Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1008 | 1009 | (Page 1010) | 1011 | 1012 | .... | 3270 | newer

  0 0

   Wananchi wakimshangilia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt.Jakaya Kikwete akizungumza na Maelfu ya wanachama wa chama cha Mapinduzi CCM  na wananchi wa Kisiwani Pemba katika mkutano wa kufunga kampeni za Chama hicho katika uwanja wa Gombani yakale leo   na kuwaombea kura wagombea wote wa CCM
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt.Jakaya Kikwete akizungumza na Maelfu ya wanachama wa chama cha Mapinduzi CCM  na wananchi wa Kisiwani Pemba katika mkutano wa kufunga kampeni za Chama hicho katika uwanja wa Gombani yakale leo   na kuwaombea kura wagombea wote wa CCM
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt.Jakaya Kikwete akizungumza na Maelfu ya wanachama wa chama cha Mapinduzi CCM  na wananchi wa Kisiwani Pemba katika mkutano wa kufunga kampeni za Chama hicho katika uwanja wa Gombani yakale leo   na kuwaombea kura wagombea wote wa CCM. Picha  na Freddy Maro

  0 0

  Mshambuliaji wa JKT Ruvu, Gaudence Mwaikimba akimtoka beki wa Mtibwa Sugar, Adrew Vicent katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka suluhu. (Picha na Francis Dande)
   Mchezaji wa JKT Ruvu, Abdulrahaman Mussa (kulia) akitafuta mbinu za kumtoka Mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Mohamed Ibrahim katika mchezowa Ligi Kuu Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Karume. Timu hizo zilitoka suluhu.  
  Mchezaji wa JKT Ruvu, Abdulrahaman Mussa (kulia) akitafuta mbinu za kumtoka Mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Mohamed Ibrahim katika mchezowa Ligi Kuu Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Karume. Timu hizo zilitoka suluhu.  

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Amos  Makalla leo asubuhi ameshiriki kifungua kinywa na wafanyakazi na wateja waNMB Tawi la Moshi na kuipongeza benki ya NMB kwa kuwa benki 10 bora Afrika mashariki, benki inayoongoza kwa kuwa na matawi mengi nchini, benki inayoongoza kwa kutengeneza faida na kusaidia jamii, benki ya riba na gharama nafuu nchini na benki yenye  huduma bora kwa wateja nchini.


  Pamoja na mafanikio hayo ameishauri benki hiyo kuendelea kuwa wabunifu wa bidhaa na kuendeleza huduma bora hasa katika kipindi hiki cha ushindani.
  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Amos  Makalla kushoto akipata chai asubuhi leo, chai iliyoandaliwa na benki ya NMB tawi la Nelson Mandela Moshi,kulia 

  Meneja wa Tawi hilo 
  Emanuel  Kishosha.

   Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Amosi  Makalla akilishwa keki na mfanyakazi wa benki ya NMB tawi la Nelson Mandela Moshi leo aliposhiriki pamoja katika kifungua kinywa.
   Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Amosi  Makalla akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi pamoja na wateja wa benki hiyo katika tawi l Nelson Mandela.

  0 0

  Description: https://pbs.twimg.com/profile_images/529573534352175104/FGz58F-d.png
  WASANII nguli wa muziki wa Bongo Fleva Ali Kiba kutoka Tanzania na Victoria Kimani kutoka Kenya kesho Jumamosi watawasha moto katika onyesho la muziki la Coke studio linalorushwa na luninga ya Clouds kila siku ya Jumamosi.

  Ali Kiba ambaye anatamba na kwa vibao vyake mbalimbali katika msimu huu wa Coke Studio amefanya Kolabo matata (Mash- up) kwa kushirikiana na mwanamuziki wa kike maarufu kutoka nchini Kenya ,Victoria Kimani.

  Wasanii wengine kutoka Tanzania waliopo kwenye msimu wa tatu wa Coke Studio mwaka huu  ni Ben Pol ambaye alifanya kolabo matata(mash-up) pamoja na  mwanamuziki nguli kutoka Kenya anayejulikana kama Wangechi, Fid Q amefanya bonge la kolabo (mash-up) na Maurice Kirya kutokana Uganda,  na wakati Vanessa Mdee amefanya kolabo matata(mash-up) na  mwanamuziki nguli kutoka nchini Nigeria ajulikanaye kama 2Face.


  Akiongea wakati wa uzinduzi wa onyesho hili hivi karibuni Meneja wa Bidhaa za Coca-Cola Nchini Maurice Njowoka alisema kuwa wasanii nguli kutoka Tanzania wanaungana na wasanii wengine 27 barani Afrika katika msimu wa tatu wa maonyesho ya  burudani ya muziki maarufu kwa jina la  Coke Studio Afrika ambalo linaendelea  kuonyeshwa katika nchi mbalimbali.

