Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1011 | 1012 | (Page 1013) | 1014 | 1015 | .... | 3284 | newer

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA  TANZANIA
  MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA


  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inapenda kutoa taarifa kwa umma kuhusu utangazaji wa matokeo ya Uchaguzi Mkuu kwa vyombo vya utangazaji kwa mujibu wa Kanuni za Huduma za Utangazaji (Maudhui) (Utangazaji wa Uchaguzi wa Vyama vya Siasa), 2015. Kanuni hizi zipo kwa mujibu wa Sheria kama ilivyotolewa na Gazeti la Serikali la Tarehe 26 Juni, 2015. Kanuni hizi zinalenga kuweka utaratibu mzuri wa kutangaza shughuli za kampeni na uchaguzi mkuu kuwa wa amani na utulivu.


  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inapenda kuwakumbusha kuwa ni marufuku kwa vituo vyote vya utangazaji kutangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu bila kupata taarifa sahihi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa utaratibu waliojiwekea.


  Vilevile, vituo vyote vya utangazaji vinapaswa kuzigatia Sheria na Kanuni za Huduma za Utangazaji (Maudhui) (Utangazaji wa Uchaguzi wa Vyama vya Siasa), 2015.


  Kanuni za Huduma za Utangazaji (Maudhui) (Utangazaji wa Uchaguzi wa Vyama vya Siasa), 2015, Na. 16 (1) na 16(2) inaelekeza kama ifuatavyo:-


  16(1) kwamba kila mtoa huduma za maudhui   atakuwa na wajibu wa kuuarifu umma juu ya matokeo ya uchaguzi, kadiri yanavyopatikana.  uangalizi maalumu ufanyike kuhakikisha   usahihi wa matokeo yote   yanayotangazwa.


  16(2) Mtoa huduma za maudhui hatatangaza maoni ambayo yanaweza kuchochea vurugu au kuhamasisha chuki kwa misingi ya mbari, kabila, jinsia, dini au Imani za kisiasa na  ambayo yanajenga uchochezi wa kusababisha madhara.


  Hivyo basi, vituo vya utangazaji vinatakiwa kufuata kikamilifu Kanuni za Huduma za Utangazaji (Maudhui) (Utangazaji wa Uchaguzi wa Vyama vya Siasa), 2015 na kwamba vituo vya utangazaji vitawajibika na matokeo ya maudhui ya matangazo ambayo hayatozingatia Kanuni.


  Mamlaka inatoa wito kwa vituo vya utangazaji kutumia weledi katika maamuzi ya kihariri kuchanganua kipi kinafaa kutangazwa na uangalizi maalumu ufanyike kuhakikisha   kuna usahihi katika kutangaza matokeo yote yatakayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).


  IMETOLEWA NA:

  MKURUGENZI MKUU

  MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

  TAREHE 25/10/2015    

    

  0 0

  SHANGWE za muziki mnene wa 93.7 EFM bado zinaendele. Ijumaa iliyopita ilikuwa zamu ya wakazi wa Tegeta . Burudani ya aina yake ikiongozwa na timu nzima ya EFM ilishushwa ndani ya kimori high way park Tegeta , huku wakazi wa Tegeta wakikutana ana kwa ana na watangazaji na RDJ’s wa 93.7EFM. 
  Burudani ilianza na kabumbu kati ya EFM na Boko beach veteran katika uwanja wa boko beach ambapo EFM waliibuka na ushindi mabao matatu huku Boko beach veteran wakiambulia sifuri. 
  "Muziki mnene bado unaendelea, nawaambia wasikilizaji wetu ambao hatujawafikia wawe wavumilivu na wajiandae kwa kuwa tutawafikia kuwapatia burudani ya aina yake", alisema Dennis Ssebo, Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Mahusiano wa EFM, ambaye pia ni kocha mchezaji.
   Wafanyakazi wa 93.7 EFM walivyojumuika na mashabiki uwanjani kushuhudia mechi kati ya EFM na Boko Beach veteran.

