Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1002 | 1003 | (Page 1004) | 1005 | 1006 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
  Rais Dkt. Jakaya Kikwete amemteua Bw. Awadh Massawe kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).

  Rais alitangaza uamuzi huo Ijumaa iliyopita wakati wa tukio la kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa bandari mpya ya Bagamoyo inayosemekana kuwa kubwa katika ukanda huu wa Afrika mara itakapomalizika.

  Akihutubia wakati wa tukio hilo, Dkt. Kikwete alisema yeye alishamaliza uteuzi huo na kumwambia Bw. Massawe afuatilie tu barua yake rasmi ya uteuzi.

  “Mimi nilishalimaliza hilo, fuatilia tu barua yako ya ajira,” alisema Rais huku akishangiliwa na umati.

  Kabla ya uteuzi huo, Bw. Massawe amekuwa akifanya kazi kama Kaimu katika nafasi hiyo tangu mwezi wa Pili mwaka huu na kufanikiwa hadi sasa kufanya mageuzi makubwa katika kuleta ufanisi katika bandari hapa nchini. 

  Pia kabla ya kukaimu nafasi hiyo, alikuwa Meneja Bandari ya Dar es Salaa.

  Baada ya kuwa Kaimu Mkurugenzi, alianzisha mikutano ya wadau yenye lengo la kurudisha mahusiano yaliyokuwa yameyumba kati ya pande hizo mbili.

  Mikutano hiyo inayofanyika kila Alhamis ya mwisho ya kila mwezi inalenga kuhusisha wadau mbalimbali katika majadiliano ya jinsi ya  kuboresha ufanisi katika bandari ya Dar es Salaam.

  Pia mwisho wa mwezi wa Sita mwaka huu, TPA ilifungua ofisi ndogo katika mji wa Lusaka, Zambia.
  Mafanikio mengine ya hivi karibuni ni kuanza kwa mfumo mpya wa malipo kwa njia ya mtandao katika bandari ya Dar es Salaam.
  Inatarajiwa kuwa baada ya kukamilika kwa ujenzi huo wa bandari ya Bagamoyo unaotarajiwa kugharimu dola bilioni 10, kutaongeza uwezo wa bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara zinazohudumia tani milioni 12 za mizigo kwa mwaka, makasha 6,000 na kuajiri watu 3,200 na vibarua 1,500.
  Bandari hiyo mpya inatarajiwa kuhudumia tani 600,000 za mizigo na makasha 1,000 kwa mwaka na kuajiri watu 1,000.
  Awamu ya kwanza ya mradi huo itahusisha gati nne ambapo mbili kati ya hizo zitatumika kwa huduma ya makasha pekee, moja kwa ajili ya mizigo mingine.
  Tayari TPA iko katika hatua za mwisho kabisa kulipa fidia kwa wanavijiji zaidi ya 2,000 walioachia ardhi yao kupisha mradi huo.
  Mradi huo utatekelezwa kwa makubaliano ya pande tatu za serikali ya Tanzania, China Merchants Holdings International (CMHI) ya China na State Government Reserve Fund (SGRF) ya Oman.

  0 0

   Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam (UDA), Bw. Tumaini Magila (kushoto) akimkabidhi gari namba PT 0828 Toyota Land Cruiser, ASP Charles Hamza (katikati) aliyepokea gari hilo kwa niaba ya Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Pwani, ACP Japhari Mohamed baada ya kazi ya ukarabati wa gari hilo kukamilika.  Tukio hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.  Kulia ni dreva, G. 6633 PC Pendael.

  Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
  KAMPUNI ya Usafiri Dar es Salaam (UDA) imesema itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kusaidia shughuli za kijamii na taasisi mbalimbali likiwemo Jeshi la Polisi ili kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali za kujenga taifa bora.

  Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa kampuni hiyo, Bw. Tumaini Magila amesema hayo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam wakati wakikabidhi gari la Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani ambalo lilifanyiwa matengenezo kwa msaada wa kampuni yao baada ya gari hilo kuwa bovu kwa muda mrefu.

  “Tumekuwa tukishiriki kusaidia masuala ya kijamii yakiwemo ya watoto yatima, na taasisi mbalimbali hapa nchini,” alisema wakati wa makabidhiano ya gari hilo lenye namba PT. 0828 aina ya Toyota Land cruiser.

  Naye ASP Charles Hamza akipokea gari hilo kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani ACP Japhari Mohamed aliishukuru kampuni hiyo kwa msaada huo.

  “Baada ya matengenezo haya, doria zetu zitaimarika,” alisema.

  Alitoa wito kwa jamii na kampuni mbalimbali kuiga mfano wa kampuni hiyo katika kusaidia jeshi la polisi katika changamoto zake mbalimbali ili liweze kuendelea na majukumu yake vizuri.

