Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1003 | 1004 | (Page 1005) | 1006 | 1007 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali vya Habari katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa Jijini Mwanza katika Semina ya siku tatu (Octoba 19 hadi 22) juu ya VYOMBO VYA HABARI NA UCHAGUZI iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA.

  Wanahabari watapata fursa ya Kujadili yale yanayoendelea katika kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Octoba 25 mwaka huu na nanma Vyombo vya Habari/ Waandishi wa Habari wanavyoripoti habari za Uchaguzi Mkuu kwa kuzingatia haki sawa kwa pande zote ikiwemo wagombea, wapiga kura huku suala la gender balance pia likizingatiwa.
  Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali vya Habari katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa Jijini Mwanza katika Semina ya siku tatu juu ya VYOMBO VYA HABARI NA UCHAGUZI iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA.

  0 0

   Mheshimiwa Naibu Balozi wa Tanzania, London, Mhe. Msafiri Marwa, akizungumza machache kumkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), Bwana Michael P. Mwanda, kuzungumza na baadhi ya Maafisa wa Ubalozi huo. Mwenyekiti huyo wa TPDC, alipata fursa ya kutembelea Ofisi za Ubalozi mara baada ya kumalizika kwa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Baraza la utetezi, ukuzaji na uendelezaji wa shughuli za kiuchumi (Global Local Content Council), kutokana na ugunduzi wa rasilimali za mafuta na gesi katika nchi husika, uliofanyika hapa London (13-15 October 2015), Mwenyekiti Michael Mwanda aliambatana na Mtaalam wa Mafuta na Gesi kutoka TPDC, Engineer Antelimi D nchini Uingereza.
   Naibu Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Msafiri Marwa (kushoto), kwenye picha ya Pamoja na  Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), Bwana Michael P. Mwanda (kati) na Engineer Engineer Antelimi. Ujumbe huo wa TPDC ulitembelea Ofisi hizo za Ubalozi na kupata nafasi ya kuzungumza na baadhi ya Maafisa wa Ubalozi.
  Naibu Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Msafiri Marwa ( wa nne, kushoto), kwenye pichani, pamoja na  Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), Bwana Michael P. Mwanda ( wa nne, kulia) na Engineer Engineer Antelimi (pili kulia). Pichani kutoka kulia ni Bwana Magnus Ulungi (kwanza kulia), dada Isabella Kafumba, Bwana Michael Mwanda, Balozi Msafiri Marwa, Bwana Yusuf Kashangwa, Bwana Allen Kuzilwa pamoja na Kanali Jackson Mwaseba.


  UJUMBE WA TPDC WATEMBELEA UBALOZI

  TANZANIA ilikuwa ni miongoni mwa nchi zilizowakilishwa kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa Baraza la utetezi, ukuzaji na uendelezaji wa shughuli za kiuchumi (Global Local Content Council), kutokana na ugunduzi wa rasilimali za mafuta na gesi katika nchi husika, uliofanyika hapa London (13-15 October 2015)


  Lengo kuu la Baraza hili ni kuzifanya nchi husika zinufaike na rasilimali inayopatikana katika nchi hizo na isiwe ni kwa wawekezaji wa kigeni tu (ambao ndio wenye mitaji na teknolojia ya kutosha inayowawezesha kutafiti na hatimaye kufikia kuivuna rasilimali hiyo).


  Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo uliongozwa na Ndugu Michael P. Mwanda, ambaye ndiye Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC). Wajembe wengine waliokuwa naye mkutanoni ni Engineer Antelimi D. Raphael kutoka TPDC na Yusuf Kashangwa kutoka Ubalozi wa Tanzania hapa London.