   Timu za 93.7 EFM na Boko Beach veteran katika picha ya pamoja kabla ya mechi kuanza.

   Mashabiki waliojitokeza uwanjani kushudia mtanange huo mkali.

   Nyomi ya wakaazi wa Tegeta walivyojitokeza kula Muziki Mnene ndani ya Kimori Highway Park Tegeta baada ya gemu. Palikuwa hapatoshi!  0 0

  Mgombea urais kwa tiketi ya Tanzania 
  Labour Party (TLP), Maximillian Lyimo.


  Mgombea urais kwa tiketi ya Tanzania Labour Party (TLP), Mhe. Maximillian Lyimo hatimaye amepiga kura yake katika Kituo cha Njia Panda, Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro, baada ya mambo kuwekwa sawa. Awali Mhe. Lyimo alishindwa kupiga kura baada ya kukosekana taarifa zake kituoni hapo.
  Mhe Lyimo aliyejiandikishia mkoani Dar es Salaam, jana alienda kufunga kampeni zake Jimbo la Vunjo na kulala huko. Asubuhi ya leo alienda kituo cha Njia Panda jimboni humo ili akapige kura.
  Baada ya kufika kituoni hapo akiwa na kitambulisho chake cha kupigia kura, alizuiwa baada ya kukosekana fomu namba 19 ambayo kisheria inayomuwezesha mgombea urais kupiga kura ya kumchagua rais kwenye kituo chochote. Baada ya Tume ya uchaguzi kutathmini hali ilivyo na kuridhika ilimruhusu apige kura yake.

  0 0


  0 0  0 0

  Macho na masikio sasa yanaangazia ukumbi wa Julius Nyerere International Convention centre  ambako  kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Uchaguzi Mhe. Kailima Ramadhani ndipo  matokeo ya Rais awamu ya kwanza yataanza kutangazwa leo  Jumatatu saa 4 asubuhi, saa 7 mchana na saa 10 jioni.
   Maandalizi yakiendelea ukumbini hapo
  Jinsi screen za TV zitavyokuwa zikitoa matokeo rasmi

  0 0


  0 0

  Mgombea ubunge Arumeru mbaroni, mamilioni wajitokeza kupiga kura, amani yatawala. Pata habari kutoka magazeti ya leo;  https://youtu.be/K3MJHg68bD4
   Yanga yaja kidigitali, N’daw aishtua Simba, Aveva aamua kuchukua hatua. Ni katika magazeti ya michezo ya leo; https://youtu.be/OxKtrvo9SaM 
   Pata habari motomoto za kisiasa katika magazeti ya leo Jumatatu Octoba 25.2015 hapa Simu.tv; https://youtu.be/GwaPCQlaY7Y

  0 0
 • 10/26/15--01:26: BEI YA MADAFU HII LEO


 • 0 0

  Huu ni uchambuzi wa Habari toka vituo mbalimbali vya Televisheni October 26, 2015.

  SIMUtv: Waangalizi wa ndani wa uchaguzi ambao ni muungano wa Asasi Mbili CEMOT umetoa matokeo ya awali muda mchache baada ya kupiga kura.
  SIMUtv: Tume ya Taifa Ya Uchaguzi Zanzibar imetangaza matokeo rasmi ya majimbo 2 ya ubunge na madiwani katika majimbo ya Fuoni Na Kiembesamaki. https://youtu.be/YKGnxP4NJ2E 

  SIMUtv: Timu ya Manchester City imerejea kileleni katika ligi kuu ya England baada ya Kutoka suluhu na mahasimu wao Manchester United. https://youtu.be/u171GDQ5STY

  SIMUtv: Wananchi wameombwa kuchangia timu ya walemavu ya mchezo wa baisikeli ili kuwawezesha kushiriki mashindano yatakayofanyika afrika kusini; https://youtu.be/9JHWqOV6_0w

