Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110019 articles
Browse latest View live

PAPA WEMBA KUTUMBUIZA TAMASHA LA KARIBU MUSIC FESTIVAL NOVEMBA 6-8 MWAKA HUU

$
0
0
 Ofisa Mauzo wa Karibu Cultural Promotions Organization (KCPO), Ernest Biseko katikati  ambao ni waratibu wa Tamasha la Karibu Music Festival akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. kushoto ni  ni msanii, Jhikolabwino Manyika - Jhikoman na Meneja Uvumbuzi wa kinywaji cha Jebel cha Kampuni ya SBL, Attu Mynah
 Msanii Jhikolabwino Manyika - Jhikoman   wasanii wa Tamasha la Karibu Music Festival walivyojiandaa na  akionesha umahiri wake wa kupiga gitaa mbele ya waandishi wa habari  leo jijini dar es saalam
 Baadhi ya waandishi wa  habari
Jhikolabwino Manyika - Jhikoman (kulia) akionesha ufundi wake wa kuimba na gitaa kwa wanahabari leo baada ya mkutano.
Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.

MWANAMUZIKI nguli wa dansi kutoka nchini Congo DR, Papa Wemba ni miongoni mwa wasanii wanaotarajia kutumbuiza katika tamasha kubwa la Kimataifa la Muziki la 'Karibu Music Festival' linaloratibiwa na Karibu Cultural Promotions Organization (KCPO) na Legendary Music Entertainment and Promotions Co. Ltd. 

 Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Ofisa Mauzo wa KCPO, Ernest Biseko alisema wanamuziki wengine na bendi zinazotarajia kutumbuiza katika tamasha hilo ni pamoja na Sarabi Band, H-Art The Band, Yuzzo & Frontline Band. 

Alisema wasanii kutoka Tanzania watakaotumbuiza ni pamoja na Jhiko Manyika (Jhikoman) na band yake ya Afrikabisa, Tomgwa Ensembe, Misoji Nkwambi mshindi wa BSS 2008, Ze Spirit. 

Isha Mashauzi, Damian Soul na babd yake, Juma Nature, Msafiri Zawose na band yake. Akifafanua zaidi Biseko alisema tamasha hilo la mwaka huu lenye kauli mbiu ‘Fahari ya Tanzania’ litafanyika kwa siku tatu mfululizo kuanzia Novemba 6 hadi 8 mwaka huu katika viwanja vya Mwanakalenge karibu na Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA). ".

Tamasha hili linalenga kukuza muziki wa Kiafrika na kuonesha tamaduni za Kiafrika kwa dunia nzima kupitia jukwaa la muziki litakalokutanisha wanamuziki kutoka sehemu mbalimbali duniani," alisema Biseko.

 Aidha alibainisha kuwa tamasha hilo ni sehemu ya kukutanisha wadau wote wa muziki kutoka dunia nzima, kubadilishana uzoefu wa kikazi na kufungua milango kwa wasanii kukuza mtandao wa marafiki na kujifunza vitu vipya toka wasanii wa je ya Nchi. Aliongeza kuwa wanamuziki wote watakaopanda jukwaani siku zote tatu za tamasha watatumbuzia na vyombo vyao 'live' na hakutakua na kutumia CD (playback). 

SERIKALI YATAKIWA KUKABILIANA NA VIASHIRIA VYA UVUNJIFU WA AMANI

$
0
0
Na Woinde Shizza,Arusha
Kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Octoba 25 mwaka huu Serikali imetakiwa kukabiliana na viashiria vya uvunjifu wa amani na kuvipatia ufumbuzi ili kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki utakaodumisha amani ya taifa.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Amani ya Apet Jijini Arusha Peter Aham  katika mjadala wa masuala ya amani hasa katika kipindi cha uchaguzi ulioudhuriwa na Wawakilishi kutoka tume ya uchaguzi,Jeshi la Polisi,Vyama vya Siasa pamoja na wadau wa amani.

Peter Ahham amesema kumekua na dalili za wazi za baadhi ya mamlaka kuonekana kuegemea upande mmoja ikiwemo Tume ya Uchaguzi,Jeshi la Polisi na baadhi ya Vyombo vya habari jambo ambalo linapingana na taaluma na weledi  na linaweza kuathiri amani.