  Baada ya Mkutano huo, ujumbe wa TPDC pia uliutembelea Ubalozi na kupata fursa ya kuongea na watumishi juu ya masuala ya msingi yanayoihusu sekta ya mafuta na gesi nchini Tanzania. Ndugu Mwanda alianza kwa kuieleza historia fupi ya utafiti wa mafuta nchini, kwamba ulianza (1954) kabla hata hatujapa uhuru. Hata baada ya Uhuru, utafutaji wa mafuta mafuta uliendelezwa tena kwa bidii zaidi hasa baada ya kuundwa kwa TPDC. Alisema pamoja na lengo kuwa la utafutaji wa mafuta, Tanzania haikuweza na haijaweza kuyapata, na badala yake imefanikiwa kugundua tu gesi.  0 0

  Maalim Seif awaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura siku ya oktoba 25 ili aweze kuwa rais wa Zanzibarhttps://youtu.be/R8WS3XvK1dM  

  Rais mstaafu wa awamu ya pili Mzee Mwinyi awaomba vijana mjini Zanzibar  kutokubali kutumika na wanasiasa kuharibu amani; https://youtu.be/BxVbGJH8ezk  

  Dkt Magufuri azidi kung’ara mjini Mwanza kwa watu wengi kujitokeza na huku akiahidi kuboresha bei ya pamba: https://youtu.be/mQ3jniGJGPc 

  Wanaharakati mjini Arusha waiomba tume ya taifa ya uchaaguzi kufanya uchaguzi kwa uwazi na ukweli ili uwe huru na wa haki: https://youtu.be/SlpOpS5Rmxw

  Mgombea urais Zanzibar Maalim Seif ameahidi kuboresha  mazingira ya wafanyabiashara wakubwa na wadogo iwapo atachaguliwa kuwa rais; https://youtu.be/f3duvz37pF8

  NEC yaeleza sheria za uchaguzi na wajibu wa mpiga kura tayoa tathmini ya muelekeo wa kampeni  na kutoa angalizo kwa wagombea; https://youtu.be/6kyRP10yDCk

   Katika kuelekea uchaguzi mkuu  je ni haki gani za binadamu zinapaswa kuzingatia katika uchaguzi mkuu? Fuatilia hapa;  https://youtu.be/ZGgTuZt1I-o
   Je sheria inasema nini juu ya kukaa mita 200 kutoka kituo cha kupigia kura siku ya uchaguzi mkuu Octoba 25,2015. https://youtu.be/gcb2OQCu9es

  Leo hii katika mjadala. Wataalam wanazungumzia mada ya Kura ya Mtanzania na Tanzania. Endelea kufuatilia hapa; https://youtu.be/zeSaLxZobR8

   Kutana na mgombea ubunge katika jimbo la Ilala kupitia TLP Bw.Salim Bendera katika mjadala; https://youtu.be/w-UBADbLUSM


  0 0

   Wakulima wakifurahia mbegu bora za mahindi, alizeti pamoja na mbolea mara baada ya kukabidhiwa na meneja miradi wa kampuni ya Agrics. Wakulima walionufaika na mbegu hizo ni pamoja na Maswa, Meatu na Shinyanga vijijini.
  Afisa Miradi wa kampuni ya Agrics Ltd, Bwana Semeni Kime (wa pili kulia) akifurahi na wakulima wa kijiji cha Mwakabeya baada ya kuwakabidhi wakulima hao mbegu za mahindi, alizeti pamoja na mbolea kwa ajili ya msimu mpya kilimo.
  Kampuni ya Agrics imetimiza ahadi ya kuwakabidhi mbegu bora za mahindi, alizeti na mbolea wakulima wa Maswa, Meatu na Shinyanga vijijini. Zoezi hili limefanyika kwa wakati kufuatia msimu mpya wa kilimo kutazamiwa kuanza hivi karibuni. Kampuni ya Agrics iliwapa fursa wakulima kuchagua aina ya mbegu wazitakazo ili kuhakikisha wanapata kile wakipendacho. Wakulima wanaendelea kuandaa mashamba yao huku wakiwa huru kabisa kwani tayari Agrics imewapatia mbegu zao kwa mkopo nafuu kabisa na wametanguliza asilimia 25%.  Zoezi la kukabidhi mbegu lilisindikizwa na viongozi mbalimbali wa vijiji ili kuhakikisha wakulima wanajipatia mbegu zao kwa manufaa ya kijiji na mkoa kwa ujumla.


  Kusoma zaidi bofya HAPA.