  SIMUtv: Hii ndio ripoti kuu ya NEC juu ya matokeo ya uchaguzi wa kura zilizopigwa jana katika uchaguzi mkuu.https://youtu.be/yIgojd11GiM
  SIMUtv: Hii ndio ripoti kuu ya NEC juu ya matokeo ya uchaguzi wa kura zilizopigwa jana katika uchaguzi mkuu Jimbo La Paje. https://youtu.be/gwVbujPU-bY

  SIMUtv: Hii ndio ripoti kuu ya NEC juu ya matokeo ya uchaguzi wa kura zilizopigwa jana katika uchaguzi mkuu Jimbo La Lulindi Mtwara. https://youtu.be/7xUpGeK5LHY

  0 0

  UNGUJA-MAKUNDUCHI
  KUSINI UNGUJA-PAJE
  MKOA-LILUNDI 


  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amewaapisha manaibu katibu wawili wa wizara na Katibu Tawala wa mkoa katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam.Manaibu katibu walioapishwa ni pamoja Ndugu Emmanuel Kalobelo anayekuwa Naibu Katibu mkuu Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia na ndugu Tixon Nzunda nayekuwa Naibu Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
  Katika hafla hiyo Rais Kikwete amemwapisha Mhandisi Madeni kipande kuwa katibu Tawala wa mkoa wa Katavi .
  Naibu Katibu Mkuu Mpya wa Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Ndugu Emannuel Kalobelo akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es salaam leo.
  Naibu Katibu Mkuu mpya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Ndugu Tixon Nzunda akila kiapo mbele ya Rais Kikwete leo.
  Katibu Tawala mpya wa mkoa wa Katavi Mhandisi Madeni Kipande akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es salaam leo na kukabidhiwa miongozo ya kazi.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(wapili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na waliapishwa keo.Kushoto ni Katbu Tawala Mkoa wa Katavi Ndugu Madeni kipande, wanne kushoto ni Naibu katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Ndugu Emmanuel Kalobelo na kulia ni Naibu Katibu Mkuu Mpya Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma Ndugu Tixon Nzunda.
  .(Picha na Freddy Maro).

  0 0


  THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS


  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Joel Laurent kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TEA).  Uteuzi huo ulianza Oktoba 18, mwaka huu, 2015.


  Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Laurent alikuwa Katibu wa Taasisi hiyo ya TEA na ndiye amekuwa anakaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu.


  Imetolewa na:

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  Ikulu,

  DAR ES SALAAM.

  26 Oktoba, 2015.

  0 0

   Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange vitabu kwaajili ya Chuo Cha ulinzi cha Taifa National Defence College(NDC) katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo.Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho cha NDC Meja Jenerali Gaudence Milanzi.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue,Mkuu wa Majeshi ya ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange,Mkuu wa Chuo Cha NDC Meja Jenerali Gaudence Milanzi wakiangali baadhi ya vitabu ambavyo Rais ameviakbidhi kwaajili ya matumizi ya Chuo hicho.

  Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Katibu mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue(watatu kushoto),Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange,(kushoto) na Mkuu wa Chuo cha Ulinzi Cha Taifa(NDC) Meja Jenerali Gaudence Milanzi(kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania muda mfupi baada ya Rais Kikwete kukabidhi vitabu kwaajili ya National Defence College) katika hafla iliyofanyika ikulu jijijini Dar es Salaam leo.
  (Picha na Freddy MRO) 

  THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS


  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo Jumatatu Oktoba 26, 2015, amelikabidhi Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) vitabu kwa ajili ya vyuo vyake na maktaba zake, ikiwa ni mara ya tano kwa Rais Kikwete kulikabidhi Jeshi hilo vitabu wakati wa uongozi wake.


  Vitabu hivyo 384 vilivyokabidhiwa leo vitatumiwa na Chuo cha Ulinzi wa Taifa cha National Defence College (NDC) na wanafunzi wanaosoma katika Chuo hicho chenye hadhi ya kimataifa.


  Mkuu wa Chuo hicho, Meja Jenerali Gaudence Milanzi amehudhuria sherehe ya makabidhiano ya vitabu hivyo ambavyo Rais Kikwete amevikabidhi kwa Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange katika sherehe fupi iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam.