  Alisema ulinzi wa watu na mali zao ni jambo la msingi ambapo kila mmoja anatakiwa kuunga mkono juhudi hizo ili kutoa fursa kwa jamii, taasisi na kampuni mbalimbali kufanya shughuli za uzalishaji kwa usalama.

  0 0

  Mmoja wa wenyeji wa msafara wa Taasisi ya Kalamu Education Foundation, Ustaadh Thabit pamoja na watoto wakipokea vifaa mbali mbali vya malazi na maji kutoka kwa baadhi ya wajumbe wa taasisi hiyo.
   Mmoja wa wajumbe wa Taasisi ya Kalamu Education Foundation Ndugu Hussein akimkabidhi magodoro Ustaadh Thabit wa kitoa cha elimu cha Irada – Bungu kwa ajiri ya vijana wanaolala hapo kwa masomo ya dini.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

  MGOMBEA Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, ameahidi kuweka mazingira bora kwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu ujao.

  Akiwahutubia wafuasi wa Chama hicho katika mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Kwageji Bububu, Maalim Seif amesema atarekebisha mfumo wa ushuru katika bandari ili kuepusha wafanyabiashara kulipa ushuru mara mbili wanaposafirisha mizigo yao kuelekea bandari ya Dar es Salaam.

  Amesema hali hiyo imekuwa ikiwadhoofisha wafanyabiashara wa Zanzibar, jambo amesema ataliwekea utaratibu mzuri, ili wafanyabiashara waweze kuendesha shughuli zao bila ya usumbufu.

  Akizungumzia wafanyabiashara wadogo wadogo wakiwemo wale wa Jua kali, Maalim Seif amesema atawaekea mazingira mazuri kuweza kufanya shuguli zao.

  Amesema chini ya uongozi wake iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar atahakikisha kuwa wafanyabiashara hao hawanyanyaswi, na watawekewa maeneo maalum ya kufanya biashara zao, na kwamba hakutokuwa na ulipaji wa kodi zisizotambulika katika maeneo yao.

  Aidha ameahidi kuanzisha benki ya uwekezaji, ili kukuza mitaji ya wafanyabiashara wadogo wadogo.

  Nae afisa uchaguzi wa CUF Bw. Muhene Said Rashid, amewataka wanachama hao kuweka utaratibu mzuri wa kuwasaidia wasioweza kupiga kura wakiwemo wagonjwa, wazee na wenye ulemavu,  ili kila aliyejiandikisha aweze kupiga kura kwa mgombea anayemtaka.

  Aidha amewataka kuelimishana juu ya namna ya upigaji kura, ili kuepuka uharibifu wa kura na kupiga kura kwa usahihi.

   Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwahutubia wafuasi wa Chama hicho katika viwanja vya Kwageji Bububu.
    (Picha na Salmin Said, OMKR)

  0 0

   Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mgimwa, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais Dkt. Bilal, kuhutubia wananchi wa Kijiji cha Idetero Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa, wakati wa hafla ya uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Mradi wa Vituo vya Mapumziko na Vyoo vya Wasafiri katika Barabara Kuu nchini, leo Okt 17, 2015.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa kuweka Jiwe la Msingi la wa Mradi wa Vituo vya Mapumziko na Vyoo vya Wasafiri katika Barabara Kuu nchini, wakati wa hafla ya kuweka jiwe la Msingi iliyofanyika katika Kijiji cha Idetero Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa leo, Okt. 17, 2015.
   Picha na OMR

  0 0

   Picha hii kutoka maktaba inamwonyesha mtoto ambaye anatumika kama askari na hivyo kumnyima haki yake ya msingi ya kuishi utoto wake,  pamoja na kupata huduma zake za msingi kama vile afya, elimu, malenzi na ukuaji  wenye hadhi. Pamoja na  Umoja wa Mataifa kuendelea na kampeni yake ya kupinga watoto  kutumika kama askari, bado  taarifa za hivi karibu za Umoja wa Mataifa, zinaeleza kuwa watoto bado wanaendelea kutumika katika baadhi ya maeneo kama askari,  huku wengine wakiingizwa katika  biashara haramu  zikiwamo za ngono.
   Bw. Suleiman Said Ali. Afisa  Mambo ya Nje , Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ( ZNZ) akifuatilia Majadiliano ya Kamati ya Nne ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, iliyokuwa ikijadili kuhusu masuala ya  misaada  ya  ulipuaji wa mabomu ya  Ardhini,  Bw.  Ali pia alishiriki katika Majadiliano ya Umalizwaji wa Ukoloni kwa  Makoloni 17 ambayo bado  hayajapata fursa ya kujitawala na kujiamulia  mambo yake yenyenyewe likiwamo  Koloni la Western Sahara, koloni pekee barani Afrika.

