Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

TANZANIA YAJIANDAA VEMA NA USIMAMIZI WA URANI

$
0
0

 Picha mbali mbali za wajumbe na viongozi na wataalamu (washauri) kutoka shirika la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) pamoja na wafanyakazi wa Tume ya nguvu za Atomiki Tanzania wakiwa katika semina ya juu ya usimamizi wa sheria na kanuni za usimamizi wa mionzi ya nyuklia Tanzania, iliyofanyika makao makuu ya Tume ya Mionzi Tanzania yaliyopo jijini Arusha. Picha na Yohana Challe.

NA; YOHANA CHALLE ARUSHA.
TUME ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), imesema kuwa imejiandaa vilivyo katika usimamizi wa uchimbaji wa madini ya urani ambayo yanapatikana kwa wingi hapa nchini.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia John Mngodo alisema kuwa moja ya majukumu ambayo serikali inafanya ni kujiandaa juu ya kusimamia uchimbajia wa madini hayo.

“Mkazo uliowekwa hapa ni kwamba ni lazima usalama wa mionzi upewe mkazo hivyo TAEC itahakikisha usalama unakuwepo na katika kila hatua ambayo watakuwa wanajiandaa au wanachimba na kusafirisha madini ya urani lazima ukaguzi ufanyike na kutoa kibali ili kuhakikisha usalama unakuwepo” alisema Mngodo.

Mngodo alizungumza hayo wakati wa kuhitimisha zoezi la kupitia taratibu za uendeshaji, ukaguzi na usimamzi wa nyuklia na mionzi hapa nchini, zoezi hili lilifanyika kwa siku kumi tangu Oktoba 4 hadi oktoba 14 mwaka huu katika makao makuu ya Tume hiyo mkoani hapa kwa kushirikiana na wataalamu kutoka zaidi ya nchi 10 duniani.

“Wataalamu hawa walikuwa wakipitia taratibu na namna ya jinsi ambavyo tunavyosimamia shughuli za mionzi na nyuklia hapa nchini” alisema Mngodo.

Wataalamu hawa wametokea katika nchi za Jordani, Irend, Ubelgiji, Sudani, Kenya,Ukreini, Argentina, Australia, Pakistani, Nigeria, Zimbabwe, Uingereza na Zambia

Wataalamu hawa walikuja kwa mwaliko wa serikali ili kuweza kuisaidia Tume hii ili kuweza kuboresha zaidi shughuli zinazoendelea hasa elimu kwa wafanyakazi, pamoja na kupitia sheria na kanuni za usimamizi wa masuala ya Nyuklia na mionzi hapa nchini.

Aliongeza kuwa changamoto kubwa wanayokumbana nayo ni jinsi ya kuwapata wataalamu wa kusimamia shughuli hizo (rasilimali watu) pamoja na fedha, japo akiipongeza serikali kwa kuendelea kujitahidi kutoa mafungu ili kuendelea kuboresha shughuli za Tume.

Kwa upande wake Leonard Kifanga ambaye ni Mwanasayansi mwandamizi wa nyuklia, alisema kuwa lazima Tanzania iwe na mipango mikakati ya kuboresha na kushughulikia ajali za kinyuklia zinazoweza kujitokeza, kwani itasaidia kujiepusha na madhara ambayo yanaweza kuepukika kwa urahisi na kwa haraka.

“Nashauri lazima Tume na Taasisi za kusimamia majanga ziwe huru ili zifanye kazi kwa uhuru zaidi na kwa haraka ili kila mtu aweze kuwajibika katika nafasi yake na hii itasaidia kujua tatizo lilipoanzia” alisema Bwana Kifanga.

Kifanga ni mmoja wa waatalamu kutoka nchini waliokwenda japani kwenye uchunguzi wa mlipuko wa kinu cha nyuklia cha Fukushima kilichotokea baada ya kutokea tetemeko la ardhi lililoharibu mfumo wa kinu cha nyuklia na hatimaye kinu kupasuka na kutokea mlipuko.

RAIS KIKWETE AFUNGUA TAWI LA BENKI KUU DODODMA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifunua pazia kuashiria kufungua rasmi tawi la Benki kuu ya Tanzania Dodoma Oktoba 15,2015.Kushoto ni Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum na Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu(picha na Freddy Maro)

KUZIONA YANGA, AZAM FC KIINGILI 5,000/=

$
0
0
SKIRIKISHO la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom siku ya Jumamosi kati ya Yanga SC dhidi ya Azam utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, kiingilio vha chini kikiwa ni shilingi elfu tano (5,000) kwa viti vyenye rangi ya bluu, Kijani na Machungwa.
Tiketi za mchezo huo zitauzwa siku ya mchezo Jumamosi katika eneo la Uwanaj wa Taifa jijini Dar es salaam, ambapo kingilio cha juu kitakua ni Shilingi Elfu Thelathini (30,000) kwa VIP A, na Shilingi Elfu Ishirini (20,000) kwa VIP B & C.
Mwamuzi wa mchezo huo atakua Abdallah Kambuzi kutoka mkoani Shinyanga, akisaidiwa na Makame Mdogo (Shinyanga), Robert Luhemeja (Mara), mwamuzi wa akiba Frank Komba (Dsm) huku Kamisaa wa mchezo akiwa Joseph Mapunda kutoka mkoa wa Ruvuma.
Michezo mingine ya Ligi Kuu ya Vodacom siku ya Jumamosi ni Majimaji FC dhidi ya African Sports katika uwanja wa Majimaji mjini Songea, Ndanda FC wakiwakaribisha Toto African katika dimba la Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Mbeya City FC watawakaribisha Simba SC kwenye dimba la uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Stand United wakiwakaribisha Tanzania Prisons kwenye uwanja wa Kambarage mjini Shinyaga, Jijini Tanga Coastal Union watakua wenyeji wa Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Mkwakwani.
Jumapili ligi hiyo itaendelea kwa michezo miwili, Maafande wa Mgambo Shooting watakua wenyeji wa Kagera Sugar uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, huku wachimba Almasi wa Mwadui FC wakiwakaribisha JKT Ruvu katika uwanja wa Mwadui Complex.