Mkuu wa wilaya ya Arusha Fadhili Nkulu amesema kuwa kwa muda mrefu amani iliyodumu nchini imekua ikihatarishwa na masuala ya udini,ukabila na itikadi za kisiasa hivyo kila mtanzania anajukumu la kulinda amani katika kipindi hiki cha uchaguzi

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la Kiserikali la USIP ,Dr.James Jesse pamoja na Kamishna wa Polisi mkoa wa Arusha  Edward Balele amesema kuwa kila mtanzania,vyama vya siasa vinawajibu wa kulinda amani na kuhakikisha kuwa uchaguzi unakua huru na salama

Siku chache zimesalia kufikia Octoba 25 ambapo uchaguzi mkuu wa kitaifa unatarajia kufanyika ambapo Watanzania watapata viong ozi wapya kuanzia ngazi ya Urais ,Ubunge na Udiwani huku suala kubwa linalogonga vichwa vya watu wengi ni juu ya uwepo wa haki na amani katika uchaguzi huo.

UCHAMBUZI WA HABARI ZA MAGAZETI OKTOBA 20,2015

$
0
0
Kesi ya mita 200 ya uchaguzi mkuu kuanza leo. Pata habari motomoto zilizopamba kurasa za magazeti ya leo; https://youtu.be/NbbanyVNgHg

Dk.Magufuli asema mabadiliko sio kuzungusha mikono, vyama vinavyounda UKAWA wasitisha kampeni; https://youtu.be/47_EU73pBfQ

Tume yatoa muongozo wa upigaji kura. Mabilioni ya Mbowe yaivuruga CHADEMA. Pata habari katika dondoo za magazeti ya leo; https://youtu.be/eFvmJ9YAsyk 

Taifa Stars kuiendea Algeria ng’ambo, Bin Zubeity avutwa TFF. Ligi kuu yapisha uchaguzi mkuu.Ni katika magazeti ya leo;   https://youtu.be/dM0CCFihJ4s

Samia afuta nyayo za Lowasa Mbeya. Dk.Dau aweka historia NSSF, NSSF yajenga daraja la kihistoria Kigamboni;https://youtu.be/z-nhKJGpXeA

SHEREHEKA NA MICHUZI EP 4

$
0
0
Kama unataka kusherekea sherehe yako na MICHUZI TV piga simu namba 0714471474 au 0712426666 Pia usisahau kujiunga(Susscribe) na MICHUZI TV Youtube

RAIS KIKWETE AFUNGUA KITUO CHA MICHEZO KIDONGO CHEKUNDU

$
0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa Ufunguzi wa Kituo cha michezo cha Jakaya M.Kikwete Youth park huko Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe  katika ufunguzi wa Kituo cha michezo cha Jakaya Kikwete Youth park huko Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akicheza mpira na baadhi ya watoto wanaopata mafunzo ya michezo katika kituo hicho kinachofunza mpira wa miguu,kikapu na volleyball ya ufukweni.
(Picha zote na Freddy Maro)

BEI YA MADAFU HII LEO

NDESAMBURO AMUOMBEA KURA MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MOSHI

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Moshi mjini aliyemaliza muda wake ,Philemoni Ndesamburo,akimnadi mgombea Ubunge katika jimbo hilo Jafary Michael (Chadema) katika mkutano wa kampeni uliofanyika jana katika kata ya Ngangamfumuni.
Baadhi ya wananchi wakiwa kando ya barabara wakifuatilia mkutano huo.
Mgombea Ubunge jimbo la Moshi mjini kupitia Chadema,Jafary Michael akiomba kura wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika kata ya Ngangamfumuni mjini Moshi.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,kandaya Kaskazini.

KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

SEMINA YA TAMWA KWA WANAHABARI KANDA YA ZIWA YABAINI WAGOMBEA WANAWAKE KUSAHAULIKA.

$
0
0
Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali vya Habari katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa Jijini Mwanza katika Semina ya siku tatu iliyoanza jana Octoba 19 na inatarajia kufika tamati kesho octoba 22 ikiangazia juu ya VYOMBO VYA HABARI NA UCHAGUZI iliyoandaliwa na Chama cha cha Wanahabari Wanawake nchini Tanzania (TAMWA-Tanzania Media Women Association).


Katika Semina hiyo, imebainika kuwa katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu, Vyombo vya Habari na Waandishi wa Habari hawajaweka kipaumbele katika kuandika na kuripoti habari za Wagombea Wanawake katika nyadhfa mbalimbali nchini huku pia idadi ya Wanawake waliojitokeza kugombea katika uchaguzi huo ikionekana kuwa finyu ikilinganishwa na idadi ya Waume.