  Alisema kolabo ya wasanii 55 itashirikisha wasanii wawili kutoka nchi mbili tofauti kuimba nyimbo mbili za mitindo tofauti. “Mtindo wa Kolabo uliwahi kutumika hapo awali katika maonyesho ya televisheni,sinema na wakati wa kupiga muziki mchanganyiko lakini safari hii unatumika katika onyesho la Coke Studio na utawawezesha wasanii watakaoshiriki kutoka sehemu mbalimbali barani Afrika kuwa wabunifu na kuboresha viwango vyao vya sauti za uimbaji”.Alisema

  0 0

  Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Baraka Luvanda akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mhe. Yasemin Eralp. Mazungumzo hayo yalihusu ukimalishaji wa Makubaliano mbalimbali kati ya Tanzania na Uturuki ili yaweze kusainiwa na kuanza kutekelezwa.
  Balozi Luvanda akisisitiza jambo katika mazungumzo hayo.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

  Na Mwandishi Wetu
  RAIS Jakaya Kikwete ambaye siku chache zijazo atamaliza muhula wake wa pili na wa mwisho wa kuiongoza Tanzania, amewaaga watumishi wa umma nchini kwa kutoa rai kuwa ili kuendeleza mageuzi katika kuwatumikia wananchi ni vyema wakautumia vyema mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).

  Rais Kikwete aliyasema hayo katika sherehe maalum iliyoandaliwa na watumishi wa umma kumuaga na kufanyika Dar es Salaam Alhamisi usiku. Watumishi wa umma walitumia fursa hiyo kumpa Rais tuzo na zawadi mbalimbali na kumshukuru kwa mageuzi makubwa aliyoyaasisi katika kuboresha maslahi ya watumishi na mfumo mzima wa mageuzi.

  Akitaja moja ya mambo ambayo Rais Kikwete atakumbukwa nayo, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alisema kuasisiwa kwa mfumo wa usimamizi na utekelezaji wa miradi wa BRN katika awamu ya pili ya Rais Kikwete kumesaidia kuongeza nidhamu ya utendaji unaopimika na ambao umesaidia kuleta mageuzi makubwa.

  “BRN imeleta nidhamu ya kuweka vipaumbele, kuvifuatilia kwa karibu na kuwawekea watumishi mfumo wa kupimwa kutokana na yale waliyotakiwa kuyatekeleza. Tunakushukuru kwa kuasisi mfumo huu,” alisema.

  Akionekana kufafanua hilo, Rais Kikwete alieleza historia na chimbuko la BRN kuwa ni matokeo ya mafanikio ya ziara zake za nje ya nchi ambapo akiwa Malaysia alijifunza jinsi nchi hiyo ilivyopata maendeleo makubwa na ya haraka kupitia mfumo kama wa BRN.

  “Si vibaya kuiga jambo jema. Niliposikia kuhusu ufanisi wa mfumo huu kule Malaysia niliomba fursa ya kuelezwa zaidi na ndipo nasi tukakubaliana kuuanzisha hapa nchini. Na katika kipindi kifupi zile sekta za mwanzo zilizoingizwa katika BRN utofauti umeanza kuonekana,” alisema Rais Kikwete.

  Akifafanua kuhusu mfumo huo unavyofanyakazi Rais aliongeza kuwa moya ya nidhamu za BRN ni kufanya uchambuzi wa kina wa kimaabara ambapo wataalum wa sekta husika; kutoka sekta za umma na binafsi hukaa pamoja ili kuchambua, kubaini changamoto na namna ya kuzifanyia utatuzi.

  Aliongeza kuwa baada ya kubaini mambo yanayohitaji kufanyiwakazi, mfumo wa BRN unasisitiza katika kuchagua vipaumbele vichache ambavyo hutekelezwa kwa mfumo wenye usimamizi madhubuti, ukomo wa utekelezaji huku pia wahusika wakisaini mikataba ya kuhakikisha malengo waliyowekwa yanatokea.

  “Huu ni mfumo wa utendajikazi ambao kila mmoja wetu anapaswa kuuchukua na kuutumia kuendesha shughuli zake,” alisema Rais huku akitoa mfano wa Mahakama ya Tanzania ambao waliichukua nidhamu BRN katika kupunguza mrundikano wa kesi hata kabla sekta hayo haijaingizwa rasmi katika BRN.

  “Siku moja Jaji Mkuu akaniambia kuwa wameanzisha BRN yao ambapo kila Jaji alipewa lengo na idadi ya kesi za kufanyiakazi kwa mwaka  na kweli baada ya muda mfupi ule mrundikano wa kesi ukapungua sana,” alisema Rais na kusisitiza.

  Sekta za awali zilizoingizwa katika BRN tangu Julai 2013 ni elimu, kilimo, nishati, maji, uchukuzi na ukusanyaji wa mapato. Kutokana na mafanikio yaliyoanza kuonekana katika sekta hizo Julai mwaka huu sekta za afya na uboreshaji wa mazingira ya biashara nazo zimeanza kusimamiwa kupitia mfumo wa BRN.


  0 0

  Afisa vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Godfrey Massawe (aliyesimama) akifuatilia majadiliano ya wawezeshaji kitaifa wakati wa kazi za kikundi kwenye Mafunzo ya Uwezeshaji wa Stadi za Maisha yaliyofanyika Kanda ya Ziwa.


  Na: Genofeva Matemu - Maelezo

  ILIGUNDULIKA kuwa ulimwenguni kote na hususan nchini Tanzania, Vijana walio nje ya shule ni miongoni mwa makundi yaliyo katika hatari ya magonjwa yanayoenea kwa njia ya ngono, VVU na UKIMWI kwa kutokuwa na taarifa na stadi za kuwaongoza hivyo kupoteza kundi kubwa la vijana ambalo ni taifa la kesho.


