Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

UCHAMBUZI WA MAGAZETI KUTOKA VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI

$
0
0
Huu ni uchambuzi wa Habari za Magazeti toka vituo mblimbali vya Televisheni October 14, 2015

TBC 
NEC Yatumia Mfumo Mpya, ni mfumo wa kujumlisha matokeo, Dkt. Magufuli aomba kura kwenye Mabasi. Pata dondoo hizi za magazeti ya leo hapa. https://youtu.be/4I5dO8epJR8

Star TV
Magufuli Aahidi Bima Ya Afya Kwa Wananchi, Lowassa Kupigania Mikataba ya Madini, Mahujaji wengine 4 wagundulika kufariki. Habarika hapa zaidi. https://youtu.be/qqM7snXi8kM

CH 10
Lowassa ageukia Madini, JK awajia Juu Viongozi Wabovu, Lowassa na Dkt Slaa waua Katiba Mpya UKAWA, Pata uchambuzi zaidi wa magazeti hapa. https://youtu.be/lVEXj7JCT9Y

Azam TV
Tambwe Abaki Burundi, Hofu yatanda, Van Perse na Depay wazichapa mazoezini, kiiza ajitoa mechi ya mbeya City. Pata dondoo za habar za Michezo. https://youtu.be/viEey0srbBQ




DUNIA YAHIMIZWA KUWAJIBIKA KWA AJILI YA AMANI

$
0
0
IMG_5771
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kushiriki katika kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa. ( Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Na Mwandishi wetu
JUMUIYA ya Kimataifa imetakiwa kuwajibika kuhakikisha kwamba wanaweza kuwepo na amani na usalama kwa kuwa hilo ndilo tatizo kubwa duniani.
Hayo alisema Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard membe katika kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
Hafla hiyo imefanyika viwanja vya Mnazi Mmoja mapema zaidi kuliko tarehe iliyopaswa ya Oktoba 24 kutokana na Tanzania kuwa katika mchakato wa uchaguzi.
Waziri Membe alisema kwamba dunia kwa sasa ipo katika changamoto kubwa ya usalama kutokana na mizozo inayoendelea katika nchi kadhaa duniani.
Alisema kumekuwepo na wimbi kubwa la mapigano ndani ya nchi mbalimbali katika nchi mashariki ya kati, Ulaya na hata Afrika, kukua kwa ugaidi na siasa za kibaguzi.
“ Sote tunafahamu shida iliyopo katika nchi kama Syria, Iraq, Somalia, Libya, Afghanistan, Yemen na jamhuri ya Afrika Kati” alisema waziri Membe na kuongeza kuwa matukio ya vita ya mara kwa mara, misimamo mikali na ugaidi vimekuwa vikisababisha vifo vingi na mateso kwa jamii.
Kutokana na hali ilivyo kwa sasa dunia haiko katika hali ya amani na hivyo juhudi zaidi zinatakiwa kufanyika ili kurejesha amani ambayo ni kiungo muhimu katika maendeleo.
Pamoja na kuzungumzia haja ya amani kutokana na dunia sasa hivi kufikia kiwango cha juu cha wakimbizi ndani na nje ya nchi zao, Waziri Membe alihimiza mabadiliko katika uendeshaji wa Umoja huo ili kuleta uwiano wa uwajibikaji kimataifa.
IMG_5783
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe akisalimiana na baadhi ya wakuu wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa nchini huku akiwa ameambatana na pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Liberata Mulamula (kushoto).

KUMBUKUMBU YA MIAKA 2 YA KIFO CHA ELIFADHILI MKAZE MNZAVA

$
0
0
KUMBUKUMBU YA MIAKA 2 YA ELIFADHILI MKAZE MNZAVA


Mpendwa mume wangu, leo umetimiza miaka 2 tangu ulipotangulia nyumbani kukaa na Bwana Yesu. 

Tunamshukuru Mungu kwa kutupa sehemu ya maisha yako ambayo yamekuwa ni baraka kubwa kwetu. Tunakukumbuka kwa upendo wako, ukarimu na uwajibikaji wako.


Daima unakumbukwa na mimi mkeo, watoto wako, wakwe zako, wajukuu wako, ndugu na marafiki. Pumzika kwa amani tutaonana tena Mbinguni kwa Baba.