Ni kutokana na hali hiyo, Wanahabari wamehimizwa kuandika na kuripoti habari/ Matukio ya Uchaguzi mkuu kiundani zaidi kwa kuzingatia usawa kwa wagombea wote bila kujali jinsi zao hususani kuwaweka kando Wanawake huku wanawake wenyewe wakihimizwa kuwa mstari wa mbele zaidi katika kushiriki masuala mbalimbali ikiwemo ya kiuongozi katika jamii.
Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali vya Habari katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa Jijini Mwanza katika Semina ya siku tatu iliyoanza jana Octoba 19 na inatarajia kufika tamati kesho octoba 22 ikiangazia juu ya VYOMBO VYA HABARI NA UCHAGUZI iliyoandaliwa na Chama cha cha Wanahabari Wanawake nchini Tanzania (TAMWA-Tanzania Media Women Association).

MAHAFALI YA KWANZA YA SHULE YA SEKONDARI YA WAVULANA YA SULLIVAN PROVOST YA KIBAHA YAFANA.

$
0
0
Baadhi ya wahitimu wa kidato cha nne wa  Shule ya Sekondari ya Wavulana ya  Sullivan Provost , wakihudhuria mahafali yao ya kwanza yaliyofanyika shuleni hapo, Kibaha kwa Mathias, Mkoani Pwani hivi karibuni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shule ya Wavulana ya Sullivan Provost,  Rachel Mwalukasa (kushoto), akizungumza katika sherehe za mahafali ya kwanza ya kidato cha ya shule hiyo shuleni hapo, Kibaha kwa Mathias, Pwani hivi karibuni. Wengine kutoka kulia ni Mkuu wa Shule, Jacob Mkumbo, Mwenyekiti wa Bodi ya shule, Godfrey Zimba na mgeni rasmi Prof. Ibrahim Shao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shule ya Wavulana ya Sullivan Provost,  Rachel Mwalukasa (wa pili kushoto), akimpongeza Emmanuel Sebyo,  mmoja wa wanafunzi waliofanya vizuri kimasomo wakati sherehe za mahafali ya kwanza ya kidato cha ya shule hiyo shuleni hapo, Kibaha kwa Mathias, Pwani hivi karibuni. Kushoto ni mmoja wa wajumbe wa bodi ya shule hiyo, Prisca Mwalukasa.

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR AWAFARIJI BAADHI YA MAJERUHI

$
0
0
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akiwafariji baadhi ya majeruhi wa ajali mbali mbali zilizotokea katika ziara za mikutano ya Kampezi mbali mbali za vyama vya Siasa hapa Nchini.
 Balozi Seif na Mkuu wa Kitengo cha kupokea Wagonjwa wa dharura katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Dr. Juma  Salum Mbwana wakibadilishana mawazo kwenye Wodi ya akina Mama ambao baadhi yao walipata ajali ya gari katika Mikutano ya Kampen za Uchaguzi.

MAJERUHI 10  wanaendelea kupatiwa huduma za matibabu katika Hospitali kuu ya Mnazi Mmoja kufuatia ajali tofauti walizopata  wakati wakielekea kwenye mikutano ya Kampeni  za uchaguzi inayoendelea katika sehemu mbali mbali hapa Nchini.

Ajali hizo takriban zote zimehusisha zaidi vijana  waliokuwa wamepanda vyombo ambavyo vyengine vikiendeshwa kwa mwendo wa kasi  na baadhi  vilijaa idadi ya abiria  kupindukia mpaka.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipata wasaa wa kufika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja kuwakagua majeruhi hao waliopata athari mbali mbali zikiwemo za kuvunjika viungo na michubuko.

Akiwafariji majeruhi hao  kutoka Vyama vya Siasa vya  CCM katika  Mkutano wao wa  Makunduchi na CUF katika  Mkutano wao wa Nungwi Balozi Seif  aliwatakia Vijana hao kupoa haraka na kurejea katika familia zao waendelee na harakati zao za Kimaisha.

Balozi Seif katika nasaha zake aliwaasa Vijana hao kuwa na tahadhari wakati wanapoendesha vyombo vya usafiri wa Bara barani kama gari na vespa kwani ni vyema wakaelewa kuwa mwendo wa kasi mbali ya kusababisha vifo lakini pia unachangia kuacha vilema vya maisha.

Naye Mkuu wa Kitengo cha kupokea wagonjwa wa dharura katika Hospitali Kuu ya Mnamo Mmoja Dr. Juma Salum Mbwana { Mambi } alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba hali za wagonjwa hao zinaendelea vyema.