  0 0

    Umati wa wananchi wa kimara michungwani  wakimsikiliza mgombea ubunge kwa tiketi ya chama cha mapinduzi(CCM) Dkt Fenella Mukangara(hayupo pichani) wakati alipokuwa akinadi sera za chama chake jimboni kibamba.
   Mgombea Ubunge kwa tiketi ya chama cha mapinduzi(CCM)  Dkt Fenella Mukangara akizungumza na wakazi wa kimara michungwani  wakati alipokuwa akinadi sera za chama chake.Dkt Fenella aliwaahidi wakazi hao kuwa wakimchagua atafanikisha kutatua suala la ajira kwa vijana ikiwemo kuwapa elimu ya ujasiriamali, kusimamia tatizo la maji,elimu na afya Bora.

  0 0

  Mgeni Rasmi katika Mahafali ya kwanza ya Shule ya Sekondari Adili High School,Moshono Jijini Arusha,Profesa Raymond Mosha akiangalia kazi zilizoandaliwa na wanafunzi wa masomo ya Sayansi ikiwa ni sehemu ya mahafali ya kidato cha Nne.
  Wazazi wa wanafunzi wanaotarajia kuhitimu Kidato cha Nne wakifatilia kazi za ubunifu zilizoandaliwa kwaajili ya kuonesha uwezo wao katika masomo ya Sayansi kwenye  Mahafali ya kwanza ya Shule ya Sekondari Adili High School.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

  THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
  Miaka 10 inatosha kwa yeyote kutumikia Urais – Rais Kikwete

  ·        Awataka watumishi wa Ikulu kumsaidia Rais ajaye kwa ari na nguvu zaidi kuliko walivyomsaidia yeye.


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa miaka 10 ya uongozi inatosha kabisa kwa mkuu wa nchi kufanya mambo mengi na kuwa hahitaji muda zaidi kuweza kumaliza ajenda yake.


  Aidha, Rais Kikwete amewataka watumishi wa Ikulu kumsaidia Rais ajaye hata kwa ari na nguvu zaidi kuliko hata walimvyosaidia yeye katika miaka yake yote 10 ya uongozi wake.


  Rais Kikwete aliyasema hayo usiku wa  Ijumaa, Oktoba 16, 2015, wakati alipozungumza na watumishi wa Ikulu katika hafla ya chakula cha jioni ambako watumishi hao waliagana na Rais Kikwete ambaye wamemtumikia kwa vipindi tofauti, wengine wakiwa wamekaa naye kwa miaka yote 10 ya uongozi wake.


  Akizungumza na watumishi hao, Rais Kikwete amesema kuwa anaondoka madarakani kwa furaha sana hata kama anaona huzuni kuagana na watumishi hao wa Ikulu ambao amekaa nao kwa miaka mingi, baadhi miaka 10.


  “Kwa hakika, naondoka mwenye furaha sana. Ni kweli nasikitika kuwa tunaachana lakini mambo yote mazuri yana mwisho wake. Nimeifanya kazi ya urais kwa miaka 10, nyie mnajua aina ya kazi hii.

   Miaka 10 ni mingi. Ni miaka inayotosha kabisa kwa mkuu wa nchi kukamilisha ajenda yake. Sidhani kama mtu anahitaji zaidi ya miaka 10 kutekeleza ajenda yake ya msingi,” amesema na kuongeza:


  “Na hata ukitaka kukaa zaidi huwezi kuyamaliza yote. Mzee Nyerere alikaa miaka 23 hakumaliza yote na yaliyobakia alimwachia Mzee Mwinyi ambaye naye alimwachia yaliyobakia Mzee Mkapa. Rais Mkapa naye alifanya mengi lakini hakumaliza yote na akaniachia mimi. Na mimi nitamwachia yaliyobakia Rais ajaye.”


  Kuhusu Rais ajaye ambaye atakuwa mkazi mpya ndani ya Ikulu, Rais Kikwete amesema: “Napenda kuwaombeni msaidieni sana Rais wetu ajaye. Kwa hakika nawaombeni tumsaidie kwa ari na nguvu zaidi kuliko hata mlivyonisaidia mimi.”
  Imetolewa na:

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  Ikulu,

  DAR ES SALAAM.

  19 Oktoba, 2015.

  0 0

  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameeleza mshituko wake mkubwa na huzuni yake nyingi, akiomboleza kifo cha Mbunge wa Ludewa, Mkoa wa Njombe, Mheshimiwa Deo Filikunjombe ambaye alifariki katika ajali ya helikopta usiku wa kuamkia leo, Ijumaa, Oktoba 16, 2015 katikati ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Selous, Mkoa wa Morogoro.