WABUNIFU WA MAVAZI NCHINI WAKUSANYA NGUVU KWA PAMOJA KUHUBIRI JUU YA UMUHIMU WA AMANI

$
0
0
Mbunifu wa Mavazi nchini, Mustafa Hassanali akizungumza na  Waandishi wa Habari hawapo pichani juu ya umuhimu wa Amani hususani katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, Mwaka huu na kusisitiza onyesho la mavazi litakalo fanyika tarehe Oktoba  17 Mwaka huu katika ukumbi wa King Solomon uliopo Eater Point Namanga, ambalo litakaloonyesha kazi za wa wabunifu mbalimbali kama Kiki Zimba pamoja na Martin Kadinda.
 Baadhi ya Waandishi wa Habari wakisikiliza kwa makini taarifa iliyokuwa inatolewa na Mbunifu Mkongwe wa Mavazi Barani Afrika,Mstafa Hassanali juu ya umuhimu wa Amani hususan kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Octoba 25,Mwaka huu.

Na Bakari Issa

Wabunifu wa Mavazi nchini Tanzania, Mustafa Hassanali,Kiki Zimba pamoja na Martin Kadinda wameazimia kukusanya nguvu kwa pamoja ili kuhubiri juu ya umuhimu wa Amani hususan kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Octoba 25,Mwaka huu.


Wabunifu hao wamekusanya nguvu kwa pamoja kwa kuwa na onyesho la mavazi litakalo fanyika tarehe 17 Octoba Mwaka huu katika ukumbi wa King Solomon uliopo Eater Point Namanga,ambalo litakalo onyesha kazi za ubunifu zilizofanywa na wabunifu hao watatu.


Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Saalam,Mbunifu Mkongwe wa Mavazi Barani Afrika ,Mustafa Hassanali amesema kutokana na wimbo wetu wa Taifa “Hekima,Umoja na Amani,hizi ni Ngao zetu”kuna umuhimu kwa vijana kukuza na kulinda Uhuru,Amani na Utulivu wa nchi.


Kwa Upande wake,Martin Kadinda amesema Uchaguzi Mkuu ni wa muhimu sana,hivyo basi vijana wa Kitanzania wahakikishe wanapiga kura kwa Amani katika Uchaguzi Mkuu wa Octoba 25 na kukaa katikahali ya Utulivu kwa kufuatilia na kukubali matokeo yatakayotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) katika hali ya Amani.

MKUTANO WA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA TANZANIA.ZANZIBAR.

$
0
0
Viongozi wa Meza Kuu wakiwa wamesimama wakati wa kuomba Dua Mkutano huo wa Baraza la Viongozi wa Vyama vya Siasa Tanzania uliovikutanisha Viongozi wa Vyama 22 vya Siasa Tamzania uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya bwawani Zanzibar.wa kwanza Jaji Lubuva Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Mzirai na Msajili Msaidi wa Vyama vya Siasa Tanzani Mhe Ibrahim Mkwawa.
Mmoja wa Viongozi wa Vyama vya Siasa Tanzania akiuombea Mkutano huo wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Bwawani Zanzibar. ukizungumzia maadili ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania .
KWA PICHA ZAIDI BOFYA.

RAIS JAKAYA KIKWETE KUWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UJENZI WA BANDARI YA BAGAMOYO

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe  akizungumza na waandi wa habari wapo picha juu ya ujenzi wa bandari ya Bagamoyo utakaokuwa wa aina yake Afrika Mashariki na Kati, unatarajiwa kugharimu dola za Marekani bilioni 10 na kukamilika kati ya miaka mitano hadi saba ijayo. kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa CMHI ambaye pia ni Makamu wa Rais Mtendaji wa kampuni ya China Merchant Group Dk Hu Jianhua.kikao hichi kimefanyika leo jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbarimbari na Mjumbe kutoka China Mkurugenzi Mtendaji wa CMHI ambaye pia ni Makamu wa Rais Mtendaji wa kampuni ya China Merchant Group Dk Hu Jianhua.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)


 WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe amewathibitishia wakazi wa Bagamoyo kuwa wale wote watakaoguswa na mradi wa ujenzi wa bandari mpya watalipwa fidia na wengine watajengewa nyumba kwenye maeneo ya mji huo.

Akizungumza na wandishi wa habari badaa ya kukutana na Mkurugenzi wa Kampuni ya China Merchants Group itakayosimamia ujenzi huo, Dk Hu Jianhao, Membe alisema katika ujenzi huo utakaochukua hekta 2400, wananchi wote watakaohuswa hawataachwa bure.