  0 0


  Rais Kikwete akifunua kitambaa ambapo nyuma yake kuna picha ya Jengo la Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje linalokusudiwa kuanza kujengwa hivi karibuni. Rais Kikwete alifunua kitambaa hicho kuashiria kuanza ujenzi wa jengo hilo.
  Mhasibu Mkuu wa Wizara, Bw. Paul Kabale akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya  watumishi wa Kitengo cha Fedha na Uhasibu
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0


   Sony Masamba ambaye ni mmoja wa waimbaji wa Skylight akiendelea kutoa burudani akisindikizwa na waimbaji wenzake jumapili iliyopita.Njoo leo kuona mambo mapya kutoka katika bendi ya Skylight katika kiota cha Escape One.
   Mwimbaji wa bendi ya skylght Natasha akiwa anawapa mashabiki vionjo vya nyimbo za taratibu (kistaarabu) huku akisindikizwa na Sam Mapenzi jumapili iliyopita ndani ya kiwanja cha Escape One Mikocheni. 
  Mashabiki wa Bendi ya Skylight wakiendelea kulisakata Rhumba la nguvu kutoka katika bendi hiyo
  Hii ni moja wapo ya Style mpya ya Bendi ya Skylight kama unataka kuijua basi jisogeze wewe na rafiki yako katika kiota cha Escape One uone mambo mapya kutoka katika bendi hiyo
  Mashabiki wakicheza kwa kuzungusha duala hapa ni kukata mauno mpaka kieleweke

  Mwimbaji wa Bendi ya Skylight,  Sony Masamba akiimba na kucheza na mashabi wao waliofika kijione mziki mkubwa wa bendi ya Skylight ndani ya Kiota Cha Escape One
  Mashabiki na wapendi wa bandi wakiendelea kuserebuka na mziki mkali kutoka katika bendi ya Skylight maana tunasema usisubili kupewa raha jipe raha mwenyewe
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

  Mwanafunzi Fuad Thabit kutoka Feza Boys Secondary aliyeibuka mshindi wa kwanza shule za sekondari katika Shindano la Genius-Cup akipokea cheti na zawadi yake ya shilingi 300,000 toka kwa  mgeni rasmi wa hafla hiyo, Ofisa Mkuu  wa Utafiti taasisi ya COSTECH, Athman Mgumia.


  0 0

   Baadhi ya Wakimbizi kutoka Burundi wakipokelewa katika Kambi ya Wakimbizi ya Nduta, wilayani Kobondo, mkoani Kigoma. Idadi ya wakimbizi kutoka nchini humo inazidi kuongezeka siku hadi siku.
  Watoto wa Wakimbizi kutoka Burundi wakiwa katika Kambi ya Wakimbizi ya Nduta wilayani Kibondo, mkoani Kigoma ambapo wanahifadhiwa. 
  Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.   

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
  Idadi ya raia wa Burundi wanaoingia nchini kutafuta hifadhi ya ukimbizi inazidi kuongezeka siku hadi siku ambapo hadi kufikia tarehe `17 Oktoba, 2015 idadi hiyo ilikuwa imefikia 107,112.


  Raia hawa wa Burundi wanaendelea kuingia nchini kupitia vijiji vya mpakani na wengi wao ni wanawake na watoto kutoka Mkoa wa Makamba nchini Burundi.


  Vijiji wanapoingilia raia hawa kutoka Burundi ni pamoja na Bukililo na Katanga wilayani Kankonko, na Kitanga, Kigadye, Manyovu, Kilelema, Biharu, Migongo na Herushingo wilayani Kasulu.  Kijiji kingine ni Mabamba kilichopo wilayani Kibondo, ambapo wengine hupitia wilayani Ngara mkoani Kagera.

  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) na wadau wengine, imekuwa ikiwahifadhi wakimbizi hawa katika makambi ya wakimbizi ambapo hupatiwa huduma zote muhimu.  Huduma hizo ni pamoja za malazi, chakula, afya, elimu na ulinzi.


  Wakati huo huo, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imeanza zoezi la kuwahamisha wakimbizi wa Burundi waliokuwa wakihifadhiwa kwa muda katika kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu na kuwapeleka katika kambi ya Nduta iliyoko wilayani Kibondo.


  Zoezi hili ambalo limeanza tarehe 04 Oktoba, 2015 linalenga kupunguza msongamano uliokuwapo katika kambi ya Nyarugusu ambayo hadi wakati huo ilikuwa na jumla ya wakimbizi 102,773 kutoka nchini Burundi.