  Ufumbuzi wa tatizo hili umeweza kufanyika kwa kuwapa vijana stadi za maisha zenye upeo mpana wa maarifa na stadi zinazoweza kuwasaidia vijana kuendana na mazingira shindani yanayobadilika.


  Stadi za maisha ni moja kati ya mikakati iliyobainika kuleta mabadiliko ya tabia za mtu. Stadi hizi uhusisha stadi na uwezo wa kujenga tabia njema ili kuepukana na matatizo yaliyopo katika maisha ya kila siku.


  Mkabala wa stadi za maisha unalenga katika kuendeleza na kukuza stadi zinazoitajika katika mahitaji ya maisha ya kila siku kama vile mawasiliano, kufanya maamuzi, fikra, kuhimili mihemko, uthubutu, ujenzi wa kujiamini, kuzuia shinikizo rika pamoja na mahusiano.


  Mkabala huu pia unashughulikia ukuaji wa mtu ili awe na stadi za kumwezesha kutumia aina zote za taarifa kuhusiana na masuala kama vile magonjwa ya ngono, VVU na UKIMWI.


  0 0

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akifanya ziara ya kukagua maandalizi ya kazi za usafishaji wa karo zinazohudumia uhifadhi ya Uchafu katika Nyumba za Maendeleo zilizopo Mtaa wa Mtemani Mjini Wete Kisiwani Pemba. Kushoto ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mh. Mar Khamis Othman. 
   Mkurugenzi wa Baraza la Mji wa Wete Kisiwani Pemba Ndugu Mgeni Othman Juma akitoa maelezo mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif juu ya hatua zilizochukuliwa katika kufanya usafi wa karo za Nyumba za Maendeleo Mtemani  Mjini Wete.
   Balozi Seif akiushauri Uongozi  wa Wizara ya Ardhi na Makaazi kuandaa utaratibu za kuzifanyia ukaguzi Nyumba za Maendeleo ili kukabiliana na changamoto zinazozikabili Nyumba hizo ikiwemo matengenezo ya kila mara.
  Picha na – OMPR – ZNZ.

  UONGOZI wa Wizara na Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Kisiwani Pemba kwa kushirikiana na Baraza la Mji wa Wete umeanza matayarisho ya kujiandaa na kazi ya usafishaji wa karo zilizotengwa kuhifadhi uchafu unaotoka katika  Nyumba za Maendeleo zilizopo Mtaa wa Mtemani Mjini Wete Kisiwani Pemba.

  Kazi hiyo imeanza kwa hatua ya awali ya uchimbaji  wa mashimo yatakayotumika kufukia mabaki ya uchafu utakaosafishwa kutoka kwenye Karo  Saba  zinazohudumia Nyumba hizo zilizojengwa katika miaka ya sabini.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa Kisiwani Pemba alipata fursa ya kukagua hatua iliyofikiwa ya  kazi hiyo itakayosaidia kuimarisha hali ya usafi pamoja na utunzaji wa  mazingira katika Mtaa huo.

  Mkurugenzi wa Baraza la Mji wa Wete Pemba Ndugu Mgeni Othman Juma alimueleza Balozi Seif kwamba Wananchi wa Nyumba za Maendeleo Mtemani Wete wamewahi kujaribu kufanya usafi katika  eneo hilo bila ya kupata mafanikio yoyote.

  0 0

  Na Father Kidevu Blog
  WANANCHI wilayayani Newala wamehakikishiwa usalama wa kutosha siku ya kupiga kura na kutakiwa kujitokeza kupiga kura na kuwachagua viongozi wao bila wasiwasi wowote.

  Akizungumza na Habarileo kwa njia ya simu, Mkuu wa Wilaya ya Newala, Christopher Magala amesema wakazi wa Newala husususani katika majimbo ya uchaguzi ya Newala Mjini na Newala vijini wasiwe na hofu juu ya amani siku ya kupiga kura.

  “Nitumie nafasi hii kuwatoa hofu wananchi na kuwahakikishia usalama wenu na mali zenu, kwamba siku ya kupiga kura hakutakuwa na vurugu zozote, Hivyo wale wote waliojiandikisha kupiga kura wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura siku hiyo bila wasiwasi wowote,”alisema Magala.

  Magala amesema wananchi waendelea kuilinda na kuitunza amani katika kipindi hiki cha kumalizia kampeni na kipindi chote cha siku ya Uchaguzi na baada ya Uchaguzi pasipo kuvuruga amani na utulivu uliopo Wilayani humo.

  “Katika kipindi hiki cha kumalizia kampeni na kipindi chote cha siku ya Uchaguzi na baada ya Uchaguzi, tuendelee kuitunza amani iliyopo katika Wilaya yetu; upendo na mshikikamano tuliona siku zote tuuimarishe zaidi kipindi hiki ili tuvuke salama na kubaki salama baada ya zoezi la uchaguzi kukamilika,”alisema Magala.

  Aidha amesema Serikali imejipanga vizuri kuimarisha doria katika kipindi cha  siku za mwisho za kampeni, wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi.

