Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1000 | 1001 | (Page 1002) | 1003 | 1004 | .... | 3284 | newer

  0 0

  UTAFITI  uliofanywa na magazeti makubwa yanayoaminika nchini Afrika ya Kusini ya Mail na Guardian baada ya kushindanisha makampuni mbalimbali  kutafuta orodha ya makampuni bora na yanayoaminika nchini humo yaliitaja Kampuni ya Vodacom  jana  kuwa ni kampuni inayoongoza kwa kuwa na mtandao bora na wa kuaminika nchini humo.

  Vodacom imetangazwa kutokana na utafiti huo uliofanywa na magazeti hayo katika hafla ya kutangaza makampuni bora ilifanyika jana katika hoteli ya Sandton mjini Johannesburg.

  Utafiti wa magazeti hayo kutafuta makampuni bora ulifanywa kwa ushirikiano na taasisi ya utafiti ya Plus 94 na kampuni kubwa zipatazo 167 zilishindanishwa ambapo kwa upande wa kampuni zinazotoa huduma za mawasiliano Vodacom imekuwa kinara kwa kushika nafasi ya kwanza na kushika nafasi ya tatu kati ya makampuni yote yaliyoshirikishwa kwenye utafiti huo.

  Ushindi huu ni mfululizo kwa kampuni ya Vodacom kwa kuwa hivi karibuni ilitangazwa kuwa mwajiri bora nchini Afrika ya Kusini.

  Mtendaji Mkuu wa Mawasiliano wa Vodacom, Maya Makanjee amesema, “Siri ya mafanikio na kupata ushindi wa tuzo mbalimbali ni kufanya kazi kwa uwazi, umakini na kuwathamini wafanyakazi wake,wateja na wabia wote inaoshirikiana nao katika biashara”

  Makanjee alisema Vodacom inajivunia kwa ushindi huo na unaipa moyo wa kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja na kushiriki katika kusaidia jamii inapofanyia biashara. “Tunazidi kufarijika kwa kupata tuzo mbalimbali na hii inazidi kutupa moyo wa kufanya vizuri zaidi na tutazidi kutoa huduma bora kwa wateja wetu, jamii,wabia wetu na kuwajali zaidi wafanyakazi wetu ili kukuza zaidi biashara yetu” aaliongeza Makanjee.


  0 0

   Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Azania ya jijini Dar-es-Salaam akizima moto kwa kutumia kizimia moto cha aina ya dry powder baada ya kupewa mafunzo ya kukabiliana na majanga ya moto kutoka Jeshi la Zimamoto na Ukoaji mkoa wa Ilala.
   Wanafunzi wa shule ya Secondari Azania ya jijini Dar-es-Salaam wakizimamoto kwa kutumia blanketi ya kuzimia moto baada ya kupewa mafunzo ya kukabiliana na majanga ya moto kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Ilala.

  ‘’Tayari tumeuzima’’ walisikika wanafunzi wa shule ya Sekondari Azania jijini Dar-es-Salaam baada ya kufanikiwa kuuzima moto kwa kuufunika kwa kutumia blanketi maalumu, huku wakishangiliwa mafunzo hayo utolewa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini bila malipo yoyote. 
  (Picha na FC Godfrey Peter).


  0 0

  Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Unicef  Dkt Jama Gulaid akitoa hotuba katika sherehe ya makabidhiano ya magari ya kubebea  wagonjwa Mkoa wa Mbeya15 Octobar  2015
  Mratibu wa Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto Ndugu Prisca Butuyuyu akitoa taarifa ya huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto katika Mkoa wa Mbeya kwenye hafla fupi ya makabidhiano ya magari ya kubebea wagonjwa 15 Octobar 2015.
  Meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi shirika la UNICEF. 
  SHIRIKA la Umoja wa Mataifa  linalo shughulikia watoto Duniani (UNICEF) limekabidhi msaada wa magari kumi  ya Kubebea wagonjwa yenye tahamni ya shilingi mil 700.7  kwa serikali ya Mkoa wa Mbeya .