  Tangu zoezi hili lianze, kiasi cha wakimbizi 3,808 kutoka nchini Burundi wameshahamishiwa katika kambi ya Nduta kutoka kambi ya Nyarugusu ambayo  inahifadhi wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).  Kambi ya Nyarugusu ina kiasi cha wakimbizi 60,000 kutoka DRC.


  Zoezi la kuwahamisha wakimbizi hawa kutoka nchini Burundi litaendelea hadi wakimbizi wote kutoka nchi hiyo walioko katika kambi ya Nyarugusu watakapoisha.


  Pamoja na kambi ya Nduta, maeneo mengine yanayoendelea kuandaliwa ili kuwahifadhi wakimbizi hawa kutoka Burundi ni Mtendeli na Karago yaliyoko wilayani Kakonko mkoani Kigoma.

  Aidha, wakimbizi wote wanaoendelea kuingia nchini kutoka Burundi kwa sasa hupelekwa moja kwa moja katika kambi ya Nduta badala ya kambi ya Nyarugusu.


  Imetolewa na Isaac J. Nantanga

  MSEMAJI – WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

  0754 484286

  18 Oktoba, 2015  0 0

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
  *Asihi viongozi, watumishi wa umma wasiache kumuomba Mungu

  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema anamshukuru Mungu kwa kumuwezesha kumaliza salama utumishi wake Serikalini kwenye ngazi za juu ambao umedumu kwa takriban miaka 15.

  Akizungumza na waumini wa Kanisa Katoliki wakati wa Ibada ya Jumapili katika Parokia ya Mt. Anna iliyoko Hananasifu, Kinondoni leo mchana (Jumapili, Oktoba 18, 2015), Waziri Mkuu Pinda amesema anamshukuru Mungu kwa nafasi aliyopewa ya kulitumikia Taifa akiwa Waziri Mkuu kwa miaka minane na miezi tisa; pia katika ngazi ya uwaziri miaka miwili na nusu na miaka mitano akiwa Naibu Waziri.

  “Ninamshukuru Mungu kwa kuniwezesha kumaliza uongozi wangu Serikalini. Ninamaliza uongozi wangu kwa amani na furaha. Katika ibada hii ya shukrani nimemuomba Mungu anisamehe kwa matamshi niliyoyatoa nikiwa kiongozi… yanaweza kuwa yaliwaudhi watu bila mimi kujua,” alisema.

  “Uwaziri Mkuu ni kazi ngumu yenye changamoto nyingi. Nitakuwa mtu wa ajabu nisipomshukuru Mungu kwa uongozi wake katika kipindi chote hicho tangu nikiwa Naibu Waziri hadi kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu,” alisema.

  “Wito wangu kwa Watanzania wote ni kwamba msiache kumtaguliza Mungu maishani kwa sababu yeye ndiye mtoaji wa yote. Wote tuendelee kumtii Mungu na viongozi wetu wa kiroho kwa sababu wako hapa kumwakilisha yeye,” alisema.

  Alisema wako baadhi ya watu ambao wakipata madaraka wanaona kwenda kanisani ni kero au ni kupoteza muda. “Tatizo lao ni kutojijua, hawatambui kwamba bila Mungu hizo nafasi wasingezipata. Ninawaomba tujue kwamba kuna maisha hata nje ya utumishi wa umma na utumishi wa kisiasa,” alisema.

  Alisema katika utumishi wake wa umma amejifunza mambo mengi lakini kikubwa alichobaini ni kujua jinsi ya kuishi na watu. “Elimu kubwa ni kujua jinsi ya kuishi, hii ni elimu zaidi ya kitabuni,” alisema. Alitumia fursa hiyo kumshukru mke wake, Mama Tunu Pinda kwa kuwa nguzo ya familia na kuwalea watoto wote walionao wakati yeye akihangaika na masuala ya kitaifa.

  Katika hatua nyingine, Abate Thadei Mhagama kutoka Abasi ya Hanga iliyoko Songea ambaye aliongoza ibada hiyo, aliwataka waumini wote nchini wazidishe sala kwa kufunga na kuomba katika siku saba zilizobakia kabla ya uchaguzi mkuu kwa sababu hali ni tete.

  “Ninawaomba waumini wote tuzidishe sala ili kwanza pawe na amani na upendo na pia Mungu atuwezeshe kupata viongozi aliowandaa kwa maana ya Rais, Wabunge na Madiwani.”

  “Sote ni mashahidi, tumeona kwenye mikutano kila mgombea akija sote tunajaa huko… hii ni kwa sababu hatujuia yupi ni yupi, ndiyo maana nasisistiza kuwa tumuombe Mungu atuletee yule ambaye amemuandaa,” aliongeza.