  Katika salamu zake za rambirambi kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Anna Semamba Makinda, Rais Kikwete amesema “Nimeshtushwa mno na taarifa za kifo cha Mheshimiwa Deo Filikunjombe. Kwa hakika, ni msiba ulionihuzunisha sana.”


  Rais Kikwete amemweleza Mama Makinda: “Tumempoteza kijana hodari na mmoja wa wabunge mahiri ambao mchango wao katika Bunge letu tukufu na katika shughuli za uongozi wa nchi yetu na wananchi wake zilikuwa zinajionyesha dhahiri. Ni kifo ambacho kimetuachia pengo kubwa la uongozi na kimetokea wakati bado Bunge lako tukufu, Chama chetu cha CCM na wananchi wa Ludewa walikuwa bado wanahitaji uongozi na mchango wake.”


  Ameongeza Rais Kikwete: “Nakutumia wewe Spika wa Bunge letu tukufu salamu zangu za rambirambi na kupitia kwako kwa Wabunge wote kwa kuondokewa na mwenzao. Aidha, kupitia kwako nawatumia wananchi wa Ludewa salamu zangu nyingi za rambirambi kwa kumpoteza Mbunge wao na aliyewatumikia vizuri na kwa moyo wote kwa kipindi chote cha miaka 10 ya Ubunge wake.”


   Aidha, nakuomba unifikishie pole zangu nyingi kwa familia ya Mheshimiwa Filikunjombe pamoja na ndugu na marafiki wa familia hiyo. Naelewa machungu ya familia kwa kuondokewa na mhimili wao. Wajulishe Wabunge, wajulishe Wana-Ludewa na ijulishe familia ya Marehemu Filikunjombe kuwa niko nao katika maomboleza ya msiba huu mkubwa kwa sababu msiba wao ni msiba wangu.  Napenda pia wajue kuwa naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu aiweke pema peponi roho ya Marehemu Deo Filikunjombe. Amen.


  Wakati huo huo, Rais Kikwete asubuhi ya Jumamosi, Oktoba 17, 2015, ameungana na mamia ya wananchi na waombolezaji kuuaga mwili wa Mheshimiwa Filikunjombe katika shughuli iliyofanyika kwenye Hospitali Kuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Lugalo, mjini Dar es Salaam.  0 0

   Mkurugenzi Idara ya Michezo Bw. Leonard Thadeo (kulia) akizungumza na  Mshauri wa Chama cha Dunia cha Mchezo wa Mpira wa Kikapu (FIBA) Bw. Lubomir Kotleba (kushoto) alipofika nchini Tanzania kufuatilia maendeleo ya mchezo huo jana Jijini Dar es Salaam.
   Mshauri wa Chama cha Dunia cha Mchezo wa Mpira wa Kikapu (FIBA) Bw. Lubomir Kotleba (kulia) akizungumza na maafisa Michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (hawapo pichani) alipofika nchini Tanzania kufuatilia maendeleo ya mchezo huo nchini. Kushoto ni rais wa Mpira wa Kikapu Tanzania Mhandisi John Bandiye.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. MOhammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Jimbo la Mufindi Kaskazini, mkoani Iringa wakati wa mkutano wa Kampeni za mgombea Ubunge wa jimbo hilo, Mohamed Mgimwa, uliofanyika juzi Okt 17.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa Jimbo la Mufindi Kaskazini, Mkoani Iringa wakati alipowasili Jimboni hapo juzi Okt 17, 2015 kwaajili ya kumnadi mgombea Ubunge wa Jimbo hilo, Mohamed Mgimwa.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya MUungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mufundi Kaskazini, baada ya kumalizika kwa mkutano wa kampeni wa mgombea Ubunge wa Jimbo hilo, Mohamed Mgimwa. 
  Picha na OMR

  0 0  MTOTO wa Kitanzania mwenye miaka 14 ametunga kitabu ambacho kimetambulika kimataifa. Kitabu hicho ni cha hadithi kinachoitwa ''LUCIANA AND THE SEVEN MAGICAL RINGS'' ambacho kimepigwa chapa na kampuni ya Kimarekani inayoitwa KIDPUB PRESS ya mjini Boston. Kinasambazwa pia na kampuni za Marekani za Amazon na Bookstore.