  Magala amesema ni haki ya kila mwananchi aliyejiandikisha kupiga kura kutimiza haki yake ya kumchagua kiongozi anayemtaka katika nafasi ya Urais, Ubunge na Udiwani katika mazingira tulivu yasiyo nafujo na hivyo kuwataka wananchi kufanya hivyo na wakishapiga kura warudi majumbani na kusubiri kutangazwa matokeo.

  “Niwatahadharishe, kama wapo, Wananchi wanaokusudia kuvuruga Uchaguzi kwa namna yoyote ile kwamba Serikali haitawavumilia. Hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yao. Vyombo vya Ulinzi vyote vipo ‘standby’ kuhakikisha utulivu unakuwepo wakati wa kwenda kupiga kura na baada ya Uchaguzi kukamilika,”alisema Magala.

  Magala pia amewaomba wananchi kutoa taarifa kwa viongozi watakaokuwa jirani nao au vyombo vyausalama vitakavyokuwa karibu, pale watakapoona dalili zinazoashiria kuvunjika kwa amani na kuwataka wachague viongozi bora, waadilifu, wachapaka kazi, watakao waletea maendeleo katika maeneo yenu ya Kata na Wilaya yetu ya Newala kwa ujumla.

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  OFISI YA WAZIRI MKUU

   TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA  Mkoa wa Dodoma

  Anwani ya Simu REGCOM

  Simu Nambari: 2324343/2324384

  E-Mail No. ras@dodoma.go.tz

  Fax No. +255 026 2320046


      Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,

                              S.L.P.  914,

                                DODOMA.

  Ndugu wananchi wa Mkoa wa Dodoma, tarehe 25 Oktoba, 2015 ni siku ya Uchaguzi Mkuu hapa nchini; ambapo, Watanzania wale wenye sifa za kupiga kura na waliojiandikisha, watapata fursa na kutumia haki yao ya kikatiba kuchagua viongozi mbalimbali wa nchi yetu, kuanzia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge na Madiwani.


  Maandalizi ya kufanikisha zoezi la Uchaguzi Mkuu kwa Mkoa wa Dodoma yamekamilika. Hadi kufikia siku ya leo tayari wasimamizi wa uchaguzi wa wilaya zote saba za Mkoa wa Dodoma wameshapokea vifaa vyote vitakavyo tumika kwenye zoezi la uchaguzi. Hadi tunavyozungumza sasa, vifaa hivyo vinapelekwa kwenye vituo vya kupigia kura.


  Vilevile, wasimamizi wa uchaguzi kwenye wilaya zote saba za Mkoa wa Dodoma wameshapokea fedha za kuendeshea uchaguzi Mkuu.  Aidha, Mafunzo kwa watendaji wote watakaoshiriki katika zoezi la uchaguzi yanahitimishwa kwenye wilaya za Dodoma.


  Mkoa wa Dodoma tumefanikiwa kuandikisha jumla ya wananchi 1,053,136 kuwa wapiga kura sawa na asilimia 102.74 ya lengo, ambapo lengo ilikuwa kuandikisha watu/wapiga kura 1,025,084, Hivyo, natumia fursa hii kuwataka wale wote waliojiandikisha kupiga kura katika Mkoa wa Dodoma, kujitokeza kwa wingi kupiga kura siku ya Jumapili Oktoba 25.


  Vituo vya kupigia kura vitafunguliwa kuanzia saa 1:00 asubuhi na zoezi la kuhesabu kura litaanza saa 10:00 jioni. Natumia fursa hii kusisitiza mambo machache ya muhimu kwenye zoezi la uchaguzi Mkuu mwaka 2015 kwa wananchi wa Mkoa wa Dodoma na wadau mbalimbali wanaoshiriki Uchaguzi Mkuu kama ifuatavyo:

  0 0


  TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

  Kitalu Na. 8, Mtaa wa Luthuli

  S.L.P 2643, DAR ES SALAAM

  Simu: +255 22 2135747/8; 2137125; 2135222

  Faksi: +255 22 2111281

  Tovuti: www.chragg.go.tz


  Oktoba 23, 2015


  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI              
  Tamko la Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kuhusu umuhimu wa kuzingatia sheria kwa ajili ya Uchaguzi Huru, wa Haki na Amani


  TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB)  imekuwa ikifuatilia kwa karibu matamshi mbalimbali ya wanasiasa, viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa Serikali, Tume ya Uchaguzi, na Jeshi la Polisi kuhusu nini kifanyike baada ya kupiga kura siku ya uchaguzi mkuu, Oktoba 25, 2015. Matamshi haya yamesababisha mkanganyiko na malumbano miongoni mwa viongozi na wananchi pia.


  THBUB inapenda kusema kwamba, licha ya changamoto kadhaa zilizojitokeza katika baadhi ya maeneo, wakati wa kampeni za uchaguzi, kwa ujumla kampeni za uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani zimefanyika nchi nzima kwa amani na utulivu. Ni wajibu wetu sote kudumisha amani katika nchi yetu muda wote, wakati wa uchaguzi na baada ya kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu.