  Alisema kila mwananchi amesikia kwamba uchaguzi ukishafanyika awe tayari kupokea matokeo. “Tumeambiwa mara kadhaa tuwe tayari kukubali matokeo… kwa vile tunamuomba Mungu kwa bidii, itakuwa rahisi kukubali hayo matokeo kuliko kwa wale ambao wanaenda bila kuongozwa na Mungu,” alisema.

  “Litakuwa jambo jepesi kwetu kukubali matokeo kwani tutasema Mungu amemleta yule aliyemuandaa, yule ambaye tumekuwa tukimuomba atuletee,” alisisitiza.

  Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Baraza la Walei la Parokia hiyo, Bw. Arbogasti Warioba alisema kama kanisa wao wanamshukuru Mungu kwa ulinzi aliompatia Mhe. Pinda kwa kipindi chake chote cha Uwaziri Mkuu.

  “Sote tunatambua kuwa kazi ilikuwa ngumu, misafara ilikuwa ni mingi na wakati mwingine ya mwendo mkali lakini Mungu alikutetea na kukulinda hadi leo uko salama. Tunakushukuru pia kwa ushirikiano ulioendelea kutuonyesha wakati ukiwa madarakani na tunakuombea uendelee kuwa na uchaji wa Mungu katika maisha yako ya uraiani,” alisema Bw. Warioba.

  (mwisho)

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S.  L. P. 3021,
  11410 DAR ES SALAAM
  JUMAPILI, OKTOBA 18, 2015.

  0 0

  Na Dotto Kahindi

  Kampeni ya uhamasishaji juu ya mabadiliko ya tabianchi kupitia uendeshaji wa baiskeli katika nchi mbalimbali Barani Afrika imeingia Tanzania Octoba 17 kwa waendesha baiskeli 21 kutoka Tanzania kuwapokea wenzao kutoka Malawi.

  Kampeni hiyo ambayo imeanzia Msumbiji, Afrika Kusini, Botswana, Zimbabwe, Zambia, Malawi na hatimaye Tanzania na itatia nanga Kenya mapema mwezi novemba mwaka huu.

  Msafara huo wa waendesha baiskeli kwa Tanzania umeanzia kwenye mpaka wa Tanzania na Malawi wa Kasumulu ambapo unataratia kwenda mpaka Namanga watakapoukabidhi kwa waendesha baiskeli wa Kenya.

  Kwa mujibu wa Meneja Miradi wa shirika la Norwegian Church Aid, Augustina Mosha lengo la msafara huo ni kujenga uelewa kwa jamii juu ya mabadiliko ya tabianchi kwa kutumia vijana kutoka kwenye taasisi za kidini nchini.

  Anasema msafara huo utahusisha pia uchukuaji wa saini za wananchi ili kuweka imani zao kwa viongozi wa kiserikali ambao watakwenda kwenye mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP21 utakaofanyika Desemba mwaka huu huko Paris, Ufaransa.

  Mama Mosha anasema kuwa wameamua kutumia uendeshaji wa baiskeli kama njia ya kuhamasisha jamii juu ya mabadiliko ya tabianchi kwa sababu chombo hicho ni rafiki wa mazingira na hakichangii uzalishaji wa hewa ukaa.
  Picha zote na tabianchi blog
  Waendesha baiskeli kutoka Malawi wakiwasili kwenye mpaka wa Tanzania na nchi hiyo tayari kwa kukabidhi kijiti cha kampeni hiyo kwa wenzao wa Tanzania.
  Mmoja wa waendesha baiskeli Tanzania ambaye pia ni Ofisa Miradi wa Norwegian Church Aid, Tanzania, Gilbert Mworia.
  Meneja Miradi wa shirika la Norwegian Church Aid, Augustina Mosha akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji juu ya mabadiliko ya tabianchi kupitia uendeshaji wa baiskeli.


  0 0

    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Mohammed Gharib Bilal, akimkpongeza Askofu Dkt. Abednego Keshmshahara wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Magharibi, Mkoani Kagera (kushoto) wakati wa sherehe za kuwekwa Wakfu zilizofanyika kwenye Kanisa la KKKT mjini Bukoba, mkoani Kagera leo Okt 18, 2015. Katikati ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Alex Malasusa.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi na Waumini wa dini ya Kikristu, wakati wa sherehe za kuwekwa Wakfu, Askofu Dkt. Abednego Keshmshahara wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Magharibi, Mkoani Kagera, zilizofanyika kwenye Kanisa la KKKT mjini Bukoba, mkoani Kagera leo Okt 18, 2015.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Askofu mpya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Magharibi, Mkoani Kagera,  Dkt. Abednego Keshmshahara (wa pili kushoto) Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Alex Malasusa (kulia) baada ya kukwekwa Wakfu.
   Askofu mpya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Magharibi, Mkoani Kagera,  Dkt. Abednego Keshmshahara, akihutubia baada ya kuwekwa Wakfu. Picha na OMR

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akimkabidhi kombe la Mchezo wa fainali ya Zanzibar Cup 2015 Mpira wa Miguu Nahodha wa Timu ya Wilaya ya Mjini Abubakar  Ameir Omar uliochezwa katika uwanja wa Amaan Studiuam Mjini Unguja jana,Mchezo huo ulimalizika kwa Wilaya ya Mjini kuwafunga W/Magharibi kwa matuta 3-1.
  [Picha na Ikulu.]