FANYENI KAZI KWA BIDII ILI MUWEZE KUJILETEA MABADILIKO YA KWELI KATIKA MAISHA YENU - MAMA SALMA KIKWETE

$
0
0
Na Anna Nkinda – Maelezo, Liwale
14/10/2015 Wananchi wa mkoa wa Lindi wameaswa kufanya kazi kwa bidii ili waweze kujiletea mabadiliko ya kweli katika maisha yao kwani kuna baadhi ya watu hawapendi kufanya kazi huku wakisubiri mabadiliko.

Rai hiyo imetolewa jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea kwa nyakati tofauti na wananchi wa  vijiji vya Ngunichile na Mbaya vilivyopo katika majimbo ya Nachingwea na Liwale (Pichni)waliohudhuria mkutano wa kampeni ya kuwanadi wagombea wa nafasi za udiwani, ubunge na urais kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mama Kikwete ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kupitia wilaya ya Lindi mjini alisema mabadiliko ya kweli hayawezi kupatikana bila ya kufanya kazi kwani kuna baadhi ya watu hasa vijana hawafanyi kazi wakiamka asubuhi kitu wanachokifanya ni kucheza  pool huku wakisubiri mabadiliko.

“Hata katika vitabu vya dini imeandikwa asiyefanya kazi na asile kwani kazi ni msingi wa maendeleo,  hata ukipiga kelele kiasi gani kama hufanyi kazi huwezi kupata mabadiliko katika maisha yako”.

“Ndugu zangu Mwenyezi Mungu ametupa akili ya kutambua mema na mabaya tusikubali kudanganywa, mabadiliko ya siku hizi siyo mazuri yanaleta uvunjifu wa Amani kwani watu wamepandikizwa maneno ya chuki wanafanya vurumai na kuharibu vya kwao, wanawachukia ndugu zao imefikia hatua watu hawazikani, hawasalimiani. Lakini hao aliowapandikiza chuki kwao kuna maendeleo”, alisisitiza.

MAHOJIANO NA WAASISI WA JABALI AFRIKA

$
0
0
Wawili kati ya waanzilishi wa JABALI AFRIKA, Justo Asikoye na Joseck Asikoye walipata fursa ya kutembelea Kilimanjaro Studio zilizopo Beltsville Maryland na kuzungumza na Mubelwa Bandio na Dj Luke Joe kuhusu kazi zao
Ilikuwa ni katika kipindi cha MISHUMAA YA KALE kinachosikika kila Ijumaa kuanzia saa 11 jioni kwa saa za Marekani ya Mashariki
KARIBU

ZADIA YAUNGA MKONO MSIMAMO WA KIZALENDO WA MH. OTHMAN MASSOUD OTHMAN

$
0
0
TAARIFA
Alipokuwa akizungumza kwenye kongamano maalum huko Zanzibar, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mh Othman Massoud Othman alielezea wajibu wa kila Mzanzabari wa kuutetea umoja wa Wazanzibar.

Akifafanua kifungu cha 23 cha Katiba ya Zanzibar, Bw. Othman alielezea kuwa, mbali na Katiba hiyo kutoa haki sawa kwa Wazanzibari wote, pia inatoa wajibu kwa wananchi.
Miongoni mwa wajibu wa kila Mzanzibar kwa mujibu wa Kifungu hicho, ni wajibu wa kulinda, kuhifadhi na kudumisha Uhuru wa Zanzibar, Mamlaka ya Zanzibar, Ardhi ya Zanzibar na Umoja wa Zanzibar.

Maelezo hayo ya Othman, yanakwenda sambamba na malengo makuu ya Jumuiya ya Wazanzibar waishio nchini Marekani (ZADIA).

Kwa hivyo, ZADIA inapenda kuchukua fursa hii kumpongeza na kumuunga mkono Mheshimiwa Othman Massoud Othman kwa kauli zake hizo za kizalendo alizozitoa tarehe10/10/215 mjini Unguja.
Bwana Othman alikumbusha jinsi alivyotekeleza wajibu wake huo wa kikatiba kivitendo kwa kupiga kura "kama alivyopiga" kwenye Bunge Maalum la Katiba kule Dodoma.

Aidha, alifafanua kasoro zilizomo kwenye Katiba pendekezwa ya Tanzania ambazo alizielezea kuwa hazina maslahi kwa Zanzibar.