“Mradi huo ni mkubwa sana unaoshirikisha kampuni hii ya China Merchants Group, wawekezaji kutoka Oman ambao wataalamu wao pia wameshafika na Serikali ya Tanzania. Tunatarajia kuwa utaibadilisha Bagamoyo kwa kiasi kikubwa na kuufannya kuwa mji wa viwanda, hatua itakayovuta wawekezaji wengi zaidi na kuzalisha ajira nyingi,” alisema.

RAIS KIKWETE AONGOZA MAMIA KUMZIKA DK.KIGODA HANDENI LEO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Jakaya Mrisho Kikwete akiungana na wananchi wa Handeni Mkoani Tanga, katika kumzika aliyekuwa waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Kigoda Rais akiwa na chepe ya mchanga.

SERIKALI ITAWACHUKULIA HATUA ZA KISHERIA WATAKAOKAIDI AGIZO LA NEC - RAIS KIKWETE

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete (pichani) amewataka wananchi wote wenye haki ya kupiga kura kuhakikisha wanaheshimu maagizo ya Tume ya Uchaguzi ya kuwataka waondoke katika vituo vya kupigia kura mara baada ya kumaliza zoezi la upigaji kura.

Rais Kikwete Amesema kuwa wenye jukumu la kukaa kituoni ni Mawakala wa wagombea na sio wapiga kura wote kama inavyodaiwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa.
Rais Kikwete ametoa kauli hiyo leo mjini Dodoma wakati wa kilele cha Mwenge wa Uhuru kilchoenda sanjari na kumbukumbu ya miaka 16 ya kifo cha Baba wa Tiafa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
“Mlinzi wa uhakika wa kura ni wakala kwani ndiye anayekuwepo wakati wote katika chumba cha kupigia na kuhesabia kura…ni jambo la kushangaza kuona baadhi ya viongozi wa vyama  vya siasa wakiwahamasisha wafuasi wako kubaki vituo mita 100…wanalinda nini? wakati kuna Mawakala ndani” alihoji Rais Kikwete.
Amesema kuwa  ikiwa wapiga kura wengi watabaki vituoni kwa madai ya kulinda kura upo uwezekano mkubwa wa kutokea fujo ambazo zitasababisha baadhi ya watu kuogopa kupiga kura na hivyo kukosa haki yao ya msingi ya kuwachagua viongozi wanaowataka.
Rais Kikwete amesema kuwa ni vema wananchi wenye sifa za kupiga kura kuondoka kwenye  vituo mara baada ya  zoezi hilo , vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yoyote atakaye kaidi agizo la Tume ya Tiafa ya Uchaguzi.
Amesema kuwa watu wenye nia ya kufanya hivyo wasiilazimishe Serikali ifikie uamuzi wa kuchukua hatua kwa kuwa wanaofanya hiyo wana nia  ovu na nchi hii.
Amesesisitiza kuwa nia yao ovu haitafanikiwa kwani Serikali imejipanga vizuri ili kuhakikisha kila mwananchi wenye sifa ya kupiga kura anafanya hivyo bila bughuza yoyote.
Aidha , Rais Kikwete amewaonya wananchi wote wanaonunua na kuuza vitambulisho vya kupigia kura kuacha tabia hiyo la sivyo dhidi yao zitachukuliwa.
Amesema kuwa ni vema kila mwananch akatunza vizuri kitambulisho chake ili siku ya kupiga kura aende katika kituo cha kupigia kura ili kutekeza haki yake ya kidemokrasia.
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa Ndugu Juma Khatib Chum akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mwenge wa uhuru wakati  wa sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge zilizofanyika katika Uwanja wa Michezi wa Jamhuri mjini Dodoma leo

Mwenge wa Uhuru unaratarajiwa kuzinduliwa mwakani mkoani Morogoro na kilele chake kitakuwa mkoani Simiyu.

Wakati huo huo....

Katika Kilele cha mbio za mwenge wa uhuru , kumbukumbu ya Baba wa Taifa , Mwalimu JULIUS Nyerere na wiki ya vijana Kitaifa, Rais  Jakaya Mrisho Kikwete katika hotuba yake amezungumzia idadi ya watu waliojiandikisha kupiga kura.

Kwa uhakika amesema kuwa idadi ya wapiga kura ni 22,751, 292 kwa upande wa Bara na 503,193 wa Zanzibar.  Hii ndiyo idadi kamili ambayo imo kwenye hotuba ya Mheshimiwa Rais na hii ndiyo idadi kamili kama ilivyotolewa na Tume ya Uchaguzi Tanzania.

Asanteni

 

Imetolewa na Premi Kibanga,

Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi

Dodoma


13 Oct, 2015


MCHAGUENI DKT MAGUFULI NDIYE ATAKAYEWEZA KULETA MABADILIKO YA KWELI-KINANA

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman akiwasili kwenye uwanja wa shule ya msingi Tunduma
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman akihutubia wakazi wa mji wa Tunduma kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Tunduma ambapo aliwaelezea wananchi hao kuwa mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli ana uwezo mkubwa wa kuibadilisha Tanzania,kubadili mfumo wa chama na atakuwa na Baraza la Mawaziri dogo, atapunguza matumizi yasiyo ya lazima ya serikali lakini pia ataondoa kodi ndogo ndogo zinazowapa kero na kurahisisha njia za kufanya biashara kwa wananchi wa mipakani.
wakazi wa mji wa Tunduma wakishangilia jambo walipokuwa wakimsikiliza Katibu Mku wa CCM,Ndugu Kinana kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma ambapo aliwaelezea wananchi hao kuwa mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli ana uwezo mkubwa wa kuibadilisha Tanzania,kubadili mfumo wa chama na atakuwa na Baraza la Mawaziri dogo, atapunguza matumizi yasiyo ya lazima ya serikali lakini pia ataondoa kodi ndogo ndogo zinazowapa kero na kurahisisha njia za kufanya biashara kwa wananchi wa mipakani.