  Tume (THBUB) inawashukuru na kuwapongeza wananchi kwa jinsi walivyoonyesha utulivu wakati wa mikutano mikubwa ya kampeni, ambayo imekuwa ikivuta maelfu ya wananchi.


  0 0

   Wakazi wa Ubungo wakimshangilia kwa shangwe mgombea wa Urais kwa Tiketi ya CCM, Dk. Magufuli.
   Wananchi wakiwamtandikia apite.

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI

   WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

  JESHI LA POLISI TANZANIA
           “PRESS CONFERENCE” TAREHE 23.10.2015. 

  NDUGU WAANDISHI WA HABARI,

  TUNAJUA KUWA TAREHE 25 OKTOBA, 2015 NI SIKU AMBAYO TUTASHIRIKI KUPIGA KURA KUWACHAGUA MADIWANI, WABUNGE NA RAIS KWA KIPINDI CHA MIAKA MITANO IJAYO.

   KATIKA KUELEKEA SIKU HIYO, YAPO MAMBO KADHA WA KADHA AMBAYO KILA MMOJA WETU KWA NAFASI ALIYONAYO ANAPASWA KUYAFUATA NA KUYAZINGATIA KWA LENGO LA KUHAKIKISHA UCHAGUZI MKUU UNAKUWA HURU NA HAKI.


  TUTAMBUE KUWA KILA MMOJA WETU ALIYEFIKISHA UMRI WA MIAKA 18 NA KUENDELEA NA ALIYEJIANDIKISHA ANA HAKI YA KUPIGA KURA. NI MUHIMU KUFIKA KATIKA KITUO CHA KUPIGIA KURA UKIWA NA KADI YA MPIGA KURA [SHAHADA YA KUPIGIA KURA] KWA MUJIBU WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI VITUO VYA KUPIGIA KURA VITUFUNGULIWA KUANZIA SAA 07:00 ASUBUHI HADI 16:00 JIONI.


  KILA MMOJA AKUMBUKE KUJIEPUSHA KUFIKA KATIKA KITUO CHA KUPIGIA KURA AKIWA AMEVAA NGUO ZENYE PICHA ZA WAGOMBEA, MANENO AU NEMBO AMA RANGI ZA CHAMA CHA SIASA, KUEPUKA KUTUMIA UVUMI, MANENO YA UONGO, HISIA AU VISINGIZIO VYENYE LENGO LA KUWAZUIA WENGINE KWENDA KUPIGA KURA, KUEPUKA KUFANYA KAMPENI KATIKA KITUO CHA KUPIGIA KURA IWE KWA MANENO YA USHAWISHI AU KWA KUONYESHA ISHARA YA CHAMA FULANI CHA SIASA.


  AIDHA NI VYEMA KILA MWANANCHI KUPIGA KURA KWA KUTUMIA JINA NA KITAMBULISHO CHAKE NA SIO CHA MTU MWINGINE, ALIYEKUFA AU MGONJWA, KUEPUKA KUFANYA FUJO AMA VURUGU KATIKA KITUO CHA KUPIGIA KURA. NI MUHIMU KILA MPIGA KURA MARA BAADA YA KUPIGA KURA KUONDOKA KWENYE KITUO CHA KUPIGIA KURA NA KUENDELEA NA SHUGHULI NYINGINE KWANI NI KOSA KUPIGA KURA NA KUENDELEA KUBAKI KATIKA ENEO LA KITUO CHA KUPIGIA KURA.


  AIDHA NI WAJIBU WA JESHI LA POLISI KUWALINDA MAOFISA WANAOSIMAMIA UCHAGUZI, KUHAKIKISHA KWAMBA ZOEZI LA UPIGAJI KURA LINAENDA SAWA, BILA VIKWAZO AU BUGHUDHA NA KUHAKIKISHA VIFAA VYA KUPIGIA KURA VIKO SALAMA.

  KWA MKOA WA MBEYA TUNA JUMLA YA MAJIMBO 13 YA UCHAGUZI, VITUO 3,899 VYA KUPIGIA KURA, KILA KITUO KITALINDWA NA ASKARI ILI KUHAKIKISHA SUALA LA ULINZI NA USALAMA LINAIMARISHWA KWA KIPINDI CHOTE CHA ZOEZI LA KUPIGA KURA, KUHESABU KURA NA KUTANGAZA MATOKEO YA UCHAGUZI.

  JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LIMEJIPANGA KUIMARISHA ULINZI KATIKA MAENEO YOTE IKIWA NI PAMOJA NA VITUO VYA KUPIGIA KURA. PIA KUTAKUWA NA DORIA ZA MAGARI, PIKIPIKI, MBWA NA ASKARI AMBAO WATAKUWA WAKITEMBEA HUKU NA KULE KWA LENGO LA KUDHIBITI VITENDO VYOVYOTE VYA UVUNJIFU WA AMANI. IELEWEKE KUWA, VITENDO VYOVYOTE VYA UVUNJWAJI WA SHERIA KABLA, WAKATI NA BAADA YA UCHAGUZI NI UHALIFU HIVYO KILA MMOJA AWE MAKINI NA AFUATE SHERIA/TARATIBU NA ATIMIZE WAJIBU WAKE WAKATI WOTE.