Dr  Mambi alisema majeruhi waliotokana na ajali hizo wwengi kati yao tayari wamesharuhusiwa kurejea nyumbani baada ya kupatiwa huduma za Matibabu katika Hospitali hiyo.

Kampeni za uchaguzi zilizokuwa zikiendelea katika maeneo mbali mbali Nchini Tanzania zinatarajiwa kufikia kilele chake ifikapo Tarehe 24 Mwezi huu na uchaguzi Mkuu utafanyika Tarehe 25 zikiwa zimebakia siku tano.
Othman  Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
20/10/2015.

MAMA SHUJAA WA CHAKULA BI. BAHATI MURIGA AHUDHURIA TAFRIJA UBALOZI WA TANZANIA, WASHINGTON DC

$
0
0
  Bi. Bahati Muriga alifika Ubalozi wa Tanzania, Washington DC kuhudhuria tafrija iliyoandaliwa na Oxfam America. Bi. Muriga aliongelea maisha yake katika Mkoa wa Mwanza alipokuwa anafanya kazi kama Mkuu wa shule ya msingi, pamoja na hayo pia aliweza kuingia katika shughuli za kilimo akitafuta kipato ya kusomesha watoto wake wawili ili kuwapatia maisha bora.

Ubalozi wa Tanzania Washington DC ulipata ugeni wa wasau kutoka mashirika mbalimbali waliokuja kuungana na Oxfam America inayoandaa Siku ya Chakula Duniani “World Food Day 2015” tarehe 16 Octoba. Bi. Muriga atasafiri kwenda katika mji wa Des Moines, Iowa kushiriki katika ziara na Oxfam inayoandaa matamasha mbalimbali kama ya “World Food Prize”.
 Bi Bahati Muriga akielezea ni jinsi gani alivyo na furaha kufika ubalozini na kuweza kukutana na watu mbalimbali kutoka mashirika tofauti hususan OXFAM.

UCHAMBUZI WA HABARI TOKA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISHENI OKTOBA 20, 2015.

$
0
0
Huu ni uchambuzi wa Habari toka vituo mbalimbali vya Televisheni  October 20, 2015.

Kamati ya Saidia Taifa Stars ishinde yatoa dira kuhakikisha timu hiyo inashinda   katika michezo yake ya kimataifa ;https://youtu.be/x5PxjRc9zpY

Shirikisho la soka Ulaya UEFA yatangaza ratiba ya mechi za mchujo za timu zitakazowania   kufuzu kucheza finali  za Ulaya mwakani nchini Ufaransa ; https://youtu.be/aq31NLL6HHg

NEC imewatahadharisha wananchi kuwa hakuna kifungu cha sheria kinachoruhusu mtu kubakia katika kituo cha kura baada ya kuoiga kura;  https://youtu.be/AGlLlvVXmdM

Tambua sababu zinapolekea ugonjwa wa figo ambao umeonekana kuathiri kundi kubwa la watu hapa Nchini,kama anavyotueleza Dk.John; https://youtu.be/b9gESJoPPwg

Fuatilia ujue Vipaumbele vya vyama mbalimbali kuelekea uchaguzi Mkuu Oktoba 25 mwaka huu vinazingatiwa?:https://youtu.be/X_0dHoFR_jU

Fuatilia namna ambavyo watanzania walivyojipanga kuhakikisha Nchi inakuwa na amani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu: https://youtu.be/hq0__StJoM4
Tambua Mchango wa vyombo vya habari katika kutuliza vurugu katika wakati huu wa kuelekea uchaguzi Mkuu zikiwa zimesalia siku 4 tu:  https://youtu.be/c0UldkD7TcE

Fuatilia muamko wa wananchi baada ya kusambazwa kwa elimu ya kupiga kura zikiwa zmesalia siku chache kuelekea uchaguzi mkuu: https://youtu.be/nGtbDZVIBxc

Mgombea Uraisi CCM Zanzibar Dkt. Ali Shein awaahidi wananchi kuendeleza mradi mkubwa wa viwanda Wa FUMBA kusaidia ajira kwa Vijana. https://youtu.be/VAF-4N0L09Q
Mgombea Uraisi CCM Dkt. John Magufuli aahidi kupambana na wavuvi haramu katika Ziwa Viktoria endapo atapata ridhaa ya wananchi. https://youtu.be/QPgoO8cztgw
Mjumbe wa Halmashauri Kuu Ya CCM Taifa Balozi Ali Abeid Karume asema wananchi wa Zanzibar wana mamlaka kamili ya kuchagua kiongozi wanayemtaka. https://youtu.be/PaTFO8jhyo8
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Raisi Jakaya Kikwete amezindua awamu ya pili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa vita ndani ya kamandi ya anga Ngelengele. https://youtu.be/ll36RCNB_qo