Wakazi wa Mji wa Tunduma na vitongoji vyake wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana kwenye mkutano wa kampeni.

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman akisisitiza jambo mbele ya umati mkubwa wa wakazi wa mji wa Tunduma kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Tunduma.

BOHARI YA DAWA (MSD) YASHIRIKI KONGAMANO LA 29 LA WANASAYANSI WATAFITI MAGONJWA YA BINADAMU

$
0
0

  Ofisa Uhusiano wa MSD, Benjamin Massangya akimuonesha Mwananchi aliyetembelea banda la MSD  nembo ya MSD iliyowekwa katika makasha na vifungashiyo vya dawa.
 Mtaalamu wa Maabara kutoka Bohari ya Dawa (MSD), Twahiri Magoolo  (kushoto), akimuelekeza jambo mwananchi  aliyetembelea banda la MSD katika kongamano la 29 la wanasayansi wa utafiti wa magonjwa ya binadamu Dar es Salaam jana. Kongamano hilo liliandaliwa na Taasisi ya Utafiti  Magonjwa ya Binadamu (NIMR).
Dawa na vifaa mbalimbali vikiwa katika banda la MSD katika kongamano hilo.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI

 WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

JESHI LA POLISI TANZANIA



       TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

   “PRESS RELEASE” TAREHE 16.10.2015.


·         MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA NA MTOTO WAKE KUTOKANA NA MGOGORO WA KIFAMILIA.



·         MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA JANGURUTU AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI WILAYANI MBARALI. 


KATIKA TUKIO LA KWANZA:

MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA MWASHIWAWALA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA DICKSON KAWAWA (50) ALIUAWA KWA KUPIGWA KWA VIPANDE VYA MATOFALI NA MTOTO WAKE AITWAE   SIKU DICKSON (20) MWENDESHA PIKIPIKI @ BODABODA, MKAZI WA MWASHIWAWALA. 


TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 15.10.2015 MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA MWASHIWAWALA, KATA YA IWINDI, TARAFA YA USONGWE, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI, MKOA WA MBEYA.


CHANZO CHA KIFO HICHO NI KIPIGO NA KUTOKWA DAMU NYINGI BAADA YA MAREHEMU KUKATAZWA NA MTOTO WAKE KUNYWA POMBE KWA MUDA MREFU NA KUKAIDI. MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA UPELELEZI WA TUKIO HILI UNAENDELEA.


KATIKA TUKIO LA PILI:

MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA JANGURUTU WILAYA YA MBARALI AITWAYE JAILOS GOYAGE (56) AFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T. 888 BRD AINA YA TOYOTA LAND CRUISER IKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE OMARY NURU (36) MKAZI WA MPAKANI UBARUKU.


TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 15.10.2015 MAJIRA YA SAA 20:00 USIKU HUKO KIJIJI CHA JANGURUTU, KATA NA TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. DEREVA AMEKAMATWA.


KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANAFAMILIA KUTATUA MIGOGORO YAO KWA KUKAA MEZA YA MAZUNGUMZO. PIA ANATOA WITO KWA WANANCHI KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA. AIDHA ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA/MICHORO NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
 Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]


KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

KAMISHENI YA HAKI ZA BINADAMU YA UMOJA WA MATAIFA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI

$
0
0
  Mwakilishi wa  Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, akizungumza  siku ya Alhamis Usiku, muda mfupi  kabla ya  kuonyeshwa kwa filamu ya "the Boy from Geita" ambayo inaelezea uovu wanaotendewa watu wenye ulemavu hususani watoto Nchi Tanzania. Katibu Mkuu  Msaidizi wa ofisi ya Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa,  Bw.  Ivan Simonvic wapili kutoka kushoto alitambua mchango wa serikali katika kuukabili uovu dhidi ya  watu wenye ulemavu wa ngozi   na akahidi  Taasisi hiyo na  nyingine za Umoja wa Mataifa  ushurikiano na  Serikali. wa Kwanza ni  Bw. Peter Ash mwanzilishi na Mkurugenzi wa  Asasi ya  Unter the Same Sun na  karibu na Balozi  ni  mwakilishi kutoka Uwakilishi wa Kudumu wa Canada katika  Umoja wa Mataifa
Sehemu wa wageni  waalikwa  waliofika kuangalia filamu ya "the Boy from Geita" iliyonyeshwa Alhamisi usiku hapa  Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. 

Na  Mwandishi Maalum, New York
SIKU moja  baada ya  Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kuelezea kwa waandishi wa habari juhudi zinazofanywa na serikali dhidi  uovu wanaofanyiwa  watu wenye  ulemavu wa ngozi.

Kamisheni  ya   Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa (UNHR ) imesema itashirikiana na  Serikali ya Tanzania katika  juhudi hizo   za kuukabili  ouovu  unaofanywa dhidi ya  jamii  hiyo ya watanzania.