  Mtunzi wa kitabu hiki ni Redempta Rugeiyamu ambaye kwa sasa anaishi nchini Afrika Kusini ambaye alizaliwa nchini Botswana walikokuwa wakiishi wazazi wake akiwa na ugonjwa unaoitwa Cerebral Palsy. 

  Amekuwa akiishi na ugonjwa huo tangu alipozaliwa miaka 14 iliyopita. Japokuwa ugonjwa huo umeathiri viungo vyake na kumpa taabu ya kutembea na kuongea lakini haukumzuia ndoto yake ya kuandika vitabu, kuimba na kucheza muziki.

  Kitabu hicho kilizinduliwa mjini Gaborone na Mwenyekiti wa Chama Cha Watanzania waishio Botswana, Bw. Nieman Kissasi, siku ya jumamosi usiku. Mgeni rasmi kwenye shuhuli hiyo alikuwa ni Balozi wa Tanzania nchini Arika Kusini ambaye aliwakilishwa na Afisa wa Ubalozi, Bw. Elibahati Lowassa.
   Mwenyekiti wa Watanzania Waishio Botswana, Bwana Nieman Kissasi, akizindua rasmi kitabu hicho mjini Gaborone siku ya jumamosi usiku kwenye mkutano mkuu wa Chama hicho. Wengine pichani ni wazazi wa Redempta, Bw. Theo Rugeiyamu na Celina Rugeiyamu.

  0 0

   Miss Tanzania 2013/2014 ,Happiness Watimanywa ambaye ni Balozi wa Saratani ya mlango wa kizazi kupia hospitali ya Marie Stopes( kushoto) na  Meneja wa Masoko wa hospitali hiyo Lilian Charles wakiingia kwenye uwanja wa taifa kutoa elimu kuhusiana na ugonjwa wa kansa ya kizazi wakati wa mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kati ya Yanga na Azam, ikiwa nisehemu ya kampeni ya kuhamasisha akinamama kwenda kufanya uchunguzi wa saratani ya Kizazi kwanye vituo mbalimbali vya afya ikiwemo Marie Stopes.Ambapo timu hizo zilitoka sare ya 1-1.
   Balozi wa Saratani ya mlango wa kizazi kupitia hospitali ya Marie Stopes,Miss Tanzania 2013 /2014,Happiness Watimanywa(kushoto)akifafanua jambo kwa  Ofisa wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude(katikati) na Menaja masoko wa hospitali hiyo Lilian Charles(kulia)Kuhusiana na kampeni ya kuwahamasisha wakina mama kufanya uchunguzi wa saratani ya shingo na kizazi katika vituo mbalimbali vya afya. Uhamasishaji huo ulifanyika kwenye uwanja wa Taifa  jijini Dar es Salaa wakati wa mechi ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kati ya Yanga na Azam ambapo timu hizo zilitoka sare ya 1-1.
   Miss Tanzania 2013/2014 ,Happiness Watimanywa,Ambaye ni Balozi wa Saratani ya kizazi kupitia hospitali ya Marie Stopes(watano toka kushoto)akiwa na maofisa wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF pamoja na Ofisa Udhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude(wa kwanza kulia) wakihamasisha kwa wakina mama kujitokeza kwenda kupima saratani ya kizazi katika vituo mbalimbali vya afya wakati wa mechi kati ya Azam FC na Yanga iliyochezwa mwishoni mwa wiki kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo timu hizo zilitoka sare ya 1-1.
  Wachezaji wa timu ya Azam FC na Yanga sports Club wakichuna vikali wakati wa mechi yao ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara iliyopigwa mwishoni mwa wiki ambapo timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.Kabla ya kuanza kwa mchezo huo Balozi wa Saratani ya mlango wa kizazi kupitia hospitali ya Marie Stopes,Miss Tanzania 2013 /2014,Happiness Watimanywa(hayupo pichani)alitumia frusa hiyo ya kuwahamasisha wakina mama kufanya uchunguzi wa saratani ya shingo na kizazi katika vituo mbalimbali vya afya.

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi wa Switzerland katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi.Florence Tinguely Mattli  wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza  na Balozi wa Switzerland katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi.Florence Tinguely Mattli wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
  [Picha na ikulu.]