Jeshi la polisi nchini limewahakikishia wananchi kuwa limejipanga vema kuhakikisha ulinzi na usalama katika vituo vya kupigia kura. https://youtu.be/e2HOVGUBcLw

Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA yavitaka vyombo vya habari kutoa habari zenye kuelimisha na kudumisha amani. https://youtu.be/nyZxEAcu9wc 

GOJU RYU KARATE-DO JUNDOKAN SEMINA UINGEREZA IMEFANA SANA!!

$
0
0


 SenSei Rumadha Fundi, amesimama mbele ya bendera ya Tanzania.
 Wakicheza Kata ya kundi kwa pamoja "Shisochin Kata"
Wakuu matawi nchi shiriki.
Kundi la wawakilishi sita wa nchi za Ulaya.

 Gasshuku au semina ya Karate mtindo wa Okinawa Goju Ryu
Jundokan So Honbu, imefungwa Jumapili usiku na kufuatiwa kwa
 tafrija kubwa ya kuwaaga washiriki "Sayonara Party" wa kike
 na kiume, umri kuanzia miaka 13 had 70 toka nchi mbalimbali
 za Ulaya na Japan ikiwemo na Tanzania iliyowakilishwa na
 sensei Rumadha. Viongozi wa Karate wa nchi zilizoshiriki ni:
 sensei Rene Ramanitrandrasana 9 Dan  wa Ufaransa,
 Sensei Antoine, Ufaransa 5 Dan, Sensei Bob Honiball 8 Dan
 Uingereza, Sensei Tony  Green 8 Dan , Uingereza, Sensei
 Jenni 5 Dan, Uingereza,  Sensei Ilpo, Sweden, 7 Dan,
 Sensei Caideiro 5 Dan, Ureno, Sensei Dr. Freidrich Gsodam 9
 Dan, Austria.

 Hii ilikuwa ni semina kubwa ya kipekee kufanyika 
 Uingereza na wakuu wake wa tano kushiriki toka visiwa vya
 Okinawa; walio ongozwa na mwenyekiti wa sasa wa mtindo huo
 Sensei Yoshihiro Miyazato, Kancho.

 Mbinu na matumizi yake ya kujihami kutumia sanaa ya Karate
 pamoja na ubora wa kata zilifanyiwa mazoezi sana katika
 semina hiyo. 

Kuzingatia nidhamu na utamaduni wa jadi wa
 Karate na kuheshimu desturi zake halisi, viongelewa
 katika  mfumo huo wa Goju Ryu Karate. 

Kwa ujuml, semina
 hiyo iliwakutanisha  washiriki  wapatao  120,
 wakiwemo na watoto wa umri wa kuanzia miaka 13 had 17.

TANZANIA KUADHIMISHA SIKU YA HAKI ZA BINADAMU AFRIKA.

$
0
0
  Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw. Idd Ramadhan Mapuri akiwasalimia wazee na watetezi wa haki za binadamu (hawapo pichani) wakati wa semina juu ya haki za wazee mapema hii leo jijini Dar es Saam.
 Baadhi ya wazee na watetezi wa haki za binadamu walioshiriki semina elekezi juu ya haki za wazee wakimsikiliza kwa makini Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi. Mary Massay wakati akitoa neno la ufunguzi mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Eliphace Marwa- Maelezo.

Na Eliphace Marwa - Maelezo
TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Tanzania kwa kushirikiana Shirika lisilo la kiserikali la Help Age Tanzania zinaujulisha umma kwamba tarehe 21 Oktoba 2015 kutakuwa na maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu Afrika.

Maadhimisho hayo yatakayofanyika katika Hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam ambapo viongozi mbalimbali wa Serikali na Mabalozi wa Afrika watahudhuria maadhimisho hayo yenye lengo la kulinda na kutetea haki za wazee Tanzania.

Akizungumza na Wazee na watetezi wa haki za binadamu, Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi. Mary Massay amesema kuwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inawajibika Kitaifa kufuatilia hatua za utekelezaji wa haki za binadamu hususani wazee ili waweze kuishi kwa furaha, amani na usalama kinyume na sasa Ambapo wazee wamekuwa wakiuawa kwa imani za kishirikina.