Kauli hiyo  imetolewa Alhamisi  usiku   na   Katibu Mkuu Msaidizi wa Ofisi ya Kamisheni ya Haki za  Binadamu, Bw.  Ivan Simonovic   muda mfupi kabla ya kuonyeshwa kwa filamu ya “ the Boy from Geita”.


Bw. Ivan Simonovic  amesema,  ushirikiano huo ni katika kutambua juhudi zinazofanywa na  serikali katika siyo  tu  kwa kuhakikisha tatizo hilo linatoweka lakini pia kwa kuwachukulia hatua za kisheria wale wote wanaohusika  na ukatili huo.


“Tofauti na  nchi nyingine,  Serikali ya Tanzania imeonyesha ujasiri na uthubutu  wa kukabiliana na uovu unaofanywa dhidi ya watu wenye ualibino. Ni  kwa kutambua juhudi hizo  tutashirikiana  na serikali katika kukomesha  uovu huu” akasema Bw. Simonovic.


Kauli ya  Bw. Ivan Simonovic ya kutambua juhudi hizo za serikali,  kumetokana na  shuttle diplomacy iliyofanywa na  Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania, Balozi Tuvako  Manongi ya kuonana na  wakuu wa Idara ambazo zimefadhili  kuonyeshwa kwa filamu hiyo hapa Umoja wa Mataifa,   pasipo kuushirikisha  wala  kuujulisha  Uwakilishi  wa Tanzania.


Aidha  maelezo ya awali kuhusu  filamu hiyo  yanaupotoshaji wa baadhi ya mambo  hali iliyomfanya Mwakilishi huyo wa Tanzania katika  Umoj wa Mataifa kuchukua  fursa ya  kuyatolea ufafanuzi.


“Usiku huu   ninapenda kutambua juhudi zinazofanywa na  Moja ya nchi Mwanachama  wa Umoja wa Mataifa, Tanzania, ambayo Mwakilishi wake  Wakudumu Balozi Tuvako  Manongi  yupo  pamoja  nasi.  Siyo tu kwamba  Tanzania imeonyesha  ujasiri na uthubutu wa kutambua ukubwa wa  tatizo linalowakumba watu wenye  ualibino   lakini  pia  imefanya juhudi za kuwaelimisha wananchi wake huku ikuchukua hatua muhimu” akasema Bw. Ivan Simonovic.


Akaeleza zaidi kwamba  kama watakavyoona kwenye   filamu hiyo. Waziri Mkuu  wa Tanzania  Mhe. Mizengo  Pinda amekuwa msemaji  na  mtetezi wa haki za watu wenye ualibino  kwa kufanya  ziara za kutembelea maeneo mbalimbali ya nchi kuhimiza   na  kuelimisha wananchi kuachana na  ukatili huo.


“Kujituma kwake  na namna anavyolichukulia tatizo hili kwa uzito wa aina yake,  ni ushahidi wa namna  gani Tanzania  inavyokabiliana na changatomo hii.  juhudi hizi zimeleta matokeo chanya ambapo    hakuta taarifa za matukio ya kuvamiwa watu wenye ualibino  katika miezi ya hivi karibuni.


 “ Ofisi ya Haki za Binadamu inakaribisha na kutambua juhudi hizo za serikali ya Tanzania katika kukabiliana na Ubaguzi. Mfumo mzima wa Umoja wa  mataifa upo tayari kuwaunga mkono” akasema  katibu Mkuu  Msaidizi.


Alipopewa  nafasi ya kuzumgumza mbele ya  hadhara hiyo. Balozi Tuvako Manongi   kwanza,  alimshukuru Katibu Mkuu  Msaidizi kwa kutambua mchango wa serikali,  na pia kumpatia fursa ya kuja kuzungumza na kutoa fafanuzi kwa niaba ya serikali yake.


Balozi Manongi, alirejea kauli  aliyoitoa mbele ya  waandishi siku ya jumatano, kwamba, Tanzania  haikatai na wala haipingi kwamba kuna tatizo kwa  watu wenye ualibino.


Akasema  pamoja na kukiri kuwapo  kwa matukio  ya uovu dhidi ya watanzania hao, lakini  angependa pia kuweka rekodi sawa  na hasa kufuatia  maelezo  ya upotoshaji ambayo yametolewa kwenye vipeperushi vinavyoitangaza filamu hiyo.


Baadhi ya mambo ambayo Balozi  ameyatolea ufafanuzi  ni lile linaloelezwa  na waandaji wa filamu  hiyo  kuwa  eti  ualibino  ualianzia Tanzania  miaka 2000 iliyopita  jambo analosema    halijathibitishwa kisayansi.


 Akafafanua pia kwamba,  Watanzania ni waumini wa dini ya kiislamu au wakristo , kwa hiyo kusema   kuwa sehemu kubwa ya watanzania wanaamini katika uchawi halina mashiko. 


Akasema kwamba si  sahihi pia kueleza kwamba wazazi ni washirika katika kutenda  maovu dhidi ya watoto wao wenye ualibino.  Amefafanua pia kuwa neno zeruzeru ni tafsri ya  Kiswahili ya neno alibino na kwamba tafsri inayotolewa na waandaji hao ni  upotoshaji.