Kitendo hicho cha kijasiri, na maelezo hayo, vinatoa changamoto kwa Kila Mzanzibar kuiga mfano huo. Nasi Wanadiaspora tumezipokea kwa moyo wote changamoto hizo na kuzifanyia kazi kama ambavyo imekuwa kawaida yetu. Natutafanya juhudi zote na tutashirikiana na wadau wote, ili kuhakikisha kuwa Zanzibar inapata hadhi yake na haki zake ndani ya Muungano wa Tanzania.
Omar H. Ali,
Mwenyekiti,
ZADIA.
zadiaspora@gmail.com
215 459 4449

PRESIDENT KENYATTA ADDRESSES EALA

$
0
0

 The President signs the visitors book at the Kenya National Assembly as the EALA Speaker, Rt. Hon Daniel F. Kidega and the Cabinet Secretary for East African Affairs, Commerce and Tourism, Hon Phyllis Kandie look on.
 The President of the Republic of Kenya, H.E. Uhuru Kenyatta addresses an attentive House.

 East African Legislative Assembly 
PRESIDENT KENYATTA ADDRESSES EALA

Lauds Assembly for improved performance, calls for more citizenry participation
East African Legislative Assembly, Nairobi, Kenya, October 14, 2015:  President Uhuru Kenyatta has today addressed EALA, calling on the Assembly to consolidate its work for the furtherance of the integration process.  President Kenyatta further said the citizens of the region were yearning to freely move, work and enjoy the tangible benefits of integration.

The President was addressing a Special Sitting of the 2nd Meeting of the 4th Session of the 3rd Assembly which commenced in Nairobi last week.

The President reiterated his commitment and that of his Government to the integration process. “I will begin by repeating my Government’s complete commitment to East African integration. I know that the future of each of us in the region is bound up with the fate of all the rest.  Leaders must create the laws, the institutions, and the framework that will help us face that future together.  Kenya will play its part in that great task”, President Kenyatta said.

The President further urged stakeholders in the integration dispensation to go the extra mile and create awareness to the citizens of the region. He remarked that citizens of the region needed to be fully aware of the integration process. He said this was a role to be undertaken by both politicians and the ordinary people as well.

“I wish to make is that we who are convinced of the imperative of integration must communicate it better to our people.Too often, the integration of East Africa is taken to be merely a political matter - a job for politicians, not ordinary people.  True, leaders must lead.  But we have failed to spark the imaginations of East Africans when it comes to integration”the President remarked.

WATAKIWA KUCHANGIA UJENZI WODI YA AKINAMAMA

$
0
0
Mgombea Ubunge kushoto Ridhiwani Kikwete akimkabidhi ilani ya uchaguzi ya CCM mgombea udiwani wa kata ya Kimange wakati wa uzinduzi wa kampeni za udiwani kwenye kata hiyo katika Kijiji cha Pongwekiona 

Na John Gagarini, Chalinze
WAKAZI wa Kijiji cha Pongwe Kiona Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo wametakiwa kushirikiana na serikali ili kukamilisha ujenzi wa wodi ya akinamama.

Hayo yalisemwa na mgombea Ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhiwani Kikwete kwenye Kijiji hicho wakati wa uzinduzi wa kampeni za Udiwani kwenye kata ya Kimange na kusema kuwa kwa sasa hakuna wodi ya akinamama.

Ridhiwani alisema kuwa moja ya vitu ambavyo amevipa kipaumbele ni upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi ikiwa ni pamoja na huduma ya afya ya uzazi ya mama na mtoto ili waweze kuhudumiwa kwa uhakika.

“Nawaombeni wananchi tuungane na serikali kwa kuchangia nguvu zetu kuhakikisha wodi ya akinamama inakamilika kwani kwa sasa hakuna hata chumba cha kujifungulia ambapo wanapojifungua wanachanganyika na wanaume jambo ambalo linasababisha kutokuwa na utu wa mwanamke,” alisema Ridhiwani.

Alisema kuwa heshima ya mwanamke inapotea kutokana na kutokuwa na wodi hiyo ambayo ingewafanya akimama kuweza kujifungulia sehemu ambayo ina wastiri tofauti na ilivyo sasa hakuna stara kwa wanawake.

“Nawaomba mnichague ili niweze kuwa Mbunge wenu niweze kuhamasisha ujenzi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo name nitahakikisha ujenzi huu unakamilika kwa wakati ili kuondoa adha wanayopata akinamama wakati wa kujifungua,” alisema Ridhiwani.