  0 0

  Dar es Salaam. Wiki moja kabla ya Uchaguzi Mkuu imebainika kwamba, ili mgombea yeyote wa nafasi ya urais ashinde kiti hicho ni lazima awe na ushawishi mkubwa kwa vijana, hasa wa kike.

  Taarifa iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ikiainisha idadi ya watu waliojiandikisha kiumri, inaonyesha kuwa asilimia 57 ya wapigakura wote waliojiandikisha na kuthibitishwa kupigakura Oktoba 25, wana umri chini ya miaka 35.

  Taarifa hiyo ambayo imewagawa wapigakura wote 22.75 milioni kwenye makundi matatu; miaka 18 mpaka 35; 36 mpaka 50 na 51 na kuendelea, inaonyesha mshindi wa urais ni lazima alishike kundi hilo ili aibuke kidedea wakati kinyang’anyiro hicho kitakapokuwa kinahitimishwa.

  Taarifa hiyo ambayo imewagawa wapigakura wote 22.75 milioni kwenye makundi matatu; miaka 18 mpaka 35; 36 mpaka 50 na 51 na kuendelea, inaonyesha mshindi wa urais ni lazima alishike kundi hilo ili aibuke kidedea wakati kinyang’anyiro hicho kitakapokuwa kinahitimishwa.

  Kati ya wapigakura wote waliopo, vijana wenye umri kati ya 18 na 35 ni 12,894,576. Kati yao wanaume ni 6,155,613 (asilimia 27) na wanawake ni 6,738,964 ( asilimia 30) ya wapigakura wote waliojiandikisha mwaka huu.

  Hii ina maana kwamba, endapo kundi hili lote litamuunga mkono mgombea mmoja na kumchagua, basi atashinda kwa asilimia 57 na ambazo haziwezi kupatikana kwa rika nyingine zilizobaki.

  Takwimu hizi zinadhihirisha mikakati ya ziada, ambayo vyama husika inatakiwa kuwa nayo ili kuongeza wafuasi na kujihakikishia ushindi.
  Mchanganuo huo unaonyesha zaidi kuwa watu wa rika ya kati, kati ya miaka 36 mpaka 50 hawafiki hata nusu ya vijana hawa, kwani wapo 5,690,668. Hiyo ni asilimia 25 ya wote waliojiandikisha. Wao wanajumuisha wanaume 2,744,422 (asilimia 12) na wanawake 2,946,247 (asilimia 13) ya wapigakura wote.

  Makundi haya mawili pekee yanatengeneza asilimia 82 ya wapigakura wote huku asilimia 18 zinazosalia yaani wapigakura 4,165,544 zikiwa ni za wazee.
  Kwa wazee hawa, wamo wanaume 1,900,555 au asilimia nane ya wanawake 2,264,990 ambao ni asilimia 10.

  Akizungumzia takwimu hizo, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), Dk Benson Bana alisema kuna haja kwa washauri na wagombea kuzitumia vizuri taarifa hizi katika kunadi sera zao, kwani kila kundi lina mahitaji yake maalumu na ndani yake pia yapo madaraja.

  Alifafanua kwamba haitoshi kusema vijana au wanawake wanajitokeza kwa wingi bila kueleza ni kwa namna gani kero zao zitataliwa, endapo chama au mgombea husika atapewa ridhaa na kundi hilo.

  “Ni vigumu kutabiri misimamo ya kiitikadi ya kundi hili. Inaweza kuwa rahisi kujua wanafunzi wa vyuo wanahitaji nini kwa sababu mawazo na mitizamo yao ni kama huwa inafanana, lakini haiwezekani kwa wale wanaofuga, kulima au waliojiajiri.

  Ni muhimu sera zikabainisha zitafanya nini na wajane, wasio na ajira, wajasiriamali na makundi mengineyo ndani ya lile la vijana,” alisema Dk Bana.

  Profesa Gaudence Mpangala wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ruaha (Ruco), alisema kuna umuhimu wa kila kundi kushiriki kwa mapana kwenye mchakato wa uchaguzi ili kuwa na nafasi nzuri ya kufanya uamuzi unaostahili. Alisema ingawa ipo dhana, inayohitaji kufanyiwa utafiti, kwamba wanawake wanaipenda CCM na vijana upinzani bado haitoshi kujiaminisha juu ya ushindi.