  0 0

  IMG_6436
  Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) Tanzania, (Ushauri na Miradi), Amon Manyama akitoa maelezo kuhusu mradi wa PEI na salamu kutoka UNDP kwa washiriki wa mafunzo hayo hivi karibuni jijini Mwanza.

  Na Mwandishi Wetu, Mwanza
  MKURUGENZI Msaidizi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Amon Manyama, alisema vita dhidi ya umaskini inakuwa na maana kubwa kama inalinganishwa na mazingira.

  Alisema kwamba umaskini wa kipato ambao umekuwa ukipiganwa sana kwa sasa unastahili kupiganwa kwa kuangalia umaskini kutokana na ukweli kuwa kuboreshwa kwa mazingira ndio hatua kubwa ya kupigana na umaskini katika sura zote zilizobaki.

  Mkurugenzi msaidizi huyo alisema hayo hivi karibuni mjini Mwanza wakati akielezea mradi wa mtaji na elimu wa UNDP ambao umefanyiwa kazi kwa pamoja kati ya shirika hilo, Tume ya Mipango, Hazina na Ofisi ya Makamu wa Rais, katika mafunzo ya siku moja ya Uimarishaji wa Ushirika wa Akiba na Mikopo, yaliyofanyika Mwanza.

  Mradi huo umelenga kuwezesha ushirika wa akiba na mikopo katika wilaya sita nchini kuwezesha wananchi kushiriki katika kukabili umaskini unaosababishwa na mazingira.

  Akifafanua alisema kwamba inawezekana muda wa kusubiri kuvuna samaki ziwani umekwisha kwa hiyo kinachotakiwa kufanyika ni kupanda samaki ndani au nje ya ziwa na watu waweze kutumia nafasi hiyo kuboresha maisha yao.
  IMG_6389
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida akitoa maelezo ya utangulizi juu ya madhumuni ya mafunzo hayo kwa washiriki kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua rasmi.

  Alisema hali hiyo pia ipo katika misitu. Wakati watu wanakata misitu unawapa elimu na mtaji wa kupanda misitu mingine na hivyo mazingira yakaendelea kubaki na kuwa mtaji wa kukabili umaskini.

  Mradi huo ambao upo katika wilaya sita kwa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2021 na ifikapo muda huo utakuwaupo wilaya 21 na kutumika kama kichochea cha utekelezaji wa malengo 17 ya maendeleo endelevu yenye nia ya kupiga vita umaskini, kuondoa ubaguzi na njaa.

  Alisema mafunzo yaliyotolewa katika kongamano la viongozi mbalimbali wa vyama vya ushirika vya aina mbalimbali mjini Mwanza kwa msaada wa UNDP na kutekelezwa na Taasisi ya utafiti wa masuala ya kiuchumi na kijamii (ESRF) yamelenga kuwezesha SACCOS kutambua fursa hizo za mazingira kukabili umaskini.

  0 0


    Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasikiliza wananchi wa jimbo la Buchosa mapema walipokuwa wakishamgilia mara baada ya kupanda jukwaani na kuwasalimia,mkutano huo wa kampeni umefanyika mapema leo asubuhi katika kijiji cha Nyehunge wilayani Sengerema mkoani Mwanza.Pamoja na mvua kunyesha hapa hapa na pale katika maeneo hayo,Dkt Magufuli anatarajia kuhutubia mkutano mkubwa wa kampeni katika jimbo la Geita Vijjini katika kijiji cha Nkome.
    Wakazi wa jimbo la Buchosa wakishangilia jambo wakati Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi mbele yao kuomba kura za kutosha ifikapo Oktoba 25 kwenye uchaguzi mkuu
   Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa jimbo la Buchosa mapema leo asubuhi katika kijiji cha Nyehunge wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
   Wakazi wa jimbo la Buchosa wakishangilia jambo wakati Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi mbele yao kuomba kura za kutosha ifikapo Oktoba 25 kwenye uchaguzi mkuu
  Wakazi wa jimbo la Buchosa wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli uliofanyika mapema leo asubuhi kijiji cha Nyehunge wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli akimnadi Mgmbea Ubunge jimbo la Buchosa,Dkt Charles Tizeba mapema leo asubuhi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Nyehunge wilayani Sengerema mkoani Mwanza
   Magufuli akiwasili kwenye mkutano wa kampeni,Nyehunge jimbo la Buchosa mapema leo mchana huku akishangiliwa .
   Dkt Magufuli akiwasalimia wananchi wa Nyehunge jimbo la Buchoasa kwenye kutano wa kampeni wilayani Sengerema.
  .
   Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Kamanga mapema leo asubuhi aliposhuka akitokea mkoani Mwanza kuelekea wilayani Sengerema kuendelea na Mikutano yake ya kampeni
   Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa kijiji cha Lwezera mara baada ya kupokelewa na viongozi mbalimali wa chama cha CCM mkoa wa Geita,akielekea jimbo la Geita Vijijini kuhutubia wananchi kwenye kutano wa kampeni
   Wanamsikiliza Mgombea Urais wa CCM alipokuwa akimwaga sera zake kwa wakazi wa kijiji cha Lwezera,Geita vijijini.