Kwa upande wake Mgombe Udiwani Hussein Hadingoka alisema kuwa endapo atachaguliwa atahakikisha anahamasisha wadau mbalimbali kuweza kuchangia ujenzi huo ambao tayari umeashaanza na uko kwenye hatua ya msingi.

Hadingoka alisema kuwa mbali ya ujenzi huo pia atahakikisha ujenzi wa zahanati za Vijiji kwenye kata hiyo unafanyika kwani baadhi ya vijiji havina zahanati hali ambayo inasababisha changamoto ya wananchi kwenda mbali kupata huduma za kiafya huku ilani ya chama ikisema kuwa kila kijiji kitakuwa na zahanati na kata kuwa na kituo cha afya.

Naye mkazi wa Kijiji hicho Asha Bakari alisema kuwa wodi hiyo ikikamilika itakuwa imewaondolea adha ya kujifungua huku wanaume nao wakiwa kwenye chumba kimoja ambapo hadhi ya mwanamke inapotea.

MABADILIKO KATIKA UPASUAJI WA UVIMBE WA SARATANI

$
0
0
Dk. Umanath Nayak, mshauri mkuu wa  magonjwa ya saratani ya kichwa na shingo pamoja na upasuaji kwa njia ya roboti katika hospitali ya saratani ya Apollo Hyderabad nchini India.

Na Mwandishi Wetu,
SEKTA ya afya duniani imeshuhudia mapinduzi yanayolenga kuongeza umri wa kuishi, ubora wa maisha, njia mbadala za uchunguzi, njia bora za matibabu, na pia ufanisi na ubora katika huduma za afya.
 Teknohama imekuwa na mchango mkubwa sana katika maendeleo ya ndani ya sekta hii muhimu. Makampuni yanayohusika na kutengeneza vifaa vya tiba hivi sasa yanalenga katika kutengeneza roboti ambazo hufanya upasuaji kwa ufanisi zaidi bila madhara makubwa kwa mgonjwa.

Kuna matumaini sana katika upasuaji kwa kutumia teknolojia ya Roboti. Teknolojia hii ni ishara ya mapinduzi katika sekta ya afya, na ni moja ya mambo muhimu yanayoongelewa sana katika upasuaji hivi leo. Mfumo wa upasuaji kwa kutumia roboti umeletwa ili kusaidia katika upasuaji mgumu, ambao hufanyika kwa shida, au unaohusisha maeneo ambayo ni magumu kufikika na hatari. Kwa kutumia mikono maalumu inayopatikana katika Roboti hilo upasuaji huo urahisishwa zaidi.

Mikono ya Roboti hudhibitiwa na kompyuta inayoendeshwa na mpasuaji kwa kutumia mikono na miguu. Udhibiti huu ni sawa na ule wa mchezo wa video, maarufu kama ‘video game’ ambao huwezesha upatikanaji kwa usahihi zaidi wa maeneo magumu kufikika ikilinganishwa na njia iliyokuwa ikitumika awali ya  ‘laparoscopic’. Kutumia matundu madogo sana, upasuaji wa aina hii unaweza kuondoa uvimbe uliojificha pasipo uharibifu wa tishu na pia humsaidia mgonjwa kutokaa hospitalini muda mrefu pamoja kupona ndani ya muda mfupi. Teknolojia hii inapunguza hatari ya uharibifu wa mishipa na tishu katika eneo husika.

TASWA FC HOI KWA NSSF

$
0
0
Na Mwandishi wetu
Timu ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa FC imeshindwa kutamba mbele ya timu ya soka ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF baada ya kufungwa mabao 2-1 katika mechi maalum ya kuadhimisha miaka 16 ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Katika mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa Bora, Kijitonyama, mabao ya NSSF yalifungwa na Linus  Bwegoge kwa shuti la nje ya eneo la hatari kutoka wingi ya kushoto na la pili lilifungwa kwa njia ya penati na Khalfan Waziri baada ya beki wa Taswa FC, Khatimu Nahela kumwangusha kwenye eneo la hatari msambuliaji wa NSSF, Ali Chuo.

Bao la Taswa lilifungwa na Khatimu Naheka baada ya beki wa NSSF, kumchezea rafu mbaya Shadraki Kilasi aliyekuwa anakaribia kufunga.  Katika mchezo, Taswa  Fc ingeweza kusawazisha na kama si kukosa penati kwa mshambuliaji wa Taswa FC, Saidi Seifu ambaye kipa wa NSSF aliipangua.