  JESHI LA POLISI LINAWATAKA WANANCHI WAHESHIMU MAELEKEZO YA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI. KWAMBA WALE WOTE WATAKAOPIGA KURA NA MARA BAADA YA KUPIGA KURA WAONDOKE MAENEO YA VITUO VYA KUPIGIA KURA WAENDE KUENDELEA NA SHUGHULI ZAO, “WASIKUSANYIKE” WASIWEKE MKUSANYIKO KWANI KWA KUFANYA HIVYO WATAKUWA WANAFANYA MKUSANYIKO USIO HALALI “UNLAWFUL ASSEMBLY” MKUSANYIKO WOWOTE USIOFUATA UTARATIBU HALALI.

  NARUDIA, JESHI LA POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VYA DOLA LIMEJIPANGA VIZURI KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA KATIKA MAENEO MBALIMBALI ILI KUHAKIKISHA ZOEZI ZIMA LINAKWENDA VIZURI, KWA USALAMA NA AMANI NA UTULIVU. KWA HIVYO WANANCHI WOTE WENYE SIFA WAENDE KUPIGA KURA, WASIOGOPE.

  NAOMBA TUELIMISHANE ILI KUEPUKA MAKOSA AMA UHALIFU, KILA MMOJA ANA WAJIBU WA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA ILI KUUFANYA UCHAGUZI UWE WENYE AMANI NA UTULIVU, HURU NA HAKI. NI IMANI YANGU KUWA KUNA MAISHA BAADA YA UCHAGUZI HIVYO TULINDE NA KUTETEA AMANI YA NCHI YETU. 
  AHSANTENI KWA KUNISIKILIZA!


  KATIKA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, MNAMO TAREHE 20.10.2015 MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LILIPOKEA TAARIFA KUWA, MTU MMOJA AITWAYE RAMADHANI JUMA MSUMA @ RAMA BAJAJI (25) MKAZI WA FOREST YA ZAMANI JIJINI MBEYA, ANATUHUMIWA KWA MAKOSA YA MATUMIZI MABAYA YA MTANDAO KWA KUTUMIA PICHA ZA KUZALILISHA WAGOMBEA WA VYAMA VYA SIASA NA KUTOA TAARIFA ZA UCHOCHEZI DHIDI YA VYOMBO VYA DOLA NA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI, KINYUME NA SHERIA.


  NJIA ALIYOKUWA AKITUMIA MTUHUMIWA NI KUTUMIA NAMBA ZA SIMU ZAKE ZA MKONONI ZILIZOSAJILIWA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII @ WHATSAPP, FACEBOOK, INSTRAGRAM NA TWITTER AMBAPO ALIKUWA AKITENGENEZA PICHA ZA UZALILISHAJI NA TAARIFA ZA UCHOCHEZI NA KISHA KUZITUMA KWA NJIA YA MTANDAO KATIKA MAKUNDI MBALIMBALI YA MITANDAO YA KIJAMII TAJWA HAPO JUU.


  AIDHA PICHA HIZO NA TAARIFA HIZO ZINATOA KASHFA KWA WAGOMBEA WA VYAMA VINGINE NA KUTOA VITISHO KWA KUELEKEA UCHAGUZI KWA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI. PIA TAARIFA HIZO NI VIASHIRIA VYA UCHOCHEZI WA VURUGU/FUJO NA UVUNJIFU WA AMANI NA USALAMA HUSUSANI KATIKA KIPINDI HIKI CHA UCHAGUZI MKUU.


  MTUHUMIWA ANAHOJIWA NA PINDI UPELELEZI UKIKAMILIKA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI MARA MOJA KUJIBU MASHITAKA YANAYOMKABILI CHINI YA SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO NA. 14 YA 2015.


  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUWA MAKINI NA MATUMIZI YA MTANDAO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA ZA MATUMIZI SALAMA YA MTANDAO ILI KUJIEPUSHA NA MADHARA YANAYOWEZA KUEPUKIKA HASA KATIKA KIPINDI HIKI CHA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU HAPO OKTOBA 25, 2015.

   Imesainiwa na:
  [AHMED Z. MSANGI – SACP]

  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
  0 0

  Huu ni uchambuzi wa Habari toka vituo mbalimbali vya Televisheni Mchana Huu October 23, 2015.
  Klabu ya soka ya Azam FC imeendelea kukabana koo na Mabingwa wa Ligi kuu soka Klabu Ya Yanga baada ya kufikisha Pointi 19 sawa na Yanga
  Timu Ya soka Ya Stand United ya shinyanga imrjinasibu na kusema wembe ni ule ule wa ushindi ili kushika usukani wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara. https://youtu.be/GDoHdphwLMA
    
  Timu ya Taifa Ya Tanzania Taifa Stars inatarajiwa kuweka kambi ya kujinoa kuikabili Aljeria kwa mtanange wa pili kuwania kushiriki kombe la Dunia.  https://youtu.be/lBtz8cMDX-o
     
  Raisi Kikwete amesema kuwa Mkongo wa Taifa Mawasiliano katika idara za Serikali kumechangia kupunguza mianya Ya Rushwa Nchini. https://youtu.be/7vBg4FRspsA
    