Maadhimisho haya ya haki za Binadamu Afrika ni sehemu ya Mpango-Kazi wa Kitaifa wa Haki za Binadamu ambao ni mkakati wa Serikali wa miaka mitano (2013 – 2017) wenye lengo la kutoa dira kwa Serikali yenyewe kwa maana ya Wizara, Idara, Taasisi za Serikali na Asasi za Kiraia na wananchi kwa ujumla jinsi ya kukuza, kulinda na kuhifadhi haki za binadamu ili kuimarisha utawala bora nchini. 

Naye Mkurugenzi toka Shirika lisilo la Kiserikali la Help Age Bwana Smart Daniel amesema kuwa kati ya nchi 96 Duniani Tanzania iko katika nafasi ya 92 kwa kulinda haki za wazee kwa kuzingatia vigezo vya upatikanaji wa huduma bora za afy, mazingira wezeshi kwa wazee, uhakika wa kipato kwa wazee pamoja na uwezeshwaji wa wazee katika fursa mbalimbali ili kujipatia kipato.

"Katika suala la kipato Tanzania iko nafasi ya 94 kwa kujali wazee kwa kuwalipa pensheni, katika suala la Afya kwa wazee Tanzania iko nafasi ya 66 na katika suala la mazingira wezeshi kwa wazee Tanzania iko nafasi ya 88 na hii inatokana na kutokuwepo kwa sheria ya wazee", alisema Bwana Smart. 

Aidha, Maadhimisho haya yanalenga kuongeza uelewa kwa umma juu ya wajibu alionao kila mwananchi wa kutetea, kulinda, kuhifadhi na kuhamasisha haki za binadamu nchini ili kudumisha amani, utulivu na maendeleo endelevu.

MAKAMU WA RAIS AIFARIJI FAMILIA YA RUBANI WILLIAM SLAA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kumfariji Meya wa Manispa ya Ilala Mhe. Jery Slaa alipofika nyumbani kwao Gongolamboto jijini Dar es salaam leo Octoba 20, 2015 kwa ajili ya kutoa mkono wa pole kufuatia kifo cha Baba yake Marehemu Rubani William Slaa aliyefariki wiki iliyopita kwa ajali ya Hekopta.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kumfariji Bibi Tabita Slaa aliyekuwa Mke wa Marehemu Rubani William Slaa aliyefariki wiki iliyopita kwa ajali ya Hekopta wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Gongolamboto jijini Dar es salaam leo Octoba 20,2015 kwa ajili ya kutowa mkono wa pole.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo kufuatia kifo cha marehemu Rubani William Slaa aliyefariki Dunia wiki iliyopita kwa ajali ya Helkopta wakati Makamu wa Rais alipofika nyumbani kwa Marehemu Slaa Gongolamboto jijini Dar es salaam leo Octoba 20, 2015. (Picha na OMR)

ZIARA YA WANAJESHI SONGWE

$
0
0
 handisi Mshauri wa Mradi wa ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Songwe, Khalil Jadallah akibadilishana mawazo na Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Songwe, Mbeya, Khamisi Amiri wakati wa ziara ya Maofisa  Wanadhimu wa Jeshi la ulinzi la Wananchi wa chuo cha Arusha (College of Senior Commandants- CSC) katiika kiwanja hicho Oktoba 15 kwa ajili ya kujifunza masuala ya usafiri wa anga.
 Naibu Mkuu wa Chuo cha Maofisa Wanadhimu wa Jeshi la ulinzi la Wananchi wa chuo cha Arusha (College of Senior Commandants- CSC), Meja Jenerali Alfred Kapinga (kushoto) akisaini kitabu cha wageni alipowasili kwenye ofisi ya Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Songwe, Mbeya jana Oktoba 15 na ujumbe wake wa maofisa 30 wa chuo hicho kwa ajili ya kujifunza masuala ya usafiri wa anga.
  Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Songwe, Mbeya, Khamisi Amiri akiwaongoza Maofisa Wanadhimu wa Jeshi la ulinzi la Wananchi wa chuo cha CSC Arusha (College of Senior Commandants- CSC) kutembelea kiwanja hicho Oktoba 15 kwa ajili ya kujifunza masuala ya usafiri wa anga.