Penati hiyo ilitolewa baada ya beki wa kati wa NSSF kumwangusha Zahoro Mlanzi aliyecheza vizuri na mshambuliaji wa pembeni wa timu Taswa FC Angetile Osiah ambaye pia alikosa mabao mawili ya wazi baada ya kupiga mpira nje.

Mbali ya Osiah, Seif, Julius Kihampa na Mohamed Akida nao walikosa nafasi nyingi za wazi katika mechi hiyo ambayo wachezaji, Wilbert Molandi, Nurdin Mponda, Jabir Johnson na Simon walicheza vizuri sana.

Mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary alisema kuwa hawajaridhika na kipigo hicho cha mara ya kwanza tokea kuanza kwa mwaka huu na kujipanga upya kwa ajili ya mechi ya marudiano.

JE MALI ILIYOPATIKANA KABLA YA NDOA INAHESABIKA NI YA FAMILIA ?.

$
0
0
MARA  kadhaa  linapoibuka  suala  la  kugawana  mali  pale  ndoa  inapohesabika  kushindikana   masuala  kadhaa  ya  msingi  na  yanayohitaji  uelewa  huwa  yanaibuka. Moja  ya  suala  kati  ya  masuala  ambayo  huibuka  ni  hili  la  kutenganisha  na  kufafanua  hadhi  ya  mali  za  wanandoa  ili  mgawanyo uweze  kufanyika  kwa  haki. Yawezekana  mwanandoa  akadhani  ana  haki  katika  mali  fulani  lakini  kumbe  kisheria  hana  haki  hiyo  ni mtazamo  wake  ndio  unamsukuma  kuamini  hivyo. 

Halikadhalika  yawezekana  mwanandoa  kudhani  hana  haki  katika  mali  fulani  kumbe  anayo  haki.  Ili kujua    una  haki  ipi katika  mali  ipi  na  huna  haki  katika  mali  ipi yahitajika  kujua  misingi  ya kisheria  inayotumika  kugawanya   mali  za  wanandoa.


1.KUGAWANA  MALI  ZA  WANANDOA.
Ieleweke  kuwa  tunapoongelea  wanandoa  kugawana  mali  tunaongelea  talaka. Hakuna  kugawana  mali  bila  talaka. Na  kisheria  talaka  inapotoka  tu swali linalofuata ni  habari  ya  mali  na  watoto  kama  wapo.  Mali  si  lazima  magari  na  manyumba  lakini  pia hata  vyombo  vya  ndani  vikiwemo  vitanda, makabati, sahani  n,k  nazo  ni  mali  kwa  mujibu  wa  sheria. Navyo  huhitaji mgao.


2.  JE  KUGAWANA  MALI  NI  NUSU  KWA NUSU ?.
Linapokuja  suala  la  kugawana  mali  wengi hudhani mtindo unaotumika  kugawa  ni  ule  wa    nusu  kwa  nusu.  Jambo  hili  si  kweli  kwakuwa  sheria  ya  ndoa 1971 iliyofanyiwa  marekebisho  2002  haisemi  kuwa  utaratibu  wa  kugawana  mali  ni nusu  kwa  nusu. Sheria  hii  imeweka  msingi  mkuu  wa  kugawana  mali  ambao  ndio  hutumika  katika  mahakama  zetu  katika  kutoa  maagizo  ya  kugawa  mali  za  wanandoa.  
Kusoma Zaidi soma bofya HAPA  AU BOFYA HAPA

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWAONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGWA MWILI WA MAREHEMU DKT. KIGODA KARIMJEE DAR.

$
0
0
Maafisa wa Bunge wakibebea Jeneza lenye mwili wa marehemu Dkt. Abdallah Kigoda, wakati ulipowasili kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuagwa.
Baadhi ya Wanafamilia wa marehemu Dkt. Kigoda.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Marehemu Dkt. Abdallah Kigoda, wakati wa shughuli ya kuagwa mwili huo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Okt. 15, 2015. Marehemu Kigoda anatarajia kuzikwa leo Jimboni kwake Handeni, mkoani Tanga.
 Picha na OMR

EVERJOBS TANZANIA CAREER REPORT.