  Waandishi wa Habari Nchini wameombwa kuwa mstari wa Mbele katika kutetea na kulinda amani ya Taifa Uchaguzi Mkuu. https://youtu.be/68BiCiwH6Ac
    
  Wananchi Mkoani Simiyu Wameungongeza Mpango wa TASAF wa Kunusuru kaya masikini kwa kuwa umesaidia walengwa kununua chakula. https://youtu.be/O9-RVyGFkSc

  Wawakilishi wa serikali za mtaa wana wajibu gani katika kuhakikisha maendeleo ya sehemu wanazowakilisha?;https://youtu.be/PwMvBw3TgVs

  Je ni kwa namna gani sera za wagombea mbalimbali zimeweza kumgusa mkulima wa Tanzania na sekta ya kilimo kwa ujumla?; https://youtu.be/R7AGuhXyoIQ

  Hii ndiyo tathmini ya siku za wanasiasa walizojinadi katika majukwaa mbalimbali na mchambuzi huru wa maswala ya katika kampeni zao;  https://youtu.be/OUwRixFpXp0

  0 0

   Katibu Mkuu Kiongozi na Mkuu wa Utumishi wa Umma Balozi Ombeni Sefue akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete orodha ya zawadi mbalimbali kutoka katika taasisi za umma wakati wa sherehe ya watumishi wa umma kumuaga Rais iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam jana.
   Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Dkt.Edward Hosea kwa niaba ya watumishi wa Umma akimkabidhi Tuzo Maalum Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutambua mchango wake katika kuboresha Utumishi wa Umma nchini wakati wa  sherehe ya Watumishi wa Umma Kumuaga Rais iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam jana usiku.
   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania Bwana Awadh Masawe akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mfano wa ufunguo wa trekta alilokabidhiwa na watumishi wa taasisi za umma jana wakati wa sherehe za kumauaga Rais katika ukumbi wa Mlimani City jana.
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete,Katibu Mkuu Kiongozi na Mkuu wa Utumishi wa Umma Balozi Ombeni Sefue,Jaji Mkuu Othman Chande,Mwanasheria Mkuu Mh.George Masaju pamoja Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bwana Florence Turuka wakiwa katika picha ya pamoja na Makatibu wakuu wa Wizara Mbalimbali wakati wa Sherehe ya Watumishi wa Umma Kumuaga Rais iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam jana. 
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia viongozi na wawakilishi wa Watumishi wa Umma katika ukumbi wa Mlimani City wakati wa Sherehe ya Watumishi wa Umma Kumuaga Rais jana.
  (Picha na Freddy Maro).

  0 0    Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na Viongozi wa Taasisi za Kiislamu katika ukumbi wa Baitul-Yamin, Malindi mjini Zanzibar.
   Baadhi ya Viongozi wa Taasisi za Kiislamu Zanzibar wakimsikiliza Maalim Seif.
  (Picha na Salmin Said, OMKR)

  Na: Hassan Hamad, OMKR.
  MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, ameahidi kushirikiana na taasisi zote za dini nchini sambamba na kuziendeleza madrasa za Kur’an, ili ziendane na wakati uliopo.

  Maalim Seif ambaye pia ni Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Wananchi CUF ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na viongozi wa taasisi za Kiislamu katika ukumbi wa Baitul-Yamin Malindi mjini Zanzibar.

  Amesema Serikali atakayoiongoza iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar itashirikiana kwa karibu na taasisi hizo ili kuona kuwa michango yao inasaidia kuchangia juhudi za maendeleo na ustawi wa Zanzibar.


  0 0
 • 10/23/15--06:28: BEI YA MADAFU HII LEO


 • 0 0

   Meneja  wa Mawasiliano  Efm, Denis Ssebo akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya kumpata mshindi wa  shindano la kubuni maneno ya Kanga kupitia kipindi cha UHONDO ambacho huruka hewani kila siku za Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa sita mchana hadi saa tisa alasiri, kikiwa na Matangazaji mahiri Dina Marios, kikao hicho kimefanika leo jijini Dar es Salaam, katikati ni mshindi wa shindano hilo Sekela Richard na wakulia ni Matangazaji wa Efm  Radio Dina Marios.
   Matangazaji mahiri Dina Marios, akimkabidhi kitita cha shilingi Kitanzania milioni moja. mshindi wa shindano hilo, Sekela Richard kulia ni Meneja  wa Mawasiliano Efm, Denis Ssebo.
  Waandishi wa habari wakimsikiliza Meneja  wa Mawasiliano Efm, Denis Ssebo
  Picha na Emmanue Massaka.

  MENEJA  wa Mawasiliano  Efm, Denis Ssebo  shindano hilo halitaishia hapo, kwani baada ya kupata mshindi neno lake la Ushindi  zitatengenezwa  kanga zitakazoandikwa neno hilo ikiwa ni hatua ya pili sasa ya kumwezesha mwanamke kujikwamua kiuchumi.

  Zikishatengenezwa kanga hizo, Efm kupitia kipindi hicho cha Uhondo, itatatoa nafasi kwa  wanawake kutengeneza pesa na kujikwamua kwa kuuza Kanga hizo na  Mwanamke yoyote hasa kwa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani atachukua kanga hizo na kuziuza ambapo kwa kila doti moja ya kanga atapata asilimia 30% ya pesa.