KIIZA MCHEZAJI BORA WA LIGI YA VODACOM SEPTEMBA

$
0
0
Mshambuliaji wa timu ya Simba, Hamisi Kiiza ndiye mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi Septemba.
Kwa kuibuka mchezaji bora, Kiiza atazawadiwa sh. milioni moja kutoka kwa mdhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom.
Kiiza ambaye ameisadia Simba kufanya vizuri kwenye mwezi huo, ikiwemo kufunga mabao matatu (hat trick) kwenye mechi dhidi ya Kagera Sugar aliwashinda washambuliaji wa timu za Stand United (Elias Maguli) na Yanga (Amisi Tambwe).
Ndani ya mwezi Septemba ambapo zilichezwa raundi tano, Kiiza amefunga jumla ya mabao matano.

WAANDISHI WAMETAKIWA KUTAJA MAJINA SAHIHI YA WATU WENYE ULEMAVU KUEPUKA UNYANYAPA

$
0
0
 Mwezeseshaji wa mafunzo ya waandishi wa habari katika uchaguzi jumuishi,kwa watu wenye ulemavu,Blandina Sembu akizungumza na waandishi wa (habari hawapo pichani) juu ya waandishi kuhamasisha watu wenye ulemavu kupiga kura katika mazingira rafiki katika semina iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Sehemu ya waandishi wakifatilia maada katika semina iliyoandaliwa  na SHIVYAWATA BA panoja na Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Dar es Salaam(DCPC) iliyofanyika jijini Dar es Salaam

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
WAANDISHI wa habari wametakiwa kuandika habari kwa usahihi wakiwataja watu wenye ulemavu kwa kutumia majina sahihi kuepuka unyanyapa dhdi yao .

Rai hiyo ilitolewa juzi jijini Dar es Salaam na Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Lucas Kija, wakati wa mafunzo ya siku mbili ya waandishi wa habari juu ya uandishi wa habari za uchaguzi kwa watu wenye ulemavu.

Mafunzo hayo ambayo yaliwashirikisha waandishi wa habari kutoka Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Lindi, Mtwara, Kilimanjaro na Tanga  yaliandaliwa na Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) kwa kushirikiana na Klabu ya Waandishi wa Habari wa Jiji la Dar es Salaam (DCPC),  kupitia Mradi wa Uchaguzi Jumuishi.
"Kuna majina sahihi na yasiyo sahihi kwa watu wenye ulemavu, hivyo waandishi wa habari lazima mtaje mhusika kwa kutumia jina sahihi," alisema Kija alipokuwa akitoa mada katika mafunzo hayo.

Kwa mujibu wa mwezeshaji huyo, miongoni mwa majina yasiyo sahihi ni kipofu, wasiosikia, vichaa, chizi, zeruzeru na watu wenye mtindio wa ubongo ambayo hayapaswi kutumiwa.

Mwezeshaji huyo aliyataja baadhi ya majina sahihi yanayopaswa kuwaita watu wenye ulemavu kuwa wasioona, viziwi na walemavu wa akili.

Katika mafunzo hayo, washiriki walipata fursa ya kupata elimu kuhusu vikwazo vikuu vinavyokwamisha ushiriki wa watu wenye ulemavu katika uchaguzi. Elimu hiyo ilitolewa na Wawezeshaji Kija na Blandina Sembu.

Wawezeshaji hao walisema vikwazo hivyo vimegawanyika katika mitazamo ya kijamii, mazingira na kitaasisi.

Amesema kuna  vikwazo vya vimekuwepo katika mchakakato wa uchaguzi kunazia kampeni,usalama kutokana na mazingira ya jamii hiyo,kukosekana kwa takwimu sahihi za watu wenye ulemavu, miundombinu isiyo rafiki na sheria kandamizi mfano gharama za uchaguzi.

Kaimu Mkurugenzi wa SHIVYAWATA, Francis Gugu ambaye pia ni mlemavu wa usikivu hafifu, alisema shirikisho hilo linajumuisha vyama 10 vya watu wenye ulemavu kitaifa na limekuwa likifanya ushawishi na utetezi kwa watu wote.
Akizungumzia mradi huo, Gugu alisema Mei 20, mwaka huu, SHIVYAWATA ilitia saini mradi huo wa mwaka mmoja na Shirika la Wanawake la Umoja wa Mataifa (UN-Women) kwa lengo la kuchoche ushiriki wa watu wenye ulemavu katika uchaguzi mkuu.