$
0
0
In a recent World Economic Forum report, Tanzania was listed as one of the 13 fastest growing economies in the world. This comes as no surprise with GDP growing around 6-7% each year since 2009. In addition, with GDP projected to grow until 2017, many industries will continue to benefit, including the services sector. This latest edition of the everjobs Tanzania career report was assembled based on data collected from  everjobsfor the month of September 2015.



New data from the everjobs Tanzania career report shows that the services industry accounted for the largest number of available job positions in September. Job opportunities in the NGO sector are growing rapidly, followed by Financial Services, and Distribution/Logistics opportunities. Not only are these three categories providing ample employment opportunities, they also seem to be popular among job seekers, receiving almost 40% of applications made. Moreover, the Broadcasting / Music / Film industry was the most popular among job seekers, receiving, 15% of applications made in September.



The financial sector in Tanzania has expanded and become more competitive in recent years. Interestingly, foreign banks are very active in Tanzania, accounting for 48% of total assets in the industry. In addition, the increase in competition has benefited customers, as quality of financial services has increased. “With the projected economic growth, it is likely that this sector will continue to provide many opportunities for job seekers” said Tanzania Country Manager Florens Roell.



The career report also finds that most employment opportunities are located in Dar es Salaam, accounting for 77% of the total. The cities that follow include Arusha and Mwanza.



everjobs is an online job portal, already operating in Cameroon, Ivory Coast, Senegal, Uganda, and Ethiopia. Launched in March 2015, everjobs aims to become the Pan-African recruitment platform. The company is backed by the Africa Internet Group (AIG).

UCHAMBUZI WA HABARI TOKA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISHENI OKTOBA15, 2015.

$
0
0
Huu ni uchambuzi wa Habari toka vituo mbalimbali vya Televisheni October 15, 2015.



SIMUtv: Michuano maalum ya gofu kufanyika jumamosi hii katika viwanja vya Lugalo jijini Dar es Salaam kwalengo ya kuunda kikosi cha taifa; https://youtu.be/yLAoH5MvQ2U

SIMUtv: Waangalizi wa Uchaguzi kutoka SADC wawataka watanzania kuwa watulivu kwa kufuata sheria na kanuni za nchi kuelekea uchaguzi mkuu. https://youtu.be/BOGEYz5goVE

SIMUtv: Watanzania waombwa kudumisha amani, umoja na mshikamano iliyoachwa na muasisi wa taifa Hili Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere. https://youtu.be/im-nOHsCoAY

SIMUtv: Raisi Jakaya Kikwete awataka watanzania kutunza shahada zao za kupigia kura ili kusiriki kikamilifu katika upigaji kura Oktoba 25.  https://youtu.be/tLHVjuI4ai8

SIMUtv: Baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam wamesema ili kumuenzi baba wa Taifa, viongozi na wananchi wanapaswa Kupinga ukabila na udini. https://youtu.be/ettrrIp1zi4

SIMUtv: Mwili wa aliyekuwa waziri wa Viwanda na Biashara Marehemu Dkt. Abdallah Kigoda umewasili jana Nchini kutokea Nchini India. https://youtu.be/8EZt57Ehw-A

SIMUtv: Tume ya Taifa Ya Uchaguzi NEC imezindua kituo cha mawasiliano kitakachosaidia wadau wa uchaguzi kupata elimu ya mpiga Kura. https://youtu.be/KazdhuLzaLM
SIMUtv: Viongozi mbalimbali waungana na wananchi kumuaga aliyekuwa waziri wa viwanda na biashara DR.Abdallah Kigoda  viwanja vya Karemjee https://youtu.be/A3JSkTe9HjQ

SIMUtv: Wadau wa biashara na viwanda nchini watoa salamu za rambirambi kwa familiya ya Dr.Kigoda na wananchi kwa ujumla; https://youtu.be/OyllSiz7MGk

SIMUtv: Anne Makinda aeleza mchango wa hayati Dr.Kigoda katika kamati ya uchumi na fedha pamoja na  kulinda haki za watoto https://youtu.be/JF6feNTGnDs

SIMUtv: Waziri wa mambo ya ndani  Mh.Mathias Chikawae kwa niaba ya Serikali atoa  salamu za rambirambi kwa waombolezaji https://youtu.be/cONLtPUFZcw

SIMUtv: Asha Kigoda, msemaji wa familia ya Dr.Kigoda atoa maneno ya shukrani kwa serikali na kueleza jinsi safari ugonjwa ya waziri ilivyokuwa https://youtu.be/AAjnwfWSArk