Balozi Manongi  pia amekanusha  taarifa zilizoelezwa na waandaji hao kwamba Asasi ya Under the Same Sun, ilipokuja Tanzania mwaka 2007  haikukuta  chama chochote cha kuwasema watu wenye ualibino si  kweli. Kwani  chama cha Tanzania Albinism Society ( TAS) kimekuwapo tangu mwaka 1978 na kimekuwa kikiendesha shuguli zake kwa kushirikiana na serikali.


“ Mashambulizi dhidi ya watu wenye ualibino nchini Tanzania,  ni  makosa ya jinai, yanayofanywa na watu  binafsi ambao wamejawa na mawazo  uovu ambayo yanaweza tu kuthibitishwa na vyombo yha sheria” akasisitiza Balozi.


Na kuongea kwamba  Tanzania inaheshimu haki za binadamu na utawala wa sheria na kwa kuheshimu  huko  haiwezi kutoa hukumu kiholela  bila ya kufuata mkondo wa sheria.


Akifafanua Zaidi kwa takwimu Balozi Manongi amesema  watu bilioni moja au Zaidi wenye aina mbalimbali za ulemavu, asilimia 80 wanatoka  nchi zinazoendelea. Na kwamba kwa mujibu wa sensa ya watu iliyofanyika  nchini, watu  2.6  milioni sawa na asilimia 5.8 ya idadi yote ya watu wana aina moja ama nyingine ya ulemavu. Kati yao 16,477 au 0.04 asilimia wana ualibino.


Wakati wa kipindi cha majibu na maswali baadhi ya  watizamaji walihoji sababu ya waandaji wa filamu hiyo kuionyesha  Marekani ili hali kwamba katika  Marekani yenyewe  pia  kuna vitendo  vya  ubaguzi   wa hali ya juu yakiwamo matukio ya watu  kuuwa.


Wengine walitaka kujua ni watu gani wanaonunua viungo vya watu wenye ualibino  swali lililojibiwa na waandaji wa filamu hiyo kuwa ni   ni matajiri  wakiwamo wanasiasa  kiuhalifu. Wakasema pia kwamba  ni watanzania wachache ambao bado wanaimani potofu dhidi ya watu wenye ualibino, huku wakibainisha  uhuru wa vyombo vya habari nchi Tanzania imechangia kwa kiasi kikubwa  kufahamika kwa madhila wanayofanyiwa watu wenye  ualubino.

UCHAMBUZI WA HABARI ZA MAGAZETI TOKA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISHENI OKTOBA 16, 2015

$
0
0
Huu ni uchambuzi wa Habari za Magazeti toka vituo mblimbali vya Televisheni October 16, 2015

TBC
Magufuli Ataja Tiba ya Ajira na Foleni Dar, Msajili wa Vyama Aonya wanaotaka kubaki vituoni. Ungana nasi upate dondoo za magazeti ya leo. https://youtu.be/E83liI7wTOM

Star TV
Mwenyekiti mwenza wa UKAWA Afariki Dunia, Ujenzi Barabara ya Juu Dar kuanza mwezi ujao, kwa hayo na mengine mengi habarika hapa. https://youtu.be/cXwsSqS_iAc

CH 10
Lowassa ainyooshea kidole NEC, Magufuli kuwasainisha mikataba mawazili wake, Magufuli ataja Mafisadi CCM. Pata dondoo hizi zaidi hapa. https://youtu.be/gwXZTku5k6w

Azam TV
Chopa iliyobeba makada CCM Yaanguka Selous, Mtuhumiwa kesi ya Bilionea Msuya aeleza alivyoteswa. Habarika kwa yaliyojiri hapa. https://youtu.be/D5SDMREvh9Q

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA MAKAMBI YA WAKIMBIZI MKOANI KIGOMA

$
0
0
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kulia) akizungumza na uongozi na watendaji wa Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma alipofanya ziara wilayani humo kwa ajili ya kukagua Kambi ya Nduta wilayani humo pamoja na Kambi za Mtendeli na Karago wilayani Kakonko ambazo zipo katika maandalizi ya kuwapokea wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa kwa muda katika Kambi ya Nyarugusu mkaoni humo. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Ruth Msafiri.
  Watoto wa Wakimbizi kutoka Burundi wakiwa katika Kambi ya Wakimbizi ya Nduta ambapo wanahifadhiwa.
Baadhi ya mahema yanayojengwa katika Kambi ya Wakimbizi ya Nduta wilayani Kibondo mkoani Kigoma ambayo yatatumika kuwahifadhi wakimbizi kutoka Burundi wanaoendelea kuwahamishiwa kambini hapo kutoka Kambi ya Nyarugusu ambapo walikuwa wamehifadhiwa kwa muda.

Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

LUKUVI AMEMBEZA MPINZANI WAKE KATIKA JIMBO LA ISMANI

$
0
0

MGOMBEA ubunge wa jimbo la Ismani kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) William Lukuvi 

Na fredy mgunda,Ismani
MGOMBEA ubunge wa jimbo la Ismani kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) William Lukuvi amembeza mgombea mwenzake anayegombea ubunge kwenye jimbo hilo kupitia chama cha demokrasia na maendeleo chadema Patrick Olle Sosopi na kusema kuwa Sosopi hata afanye hawezi kuvaa viatu vyake kwa kuwa mbunge wa jimbo hilo.