  0 0

  Meza kuu kutoka kushoto ni Bi. Jennifer Jones ambaye ni ni mkuu wa Kamisheni ya wanawake kaunti ya Prince George, Afisa Suleiman Saleh ambaye alimwakilisha Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi. Kulia ni Dr. El Senzengakulu Zulu ambaye ndio mwanzilishi na mmiliki wa shule ya Ujamaa inayofundisha tamaduni za bara la Afrika. PICHA NA KWANZA PRODUCTION/VIJIMAMBO BLOG.
  Kutoka kushoto ni Dr. John Rutayuga ambaye ni mwanzilish wa Ukwimwi Orphans akiwa meza kuu na Mr and Mrs William.
  Mshereheshaji Tuma akifungua pazia ya kuashiria SHINA Gala imefunguliwa rasmi siku ya Jumamosi Octoba 17, 2015 ndani ya Hotel ya Hilton iliyopo Greenbelt, Maryland na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali Watanzania na marafiki zao wakiwemo wawakilishi wa makampuni yanayoshirikiana na SHINA kwa ajili ya kusaidia misaada mbalimbali ikiwemo ujenzi wa shule nchini Tanzania. 
   Kikundi cha sanaa cha Taratibu Youth Association kikifungua pazia la burudani hku wakishangilia muda wote kwa umahiri wao wa kucheza ngoma za asili kutoka Tanzania. Kundi hili hupata mialiko mabara mbalimbali kujifunza na kufanya maonesho ya ngoma za asili ambazo hua kivutia kwa watazamaji.

  0 0

  Mwanafunzi Fuad Thabit kutoka Feza Boys Secondary aliyeibuka mshindi wa kwanza shule za sekondari katika Shindano la Genius-Cup akipokea cheti na zawadi yake ya shilingi 300,000 toka kwa mgeni rasmi wa hafla hiyo, Ofisa Mkuu  wa Utafiti taasisi ya COSTECH, Athman Mgumia.
  Wanafunzi Sita Washindi wa Shindano la Genius-Cup (mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na vyeti vyao mara baada ya kuibuka washindi. Nyuma yao ni meza kuu katika hafla ya kuwazawadia ikipata picha ya ukumbusho na mabingwa hao. 
  Baadhi ya wanafunzi walioingia fainali katika shindano la kuwatafuta washindi wa shindano la Genius-Cup wakifuatilia hafla hiyo jana.

  WANAFUNZI Sita walioibuka mabingwa wa Shindano la Genius-Cup la masomo ya sayansi na hisabati wamezawadiwa zawadi zao jana katika fainali za mashindano hayo zilizofanyika katika Shule ya Wavulana ya Feza Sekondari iliyopo Tegeta Jijini Dar es Salaam.


  Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mara baada ya kumalizika kwa shindano hili, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Feza, Ibrahim Yunus alisema wanafunzi sita walioibuka washindi na kupatia vitita vya fedha ni pamoja na Fuad Thabit mshindi wa kwanza kutoka Feza Boys Secondary aliyejipatia shilingi 300,000 na Zulfa Khamis msindi wa pili toka shule za sekondari Mkoani Tanga aliyejishindia shilingi 200,000.

  Bw. Yunus alimtaja mshindi mwingine wa kwanza shule za msingi ni Mvano Michael Cabangoh kutoka shule ya Green Acres aliyejishindia shilingi 300,000 na Shammah Kiunsi mwanafunzi wa shule ya msingi kutoka Mkoa wa Mbeya aliyejishindia kitita cha shilingi 200,000 pamoja na Dorice Ernest Msafiri mshindi wa tatu (msingi) kutoka Mkoa wa Dodoma Ignatius School aliyejinyakulia shilingi 150,000/-.

  Akifafanua zaidi Mwalimu Mkuu wa Sekondari ya Wavulana ya Feza, Bw. Yunus alisema wanafunzi walioingia fainali na kukutanishwa kwa pamoja ni 70 kati ya wanafunzi 1,486 walioshiriki katika kinyang'anyiro hicho. Aliongeza kuwa hii ni mara ya pili shindano la GENIUS CUP linafanyika kwani kwa mara ya kwanza lilifanyika mwaka jana huku likilenga kukuza mapenzi ya masomo ya sayansi na hisabati kwa wanafunzi wa Tanzania.

  Kwa upande wake Ofisa Mkuu wa Idara ya Elimu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Fredrick Shuma akizungumza kabla ya kukabidhi vyeti kwa wanafunzi washindi aliupongeza uongozi wa shule za fedha nchini kwa kuliendeldeza shindano hilo kwani linachangia kuleta chachu ya mapenzi kwa masomo ya sayansi na hisabati kwa wanafunzi nchini Tanzania ambao wamekuwa wakiyaogopa masomo ya sayansi.