  Hiyo ni mara tano kwa Rais Kikwete na Amiri Jeshi Mkuu kukabidhi vitabu kwa JWTZ katika azma yake ya kuboresha vyuo na maktaba ya vyuo hivyo vya Jeshi. Mpaka sasa, Rais Kikwete amekwisha kabidhi vitabu 3,136 kwa Jeshi.


  Rais Kikwete aliahidi kulinunulia na kulikabidhi Jeshi vitabu (titles) mbali mbali 503 na kufuatia makabidhiano ya leo, sasa vimebakia vitabu (titles) 27 ambavyo navyo tayari vimenunuliwa na vinasubiriwa kusafirishwa kuletwa nchini kutoka vilikonunuliwa.


  Imetolewa na:

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  Ikulu,

  DAR ES SALAAM.

  26 Oktoba, 2015

  0 0


  0 0

   Baada ya mafanikio makubwa 2014, tamasha kubwa la muziki Karibu Music Festival lifanyikalo kila mwaka limerudi tena mwaka huu kwa kishindo kikubwa Novemba hii tarehe 6, 7 na 8.
  Tamasha la Karibu Music Festival hufanyika kwa mfululizo wa siku 3 na litafanyika kwenye viwanja vya Mwakalinga Bagamoyo karibu kabisa na ufukwe wa bahari ya Hindi.

  Mambo mazuri kwenye tamasha hili ni mchanganyiko wa mziki, utamaduni , michezo mbali mbali kutoka kwa wasanii mbali mbali watokao barani Asia, Ulaya , America na Afrika.Moja ya sababu ya kuanzishwa kwa tamasha hili ni kukuza na kutangaza mziki na utamaduni wa Afrika kwa nchi zingine. Miziki yenye asili ya pop, rock, Reggae, Hip Hop Jazz, country hupata umaarufu miongoni mwa wahudhuriaji.
   Mwaka huu watunzi na waimbaji watapata nafasi ya kuuza na kuoromote albam zao, pia wachonga vinyago na wasanii wengine watapata fursa ya kuonyesha kazi zao nzuri kwenye tamasha hili.
  Kaymu Tanzania inakupa nafasi nzuri ya kuhudhuria tamasha hili la kipekee kwani tiketi zitauzwa kwa bei nafuu sana haijawai kutokea.

  Kwa watu 50 wa kwanza watajipatia tiketi kwa Tsh 2,500 badala ya Tsh 5,000


  Nunua tiketi yako kwa kubofya Kaymu.

  Usisahau kumtaarifu na umpendae juu ya jambo hili jema.

  0 0

  Tarehe 22 Oktoba, 2015 Mhe. Balozi Victoria Richard Mwakasege alipata fursa ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Prof. Arthur Peter Mutharika katika Ikulu ya Kamuzu Palace mjini Lilongwe.
  Mhe. Balozi Victoria Richard Mwakasege akipigiwa nyimbo za taifa za Malawi na Tanzania huku akishuhudiwa na maafisa Ubalozi.

  Mhe. Balozi Victoria Richard Mwakasege akikagua gwaride lililoandaliwa kwa heshima yake.
  Mkuu wa Itifaki Bw. Harvey Chigumula akimtambulisha Mhe. Balozi Victoria Richard Mwakasege kwa Mhe. Prof. Arthur Peter Mutharika

  Mhe. Balozi Victoria Richard Mwakasege akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Rais Prof. Arthur Peter Mutharika.

  Mhe. Balozi Victoria Richard Mwakasege akipata picha ya pamoja  na Mhe. Prof. Arthur Peter Mutharika 

  Mhe. Balozi Victoria Richard Mwakasege akiagana na Mhe. Prof. Arthur Peter Mutharika baada ya hafla hiyo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA  0 0


  0 0
  0 0older | 1 | .... | 1011 | 1012 | (Page 1013) | 1014 | 1015 | .... | 3284 | newer