  0 0

  TIMU ya taifa ya mpira wa magongo ya wanawake kesho inacheza mechi yake ya kwanza ya ufunguzi dhidi ya 
  zimbambwe itakayopigwa nchini Afrika kusini,katika mashindano kuwania kufuzu michuano ya Olympic ya mwaka 2016 ambayo itafanyika mjini Rio de Janeiro, nchini Brazil.

  Kocha wa timu ya taifa ya wanawake ya mpira wa Magongo  Varentina Quaranta amesema kwa upande wa wanaume mechi yao ya ufunguzi watacheza na misri siku ya jumapili. 

  Kocha Quaranta ambaye yuko na timu nchini afrika kusini amesema wachezaji wote wako tayari na morali ya kutosha kuelekea katika mashindano hayo,huku pia akitoa shukrani kwa benki ya NMB na baadhi ya wadau wa mchezo huo kwa kuwezesha safari hiyo

  0 0

  Na Mwene Said wa blogu ya jamii, Dar es Salaam.
  George Aloyce Kimaryo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la kusambaza taarifa zauongo kupitia katika kundi la Adios la mtandao wa WhatsApp  kuwa Mwanafunzi  wa Chuo cha DIT,  Benedict Angello  Ngonyani amejitokeza  kwa mara ya pili mahakamani na kuishangaza kwa kumtaka Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange ajitokeze na kukanusha kuwa amelishwa sumu.

  Wakili wa Serikali  Jaquline Nyantori akishirikiana na Wakili Mwandamizi wa TCRA, Johannes Kalungula  walidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa Oktoba 13,2015 katika mtandao huo wa kijamii mshtakiwa huyo alisambaza taarifa hiyo kinyume na kifungu cha  16 cha sheria  ya Mtandao namba 14 ya 2015.

  Baada ya kusomewa shtaka hilo, Mshtakiwa huyo alikana na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi bado haujakamilika na Hakimu Simba aliiahirisha kesi hiyo hadi Novemba 3,2015 kwa ajili ya kutajwa na kufikiria juu ya maombi ya  dhamana.

  Mwanafunzi  huyo  wa Chuo cha DIT,  Benedict Angello  Ngonyani  yeye anakabiliwa na kesi  ya  kusambaza taarifa za uongo kupitia mtandao wa  WhatsApp na Facebook kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange amelishwa sumu.

  Tangu afikishwe mahakamani hapo kwa mara ya kwanza siku 14 zilizopita leo yaani jana ndiyo alipanda kwa mara ya pili  kizimbani mbele ya Hakimu Respicius Mwijage ambapo Wakili Nyantori alidai kuwa kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi wake bado haujakamilika.

  Nyantori alidai katika kesi hiyo, kuwa kesi hiyo inahusisha mtandao bado wanakusanya taarifa ambazo ni za muhimu kupitia mfumo huo.

  Hata hivyo wakili wa kujitegemea, Mnyela Abdallah alijitokeza mahakamani hapo na kujitambulisha kuwa yeye atakuwa wakili wa mshtakiwa huyo atakayemtetea kwenye kesi hiyo na akajulishwa kuwa mteja wake amewekewa zuio la dhamana na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

  Hakimu Mwijage aliuambia upande wa mashtaka kuwa uliweka zuio hilo la dhamana na kutoa sababu ndani ya siku hizo 14  na kuwaambia kuwa sasa kuna umuhimu wa kulijadili dhamana ya mshtakiwa huyo na kitu ambacho kinapelekea andelee kuzuiwa kwa dhamana yake maana lazima kuwepo na sababu hivyo aliwataka  Novemba 3,2015 kesi itakapotajwa kwa ajili ya kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la, waeleze sababu.

  Ngonyani amekuwa ni mshtakiwa  wa kwanza kufikishwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka kupitia sheria hiyo mpya ya mtandao ambayo inazuia mtu yoyote kusambaza ama kuchapisha data, taarifa za uongo, uzushi  na zile ambazo hazijathibitishwa ama hazina chanzo pamoja na  picha za matusi katika mitandao ya kijamii.

  Katika kesi hiyo,  Ngonyani anadaiwa kuwa Septemba 25,2015, jijini Dar es Salaam, alisambaza taarifa za uongo kupitia mitandao ya WhatsApp na Facebook kuwa Jenerali Mwamunyange  amelishwa sumu na kwamba amepelekwa Nairobi Kenya kwa matibabu wakati akijua taarifa hizo zilikuwa na lengo la kupotosha umma.

  Mbali na kesi hiyo, Mshtakiwa  Raia wa China, Royce Lee na raia wa Pakistani Iqbal Wasif na Mohamed Jamil wamepandishwa kizimbani mahakamani hapo wakikabiliwa na kesi tofauti za kuingiza mitambo  ya kielektroniki ya mawasiliano nchini bila ya kuwa na leseni kutoka TCRA, wakaisimika na kutoa huduma za simu za Kimataifa kinyume cha sheria na kuisababishia mamlaka  hiyo hasara ya zaidi ya Sh 500 milioni.

older | 1 | .... | 1008 | 1009 | (Page 1010) | 1011 | 1012 | .... | 3270 | newer