  0 0

   Bando la kumkaribisha Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia Suluhu Hassan,likiwa limeshikwa na wananchi katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine mjini Sumbawanga mkoani Rukwa  leo
   Chopa iliyomsafirisha Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan ikiwasili katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Sumbawanga mkoani Rukwa leo, ambako mgombea huyo alihutubia mkutano mkubwa wa kampeni.
   Chopa iliyomsafirisha Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan ikiwasili katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Sumbawanga mkoani Rukwa leo, ambako mgombea huyo alihutubia mkutano mkubwa wa kampeni.
   Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia suluhu Hassan akisalimia wananchi baada ya kuwasili kwa Chopa kuhutubia mkutano wa kampeni leo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Sumbawanga.
  PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO.

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso akizungumza kabla ya kukabidhi darasa la awali ‘Chekechea’ lililokarabatiwa kwa hisani ya Wafanyakazi wa Airtel kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Kumbu Kumbu iliyopo Block 41, jijini Dar es Salaam jana. 
   Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso akikata utepe kama ishara ya kukabidhi darasa la awali ‘Chekechea’, lililokarabatiwa kwa hisani ya Wafanyakazi wa Airtel kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Kumbu Kumbu iliyopo Block 41, jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Priscilla Moshi (wa pili kushoto), Mwenyekiti wa Shule, Mwemba Mwilima (wa tatu kushoto), Wafanyakazi wa Airtel na watoto wa chekechea.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kulia), Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kumbukumbu, Priscilla Moshi (kushoto) na Mkurugenzi wa Raslimali Watu wa Airtel Tanzania, Patrick Foya (wa pili kulia), wakiwa na watoto wa Chekechea, baada ya kukabidhi darasa la awali ‘Chekechea’, lililokarabatiwa kwa hisani ya Wafanyakazi wa Airtel kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika shule hiyo iliyopo Block 41, jijini Dar es Salaam jana.
   Wafanyakazi wa Airtel wakifurahi na watoto wa Chekechea katika Shule ya Msingi Kumbukumbu, baada ya kukabidhi darasa la awali ‘Chekechea’, lililokarabatiwa kwa hisani ya Wafanyakazi hao, kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika shule hiyo iliyopo Block 41, jijini Dar es Salaam jana.
   KAMPUNI  ya Simu za mkononi ya Airtel Tanzania kupitia kampeni yao ya “Airtel Tunakujali” inayoendeshwa na wafanyakazi wake imekabidhi darasa kwa shule ya msingi kumbukumbu Jijini Dar es Salaam ambalo imelikarabati kwa ajili ya wanafunzi wa awali maarufu kama chekechea.

  Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania Sunil Colaso alielezea umuhimu wa ukarabati wa darasa la chekechea kwa wafanyakazi wa Airtel.

  Leo Airtel, kupitia mpango wetu wa “Airtel Tunakujali", tunatimiza dhamira yetu tuliyotoa ya kuwezesha shule ya msingi Kumbukumbu kuwa na uhakika na mazingira salama ya kusomea kwa wanafunzi wawapo hapa shuleni.

                                                                                                                                 
  Kwani elimu bora huanzia kwenye hatua ya awali hivyo ukarabati wa darasa hili utakuza chachu ya wanafunzi hawa wadogo kujijengea mazingira ya kupenda kusoma wakiwa wakubwa”.

  Akifafanua amesema, “wanafunzi wanapokuwa shuleni walimu huwa watu muhimu sana kwao, kwani huwafundisha watoto misingi bora ya kuishi hapa duniani, ambapo uwepo wa mazingira mazuri ya kufundishia huwapa morali walimu.

  Ushirikiano wetu na shule ya msingi Kumbukumbu hautaishia hapa kwani tumepanga kuiwezesha ili iwe shule bora ndani ya manispaa ya Kinondoni na taifa kwa ujumla” aliongeza.

  0 0

  ufafanuzi na jinsi ambavyo Kamati ya Maadili ya vyama vyenye wagombea Urais Taifa Ilivyo shughulikia malalamiko toka kwa Mgombea Mwenza wa CHADEMA Ndg J. Duni , kwamba Tume ya taifa ya Uchaguzi imeandaa Vituo vya wapiga kura HEWA zaidi ya 20,000.
  Viambatanisho 
  1. Maamuzi ya Kamati 
  2. Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Hamid Mahmoud Hamid

older | 1 | .... | 1002 | 1003 | (Page 1004) | 1005 | 1006 | .... | 3286 | newer