LIGI KUU YA VODACOM KUENDELEA WIKI HII

$
0
0
Ligi kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) inatarajiwa kuendelea kesho Jumatano kwa michezo minne kuchezwa katika viwanja tofauti nchini, huku timu 8 zikisaka kupata pointi tatu muhimu.
Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Young Africans watawakaribisha Toto Africans, mchezo utakaonza majira ya saa 10:30 jioni, mjini Shinyanga Stand United watakua wenyeji wa Majimaji katika uwanja wa Kambarage mjini humo.
Tanzania Prisons watawakaribisha Simba SC katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, huku Wagosi wa Kaya, Coastal Union wakiwakaribisha Kagera Sugar katika uwanja wa Mkwakani jijini Tanga.
Alhamis ligi hiyo itanendelea kwa michezo minne pia kucheza katika viwanja mbalimbali, JKT Ruvu wataikaribisha Mtibwa Sugar uwanaj wa Karume jijini Dar es salaam, Mwadui FC watacheza dhidi ya Mgambo Shooting katika uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga.
Jijini Mbeya, Mbeya City watawakaribisha African Sports katika uwanja wa Sokoine, huku Ndanda FC wakiwa wenyeji wa waoka mikate wa bakhresa Azam FC katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

WARIDHISHWA NA HUDUMA ZA KITUO CHA AFYA KIVUNGE, UNGUJA

$
0
0
IMG_20151016_175545
Pichani juu na chini ni muonekano wa Jengo la kituo cha afya Kivunge Wilaya ya Kaskazini "A" visiwani Unguja kilichojengwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa.

Na Mwandishi wetu
BAADHI ya Wananchi wa Kijiji cha Kivunge Wilaya ya Kaskazini “A” wameelezea kuridhishwa kwao na huduma za afya zinazotolewa katika kituo kipya cha afya cha Kivunge.

Kituo hicho kimejengwa chini ya mradi wa Umoja wa Mataifa(UN) wa kuviwezesha vituo vya afya mbali mbali nchi ambapo kituo hicho kinatoa huduma mbali mbali za akina mama na watoto pamoja na masuala ya kutibu vidonda na majeraha mbali mbali.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkazi wa kijiji hicho, Kassim Haji Simai alisema kituo hicho kimekuwa mkombozi wa wananchi kwani pindi panapotokea mgonjwa wa ghafla ufika katika kituo hicho na kupewa matibabu ya haraka.

Alizitaja changamoto kubwa iliyopo kituoni hapo kuwa ni pamoja na upungufu wa madakta na wauguzi jambo ambalo baadhi ya wananchi ukaa muda mrefu wakisubiri huduma kwani wagonjwa wanakuwa wengi kuliko watoa huduma.
IMG_9525
“Tunawashukru sana wafadhili waliojenga kituo hiki na serikali kwa ujumla kwani wametusaidia sana huduma hizi tulikuwa tunazifuata mbali sana”, alisema Haji.

Kwa upande wake Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez alifika katika kituo hicho na kutembelea maeneo mbali mbali ya kituo hicho na kuona ni jinsi gani kinatoa huduma kwa wananchi.

Alisema kuwa ufanisi wa mradi huo unaongeza ushawishi kwa Umoja wa Mataifa kuongeza zaidi msaada hasa vifaa vya kisasa vya huduma za afya pamoja na wataalamu wa afya ili kuhakikisha wananchi wanaendelea kupata huduma za afya kwa ufanisi zaidi.

“ Kituo hiki kinatoa huduma kwa wananchi wengi hivyo nitapeleka salamu makao makuu ili tujadiliane na kuona ni jinsi gani tunaendelea kusaidia kituo hiki hasa katika suala la vifaa vya kisasa na madaktari.”, alifafanua Bw.Rodriguez.
IMG_9533
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akitazama jengo la kituo cha afya Kivunge alipofanya ziara fupi ya kukagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa visiwani Unguja ikiwa ni sehemu ya sherehe za miaka 70 ya Umoja wa Mataifa tangu kuaznishwa. Kulia ni Daktari wa kujitolea wa kituo cha afya Kivunge, Alexander Vogt.

Naye Mratibu wa Mradi wa Health Improvement Project (HIP), Jabir James alisema kituo hicho kinatoa huduma bora na zenye kukidhi mahitaji kwa wananchi ambapo kwa siku wanapokea zaidi ya wagonjwa 100 hadi 200 hali ambayo kitathimini ni kubwa kutokana na uwezo wa kituo hicho kimatibabu.

Alisema kuwa bado wanaendelea kutafuta ufumbuzi wa kuongeza vifaa na madaktari ili kuhakikisha wanaongeza ufanisi katika utoaji wa huduma bora ili kufikia dhana ya umoja wa mataifa katika masuala ya afya ya kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na uhakika wa kupata huduma bora za afya na endelevu.
Viewing all 110019 articles
Browse latest View live




Latest Images