  PICHA NA MICHUZI JR-SENGEREMA/GEITA

  0 0

  Kipande cha Video ya mahojiano.
   Majaji kwa Upande wa wabunifu wa Mitindo-Mavazi na Upigaji wa Picha wakiwa wanaendelea na kazi za uhakiki wa Majina ya kuwapata washiriki 20 ambao wataingia katika Shindano hilo.
  Mbunifu na Mwanamitindo wa Mavazi ambaye pia ni Balozi wa Fasdo Martin kadinda akiongea kwa niaba ya Majaji upande Majaji wa Mitindo akielezea jinsi mchakato ulivyo kwenda.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0
 • 10/19/15--04:55: BEI YA MADAFU HII LEO


 • 0 0
 • 10/19/15--05:38: SHEREHEKA NA MICHUZI EP 3
 • Kama unataka kusherekea sherehe yako na MICHUZI TV piga simu namba 0714471474 au 0712426666 Pia usisahau kujiunga(Susscribe) na MICHUZI TV Youtube.

  0 0

  Mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Sunrise ya mjini Mwanza Janeth Malima akionyesha kipaji cha kucheza kwenye tamasha la Coke Studio lililofanyika shuleni hapo.

  Wanafunzi wa shule za sekondari za Bwiru na Sunrise wakionyesha vipaji vyao vya kucheza na kuimba wakati wa tamasha la Coke studio.
  Wanafunzi wakifuatilia burudani za tamasha la Coke Studio wakiburudika na kinywaji cha Coca-Cola

  Mwanza,Dar,Mbeya na Arusha waonyesha vipaji vyao  vya kuimba
  Msimu wa Coke studio mwaka huu ambao unajumuisha kolabo ya wanamuziki wa Tanzania na  wanamuziki kutoka nje ambao umezinduliwa mapema wiki iiyopita unazidi kuleta burudani katika makundi mbalimbali ya jamii ambao wanafunzi wa sekondari wamepata fursa ya kushiriki na kuonyesha vipaji vyao vya kucheza na kuimba.

  Katika matamasha yaliyofanyika mwishoni mwa wiki  katika mikoa  ya Arusha,Mbeya,Mwanza na  Dar es Salaam wanafunzi kutoka shule mbalimbali waliweza kushiriki burudani za matamasha ya Coke studio na kuonyesha vipaji vyao vya kuimba na kucheza.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe akiongea na Waheshimiwa Mabalozi wanaowakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali na Wakuu wa Idara/Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje. Wengine katika picha hiyo ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Liberata Mulamula. Waziri Membe aliwataka Mabalozi hao kuhakikisha kuwa mafanikio ya kidiplomasia ambayo Serikali ya awamu ya nne imeyapata yanadumishwa na kuendelezwa katika kiwango cha juu zaidi. picha nyingine ni Waheshimiwa Mabalozi waliohudhuria kikao hicho.
  Mhe. Membe anaonekana akifurahia zawadi ya ramani inayoonesha mandhari mbalimbali za nchi ya Japan. Zawadi hiyo alikabidhiwa na Balozi wa Tanzania nchini Japan, Mhe. Batilda S. Burian.

older | 1 | .... | 1003 | 1004 | (Page 1005) | 1006 | 1007 | .... | 3272 | newer