Kauli ya Lukuvi aliitoa juzi wakati akiwahutubia wananchi wa vijiji vya Igingilanyi,Kising’a,Kinywang’anga,Mkungugu,Matembo na Ilambilole vilivyopo tarafa ya Isimani katika Jimo la Ismani alisema kuwa Sosopi hawezi kuvaa viatu vyake kwa kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa maana hana staha ya kuweza kuwashawishi wananchi kuwaletea maendeleo na badala yake anawabeza wagombea wa chama cha mapinduzi CCM pamoja na mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa kusema kuwa kwa kipindi cha miaka 20 ya ubunge wa Lukuvi hakuna maendeleo yoyote yaliyofanywa na chama hicho.

 “Mimi kiatu change navaa namba nane Sosopi anavaa namba moja hivi kweli ataweza kuwa mbunge wa jimbo hili?alihoji huku akishangiliwa sana na wananchi hao,kiukweli niwaambie kama mnataka maendeleo kichagueni CCM ndicho chama pekee kitakachowaletea maendeleo na sio chama kingine.”alisema Lukuvi.
Kusoma zaidi bofya HAPA NA KUONA TIMU BAJAJ SIMIYU  BOFYA HAPA.

UCHAMBUZI WA HABARI TOKA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISHENI OKTOBA 16, 2015.

$
0
0
SIMUtv: Utambue mpango wa kujitolea kuwasaidia watanzania kiafya ikiwemo magojwa ya saratani ya matiti na magojwa mengine yasioambukizwa:Huu ni uchambuzi wa Habari toka vituo mbalimbali vya Televisheni October 17, 2015.

SIMUtv: Fuatilia namna ambavyo vuguvugu la kampeni za uchaguzi Mkuu linavyoweza kusababisha vurugugu siku ya uchaguzi https://youtu.be/EUyKaqh2fgQ

SIMUtv: Tambua ni kwa kiasi gani sera za wagombea kutoka vyama mbalimbali zimegusia saula la kupunguza ajari za barabarani: https://youtu.be/hnHRM2cXuY4

SIMUtv: Fuatilia namna serikali ilivyojipanga kulinda amani ya Nchi zikiwa zimesalia sikiu chache kuelekea uchaguzi Mkuu: https://youtu.be/otIRUog8MTY

SIMUtv: TFF yaunda kamati maalumu itakayoshugulikia mwenendo na maandalizi ya timu ya soka Taifa Stars kukabiliana na michuano ya kimataifa https://youtu.be/H5oCwIy6gcc

SIMUtv:  Mgombea uraisi CCM Dkt. Magufuli aahidi kudumisha muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulioanzishwa na Baba Wa Taifa https://youtu.be/_ReVGfr6qHI

SIMUtv: Waangalizi 86 wa Uchaguzi toka Nchi wanachama wa SADC kutawanywa katika mikoa 25 kuangalia mwenendo wa Uchaguzi Mkuu https://youtu.be/vRovhW4YHSU

SIMUtv: Mgombea Uraisi CHADEMA adai tume ya Taifa NEC kuwa chanzo cha kusababisha vurugu endapo itashindwa kubainisha idadi ya wapiga kura. https://youtu.be/JU-OUxS5rvI
SIMUtv: Serikali kupitia mfuko wa bima ya afya wafungua kituo cha afya mkoani Dodoma itakayosaidia kuongeza wigo wa huduma za figo nchini https://youtu.be/jSYcr4neIGM
SIMUtv: Kutotambulika  kisheria kwa wasaidiza wa sheria nchini kumechangia kwa kiasi kikubwa wananchi kushindwa kupata haki zao kwenye vyombo vya sheria; https://youtu.be/tv-fKzYyGvA

Serikali yasaini mkataba na serikali ya China kwajili ya mradi wa ujenzi wa barabara za juu  katika eneo la TAZARA;https://youtu.be/oHaYxYCvtsc

SIMUtv:  Serikali kupitia mfuko wa bima ya afya wafungua kituo cha afya mkoani Dodoma itakayosaidia kuongeza wigo wa huduma za figo nchini https://youtu.be/jSYcr4neIGM
SIMUtv: Kutotambulika  kisheria kwa wasaidiza wa sheria nchini kumechangia kwa kiasi kikubwa wananchi kushindwa kupata haki zao kwenye vyombo vya sheria; https://youtu.be/tv-fKzYyGvA

SIMUtv: Serikali yasaini mkataba na serikali ya China kwajili ya mradi wa ujenzi wa barabara za juu  katika eneo la TAZARA; https://youtu.be/oHaYxYCvtsc

INAUGURATION OF 2015 UWEZO ANNUAL LEARNING ASSESSMENT IN HANDENI DISTRICT

$
0
0
Uwezo annual learning assessments are citizen-led assessments, aimed at collecting household data on children’s mastery levels of reading and arithmetic. On 14th October, 2015, Twaweza inaugurated this assessment for Handeni District. 