SIMUtv: Tambau mambo ya kufanya kabla na baada ya kumalizika kwa uchaguzi Mkuu ambapo zimesalia takribani siku 9 kwa uchaguzi huo kufanyika https://youtu.be/Q6SZSWJaogc

SIMUtv: Yajue mafanikio ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwa mradi wa kilimo wa matrekta wa suma JKT katika kuboresha sekta ya kilimo Nchini https://youtu.be/SdPfaBfR1PE

SIMUtv: Yajue maswali ambayo huulizwa kwa wingi na wananchi kwa Dokta Mwaka kutokana na magojwa mbalimbali yakiwa na ufafanuzi wake pia https://youtu.be/qOdQy8Ho3nI

SIMUtv: Fuatilia mada inayozungumzia elimu ya mpiga kura zikiwa zimesalia siku chache kuelekea uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25: https://youtu.be/JCuUZf32tSA

UCHAMBUZI WA HABARI ZA MAGAZETI TOKA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISHENI OKTOBA 15, 2015

$
0
0
Huu ni uchambuzi wa Habari za Magazeti toka vituo mblimbali vya Televisheni Oktoba 15, 2015.
Channel 10
TBC 
Hatutawavumilia watakaofanya vurugu wakati wa uchaguzi mkuu, Mwili wa waziri Kigoda kuagwa leo. Ndivyo yasemavyo magazeti ya leo;  https://youtu.be/CGjIrO7T8q0

Azam TV
Yanga yaipania Azam fc, Mwingereza,Mholanzi vitani . Pata kujua kile wahariri wa michezo walichokipa kipaumbele siku ya leo; https://youtu.be/31MOwWiwhnI

MLIMANI TV 
Sh.Bilioni 7.8 zatumika ‘kununua’ ikulu. Waratibu walipwa mil.4 kwa mwezi tangu 2013, Mfanyabiashara maarufu nchini adaiwa kuratibu dili, https://youtu.be/yeESunsrHNs

DKT MAGUFULI AENDELEA NA KAMPENI ZAKE LEO, AHUTUBIA KISARAWE,UKONGA NA BAADAE KUHUTUBIA PEMBA

$
0
0
 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akimpongeza mmoja wa wakazi wa Ukonga mara baada kughani shairi lililokuwa likimsifia kuwa ana sifa zote za kuwa Rais wa Tanzania,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika mapema leo asubuhi kwenye uwanja wa mpira wa Moshi Bara,Ukonga jijini Dar
  Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akimpongeza mmoja wa wakazi wa Ukonga mara baada kughani shairi lililokuwa likimsifia kuwa ana sifa zote za kuwa Rais wa Tanzania,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika mapema leo asubuhi kwenye uwanja wa mpira wa Moshi Bara,Ukonga jijini Dar
  Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akiwahutubia wakazi wa jimbo la Ukonga mapema leo mchana kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa mpira wa Moshi Bara,Dkt Magufuli amemaliza mkutano wake wa kampeni jimbo la Kisarawe,Ukonga na baadae anatarajia kuhutubia mkutano wa Kampeni Pemba na Unguja.
 Wakazi wa Ukonga wakishangilia kwenye mkutano huo wa kampeni.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akiwahutubia wakazi wa jimbo la Ukonga mapema leo mchana kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa mpira wa Moshi Bara,Dkt Magufuli amemaliza mkutano wake wa kampeni jimbo la Kisarawe,Ukonga na baadae anatarajia kuhutubia mkutano wa Kampeni Pemba na Unguja.
 Wakazi wa Ukonga wakifuatilia mkutano wa kampeni wa Dkt John Pombe uliofanyika leo mchana kwenye uwanja wa mpira moshi bar.

 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akimwombea kura mgombea Ubunge jimbo la Kisarawe Selemen Jaff mapema leo asubuhi kwenye mkutano wa kampeni
  Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akimwombea kura mgombea Ubunge jimbo la Kisarawe Selemen Jaff mapema leo asubuhi mbele ye Wakazi wa mji huo kwenye mkutano wa kampeni
 Mgombea Urais wa CCM John Pombe Magufuli akionesha picha yake aliyokabidhiwa kama zawadi na mkazi wa Kisarawe mapema leo asubuhi kwenye mkutano wa kampeni.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akihutubia wakazi wa Ukonga mara baada ya kumsimamisha wakitaka awasalimie na wamweleze shida zao ili atakapokuwa Rais aweze kuwasaidia,Dkt Magufuli alikuwa akitokea Kisarawe kwenye mkutano wake wa kampeni.
 Katika hali isiyo ya kawaida vijana walijitokeza kuanza kufuta barabara ya vumbi ili Mgombea Urais Dkt Mafuguli aweze kupita.PICHA NA MICHUZI JR-DAR

