhimishwa kila baada ya miaka mitano tarehe 20 Oktoba ambapo kwa mwaka huu maadhimisho haya yameongozwa na Kauli mbiu isemayo “Takwimu Bora, Maisha Bora”.

ASKARI MOSHI,WANAVYOJIWEKA TAYARI KWA UCHAGUZI WA KESHO

$
0
0
Baadhi ya viongozi wa ngazi ya Juu Katika jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro wakiwa katika maandalizi ya mazoezi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro.Fulgence Ngonyani akipokea taarifa fupi toka kwa kiongozi wa kikosi cha kutuliza ghasia.
Askari Polisi wa vikosi mbalimbali vya jeshi hilo mkoa wa Kilimanjaro wakiwa katika zoezi maalum.

Asakari Polis wakiimba nyimbo katika zoezi hilo.
Baadhi ya viongozi wa jeshi hilo.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

AMSHA AMSHA YA MWANZA, KUELEKEA MKUTANO WA KUFUNGA KAMPENI ZA CCM

$
0
0
 Leo ni Leo Mwanza... maana wakazi wa jiji La Mwanza na vitongoji vyake wamejitokeza kwa wingi kumpokea mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli. Huku Maelfu ya watu wamejitokeza kwenda CCM Kirumba jijini Mwanza kuhudhuria mkutano wa kufunga kampeni leo Oktoba 24, 2015.
 Kila mmoja akijikaza kujongea CCM Kirumba, Mwanza.
 Vijana wamehamasika kweli kweli....

DKT JAKAYA KIKWETE NA DKT JOHN POMBE MAGUFULI WAWASILI JIJINI MWANZA MCHANA HUU KUHITIMISHA SHUGHULI ZA KAMPENI

$
0
0
 Mwenyekiti wa CCM,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na Mgombea Urais wa chama hicho Dkt John Pombe Magufuli,mara baada ya kuwasili katika uwanja wa CCM Kirumba kuhitimisha shughuli za kampeni nchini kote,ambapo hapo kesho wananchi wanatarajia kupiga kura ya kuwachagua viongozi wawatakao.
 Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Kikwete na Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli wakielekea jukwaani kwa pamoja mara baada ya kupokelewa katika uwanja wa CCM Kirumba ambapo umati mkubwa watu umejitokeza kushuhudia tukio hilo adhimu.
 Mara baada ya kuwasalimia Wananchi kwa pamoja wakirejea meza kuu.

 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania kupitoa chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwasili ndani ya uwanja wa CCM Kirumba huku akilakiwa na melfu ya wakazi wa jiji la Mwanza waliofurika hivi sasa kwenye hitimisho la mikutano ya kampeni.
 Wakazi wa jiji la Mwanza wakishangilia wakati Mgombea Urais wa CCM alipokuwa akiwasili ndani ya uwanja wa CCM Kirumba hivi punde kuhitimisha mikutano ya kampeni,ambapo kesho Wananchi nchini watapiga kura kuwachagua viongozi wawatako kuwatumikia katika awamu ya tano.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania kupitoa chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwasili ndani ya uwanja wa CCM Kirumba huku akilakiwa na melfu ya wakazi wa jiji la Mwanza waliofurika hivi sasa kwenye hitimisho la mikutano ya kampeni.
PICHA NA MICHUZI JR-MWANZA

MKURUGENZI WA SHIRIKA LA MISAADA LA UINGEREZA AKUTANA NA RAIS.

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana  na Mkurugenzi wa Shirika la misaada la Uingereza DFID Vel Gnanendran alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kuzungumza na Rais leo (katikati) Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bibi. Dianna Melrose.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na mgeni wake Mkurugenzi wa Shirika la misaada la Uingereza DFID Vel Gnanendran alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
 [Picha na Ikulu.]

RAIS KIKWETE ATEUA MAKATIBU WKUU WANNE WAPYA

$
0
0
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete usiku wa Ijumaa, Oktoba 23, 2015, amewateua Makatibu Wakuu wanne wapya wa wizara mbalimbali.
 
Aidha, Rais Kikwete amewateua Naibu Makatibu Wakuu wapya watano, amewateua Makatibu Tawala wa Mikoa wawili na pia amewahamisha Naibu Makatibu Wakuu wawili.
 
Kwa mujibu wa uteuzi huo, Rais Kikwete amemteua Ndugu Hab Mkwizu kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma; Profesa Elisante Ole Gabriel kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo; Dkt. Yamungu Kayandabila kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na Mhandisi Omari Chambo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini.
 
Aidha, kwa mujibu uteuzi huo, Rais Kikwete amemteua Mhandisi  Paul M. Masanja kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini; Dkt. Maria Mashingo kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Ndugu Zidikheri  Mgaya Mundeme kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.
 
Wengine walioteuliwa kuwa Naibu Makatibu Wakuu ni Ndugu Tixon T. Nzunda ambaye anakuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Ndugu Emmanuel Kalobelo ambaye anakuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.
 
Walioteuliwa kuwa Makatibu Tawala wa Mikoani Ndugu Eliakim Maswi ambaye anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara na Mhandisi Madeni Kipande ambaye anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi.
 
Katibu Mkuu ambaye anahamishwa ni Bibi Sihaba Nkinga ambaye anakwenda kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Wanawake, Jinsia na Watoto kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
 
Naibu Makatibu Wakuu wanaohamishwa ni Ndugu John T. Mngodo ambaye anahamishiwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kutoka Wizara ya Uchukuzi na Ndugu Mwamini Juma Malemi ambaye anakwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
 
Wateuliwa hao wote wataapishwa asubuhi ya Jumamosi, Oktoba 24, 2015, Ikulu mjini Dar es Salaam.
 
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
24 Oktoba, 2015
 
 

VIJANA WA NCHI MWANACHAMA WA MAZIWA MKUU KUSHUHUDIA MAMBO YA UCHAGUZI MKUU HAPA NCHINI

$
0
0
Balozi wa maziwa makuu nchini Kenya, katika wizara ya mambo ya nje, Muburi Muita,MBS  akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya ushiriki wa vijana katika uchaguzi mkuu utakaofanyika kesho Oktoba 25 mwaka huu pamoja na ushiriki wa vijana katika uchaguzi huo. 
Mwenyekiti wa wa kamati ya uchaguzi wa  vijana wa nchi za maziwa makuu ,Adv.Kabyemela Lushagara akitoa maada katika mkutano wa vijana wa nchi mwanachama wa maziwa makuu pamoja na kuzungumza na baadhi ya vijana wa nchi za maziwa makuu leo katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam kuhusiana jinsi democrsia jinsi ilivyokua hapa nchini na ushiriki wa wapiga kura kesho Oktoba 25 mwaka huu.


Baadhi ya vijana walioshiriki mkutano wa vijana wa nchi za maziwa mkuuu wakimsikiliza mtoa mada leo katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.  
Baadhi ya wadau na vijana wa nchi za mwanachama wa maziwa makuu wakimsikiliza Balozi wa maziwa makuu nchini Kenya, katika wizara ya mambo ya nje, Muburi Muita,MBS  leo wakati akiipongeza Tanzania kuendeleza uchumi pamoja na kushirikiana na nchi mwananchama kuunda uchumi wa nchi Balozi pia alipongeza nchi kwa kukua wa demokrasia 
Balozi wa maziwa makuu nchini Kenya, katika wizara ya mambo ya nje, Muburi Muita,MBS  akiwa katika picha ya pamoja na vijana wa nchi mwananchama wa maziwa makuu  leo jijini Dar es Salam.
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>