The Handeni District Commissioner, Honorable Husna Rajab Msangi, emphasizes a point during the inauguration of a two-days training of community volunteers who are prepared to undertake the Uwezo Annual Assessment on literacy and numeracy in Handeni Town Council. The workshop was held on 14th October, 2015 at Bwawani Hotel, in Handeni.
 Mr. Musa Gunda, the facilitator of the Uwezo Annual Assessment for 2015 volunteers’ workshopcoordinated by Twaweza, clarifies a point during the session. The workshop was held on 14th October, 2015at Bwawani Hotel, Handeni District.
Participants of the Uwezo Annual Assessment for 2015 volunteers’ workshop prepare to present their group work. The workshop was held on 14thOctober, 2015at Bwawani Hotel, Handeni District. 
(Photos by Masozi Nyirenda)

BENKI YA POSTA YABORESHA ZAIDIN HUDUMA ZAKE, MTEJA ATATOA MAONI BILA KUANDIKA KWENYE KARATASI, NI "KUBOVYA TU" KWENYE MASHINEAKATHE

$
0
0
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, TPB, Sabasaba Moshingi(wapili kulia), akihudumia wateja kwenye tawi la benki hiyo Kijitonyama jijini Dar es Salaam, leo Ijumaa Oktoba 16, 2015, kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja ya benki hiyo. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)

NA K-VIS MEDIA

KATIKA kuhakikisha inatoa huduma bora kwa wateja wake hapa nchini, Benki ya Posta Tanzania, imeweka mashine maalum ambayo wateja wa benki hiyo wanaofika kupatiwa huduma watatoa maoni yao juu ya huduma wazipatazo kwa kubonyeza vitufe vinavyoelekeza nini maoni yake juu ya huduma aliyoipata.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja ya benki hiyo, kwenye tawi lake la Kijitonyama jijini Dar es Salaam, Oktoba 16, 2015, Aisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Sabasaba Moshingi alisema, benki yake imelenga kutoa huduma zilizo bora na za kisasa ili kurahisisha utendaji wake wa kazi.

Moshingi ambaye aliongoza maafisa wa benki hyo kutoka makao makuu kwa kutoa huduma kwa wateja, kuwasikiliza na kuwasaidia namna ya kujaza fomu na kutoa pesa, alisema,hatua ya yeye kuongoza maafisa wake kutoa huduma, ni kuwaonyesha wateja kuwa benki yao inawajali.
“Ili kufanikisha lengo hili benki imeanzisha matumizi ya mashine za kisasa zitakazomuwezesha mteja kutoa maoni ya jinsi gani anafurahia au kutofurahia huduma zetu bila kuhitaji kuandika kwenye karatas, mteja atabofya kitufe ili kupata maoni yake, nasi tutayafanyia kazi maoni yake haraka iwezekanavyo.”i.” Alisema Moshingi.
Alisema matumizi ya mashine hizo yataboresha utoaji huduma za kibenki, na hivi sasa mipango ya kuziweka kwenye kila tawi inaendelea.
 Moshingi akimuelekeza mteja namna ya kujaza fomu za kuweka pesa.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

RAIS TFF ATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA MAKAIDI

$
0
0
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi (Anayehojiwa na waandishi wa habari pichani)ametuma salamu za rambirambi kwa Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa kiongozi wa klabu hiyo Emmaneul Makaidi aliyefariki Dunia jana mkoani Lindi.
Katika salam zake, Malinzi amewapa pole wafiwa, ndugu, jamaa, marafiki, wapenzi wa klabu ya Simba pamoja na wadau wa mpira wa miguu nchini, kufuatia kifo hicho cha kiongozi huyo.
Marehemu Emmanuel Makaidi alipata kuwa kiongozi wa klabu ya Simba 1960-1970 katika nafasi mbalimbali zikiwemo nafasi za Katibu mwenezi, Katibu Mkuu na kukaimu Uenyekiti wa klabu ya Simba kabla ya kujiunga na masuala ya kisiasa.
Kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini na watanzania, TFF inawapa pole wafiwa na kuwatakia faraja katika kipindi hichi cha maombelezo.

BUKOBA VETERAN KUCHEZA MCHEZO WA KIRAFIKI KESHO JUMAMOSI 17.10.2015 NA BUSWELU VETERAN

$
0
0
Bukoba Veteran kucheza mchezo wa Kirafiki kesho jumamosi 17.10.2015 kwenye Uwanja wa shule ya seminari ya Ntungamo Bukoba na Timu ya Buswelu Veteran kutoka Jijini Mwanza. Mtandao wa Bukobasports.com ukiongea na Nahodha wa Timu hiyo Kepteni Mwinyi Rajab umeelezwa kwamba mpambano huo wa kirafiki utapigwa kesho jioni na amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi katika Viwanja hivyo. Pia ameweza kuongeza kuwa kutapigwa mtanange mwingine wa kirafiki utaochezwa kesho yake jumapili 18.10.2015 kwenye Uwanja huo kuanzia 10:00 jioni. Bukoba Veteran Sports Club ni umoja wa wanamichezo waliowahi kucheza klabu mbalimbali zikiwemo za Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara maskani yake yakiwa mjini Bukoba, Kagera.
Baadhi ya Wachezaji wa Timu ya Bukoba Veteran yenye maskani yake mjini Bukoba.
Maandalizi hayo ni pamoja na kujiandaa na Mtanange mkubwa wa Kirafiki kati ya Bukoba Veteran na Masaka Veteran utakaofanyika mwezi ujao tarehe 28.11.2015 huko Kampala Uganda.Wapenzi wa Soka Mjini Bukoba mnaombwa kujiokeza kwa wingi katika safari hiyo ya Masaka mwezi ujao na kwa kujua zaidi ya safari hiyo mnaombwa kuwasiliana na Uongozi wa Bukoba Veteran kupitia kwa Nahodha wa Timu hiyo au Viongozi wake.
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images