WASIMAMIZI WA UCHAGUZI WATENDE HAKI :TAWLA

$
0
0
Ofisa Uchaguzi na Utawala Bora wa Halmashauri ya Kisarawe, Constantene Mnemere, akizungumza na washiriki wa mdahalo wa amani wakati wa uchaguzi kwa watendaji wa Serikali za Mitaa,Polisi na watumishi wa Halmashauri hiyo jana.
Ofisa Habari wa Chama Cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA), Goodness Mrema, akielezea muongozo wa mdahalo wa amani kwa wenyeviti, watendaji wa serikali za mita na Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani jana, wakati wa mdahalo wa kujadili amani wakati wa uchaguzi.

BEI YA MADAFU HII LEO

TANROADS NA KAMPUNI YA SUMITON MITSUI CONSTRACTION CO. LTD WASAINI MKATABA KWAAJILI YA UJENZI WA BARABARA YA JUU ENEO LA TAZARA LEO JIJINI DAR

$
0
0
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara TANROADS Eng. Patrick Mfugale akisoma risala kwa mbele ya wadau wa ujenzi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, mara baada ya kukutana na kusaini mkataba wa ujenzi wa barabara ya juu (Fly over) eneo la Tazara jijini Dar es Salaam mkataba uliosainiwa kati ya Tanroads na kampuni ya Sumiton Mitsui Constraction Co. LTD ya nchini Japan mkutano uliofanyika  jijini Dar es Salaam leo.
Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada akizungumza na wadau wa ujenzi walipokutana kusaini mkataba wa ujenzi wa ujenzi wa barabara ya juu (Fly over) eneo la Tazara jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara TANROADS Eng. Patrick Mfugale wakiwa na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada wakisaini mkataba kwaajili ya ujenzi wa barabara ya juu (Fly over)eneo la Tazara jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli akiwashukuru wadau wa ujenzi leo jijini Dar es Salaam na kuhusiana na kusaini mkataba wa ujenzi wa barabara ya juu (Fly over) maeneo ya Tazara ambao utajengwa na kampuni ya Sumiton Mitsui Constraction Co. LTD ya nchini Japan. 

 
Baadhi ya wadau waliohudhulia mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.

MSANII WA NCHINI KENYA KUTUMBUIZA IJUMAA HII JIJINI DAR

$
0
0
 Msanii wa mziki wa Hip hop wa nchini Kenya ambaye pia ni Daktari nchini humo, Francis Hamis ( a.k.a Frasha) akizungumza leo katika mkutano uliofanyika katika ukumbi uliopo katika jengo la VIVA Tower na waandishi wa habari kuhusiana na kutumbuiza kesho Ijumaa ambapo baada ya kutumbuiza atatembelea vituo kadhaa vya watoto yatima hapa jijini Dar es Salaam ataanza na kituo cha Trust youth Care pia mesema kuwa kiingilio kitakuwa ni shilingi elfu 10 kwa kabla ya saa  sita usiku na baada  ya saa sita kiingilio kitakuwa ni shilingi elfu 15 atatumbuiza katika ukumbi uliopo katika jengo la VIVA TOWER jijini Dar es Salaam. Nyimbo atakazo tumbuiza ni WekaWeka Kutibu pamoja na Dalia.
Kulia ni Meneja mauzo wa kinywaji cha Johnnie worker, Francis Tibaikana akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na vinjwaji vitakavyokuwepo wakati wa msanii Frasha akitumbuiza amesema kuwa chupa moja ya kinjwaji cha Johnnnie Worker itauzwa kwa shilingi laki moja na elfu idhirini badala ya shilingi  laki moja na elfu hamsini. Pia aliwaalika watanzania kuhudhulia wakati wa msanii huyo akitumbuiza na kujipatia ofa za pumbuzo la bei la kinywaji cha Johnnie Worker ikiwa msanii huyo atatumbuiza katika ukumbi uliopo katika jengo la VIVA TOWER jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhulia katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images