  Aidha shirika hilo lina mpango wa kuboresha vituo 184 vya kutolea huduma za afya katika mkoa huo wa mbeya ambavyo ni vituo afya na hospital 30 pamoja na zahanati 154  sanjali na kuvipatia vifaa muhimu vya kutolea mafunzo kwa watumishi wake.


  Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Octobar 15 mwaka huu  Mwakilishi wa shirika la  UNICEF   nchini Tanzania Dkt Jama Gulaid  amesema shirika hilo limetenga kiasi cha shilingi bilioni 2 kwa ajili ya mradi huo.


  Amesema mchango wa UNICEF katika sekta afya na lishe hapa mkoani mbeya imepanua wigo kutoka halmashauri mbili za mkoa huo hadi kufikia halmashauri zote katika kipindi cha miaka miwili .


  Aidha Dtk, Jama amesema katika kukabiliana na magonjwa na vifo vya watoto na wanawake wajawazito ,UNICEF imechangia vifaa tiba muhimu ikiwa ni pamoja vile vya uchunguzi wa ujauzito ,upasuaji  sanjali na vifaa kuwasaidia watoto wachanga kupumua mara wanapo zaliwa na vifaa vingine vya utoaji wa huduma katika idara ya uangalizi maalumu  ICU.


  Aidha  amewataka viongozi hao wa mkoa wa Mbeya kuhakikisha wanaweka juhudi kubwa zaidi katika kupunguza vifo vya akina mama na watoto wachanga kwa kuhakikisha kwamaba kina mama wajawazito wote wanapata huduma za afya bure kwa wakati.


  Awali akisoma  taarifa ya huduma za afya ya uzazi na mtoto katika mkoa mbeya mratibu wa huduma za afya ya uzazi na mtoto Ndugu Prisca  Butuyuyu amesema toka shirika hilo la UNICEF  lianze kufanya mwaka 2012 huduma za afya zimeimalika kwa kiasi kikubwa hususani kwa kuweza kuzuia vifo vya uzazi na vya watoto wachanga.


  Amesema kwa ujumla hali ya vifo hususani vilivyokuwa  vinatokea katika vituo vya huduma vimepungua kutoka 140  kwa mwaka 2012 na kufikia vifo 94 kwa kwa mwaka 2014 pamoja na kupunguza vifo vya watoto wachanga kutoka 602 kwa mwaka 2012 hadi kufikia 568  mwaka 2014 ambapo punguzo hilo ni sawa na asilimia 33.9 na 5.7 kwa watoto wachanga.


  Akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Kaimu katibu Tawala Ndugu Kastro Msigala amelishukuru shirika hilo kwa msaada wa magari hayo sanjali na kutoa wito kwa viongozi  wa halmashauri ambao ni wakurugenzi na waganga wakuu kuhakikisha wanayatunza magari hayo ili yaweze kutoa huduma stahiki kwa wananchi.


  Msaada huo wa magari imegawanywa katika halmashauri zote mkoa huo wa mbeya ambazo ni Ileje,Mbozi,Mbeya vijijini,Rungwe,Busokelo,Mbarali pamoja na Kyela na Momba.

  0 0
 • 10/16/15--03:43: BEI YA MADAFU HII LEO


 • 0 0  IFC, a member of the World Bank Group, this week launched a $5 million program to increase access to energy in Tanzania by developing a market for mini-grids. The initiative aims to bring affordable, off-grid renewable energy to households and businesses in rural Tanzania. 

  IFC will work with project developers in Tanzania to promote commercially viable mini-grid business models, and will advise banks and financial institutions on how to extend long term finance to mini-grid developers.

  Tanzania has been selected as one of the first countries to test the concept of using small-scale renewable energy production sources under a new program, called the Scaling-up Renewable Energy in Low Income Countries Program. In Tanzania, it aims to help diversify energy production away from fossil fuel based sources.

  Mini-grids are technically and commercially viable for high-density populations that live outside the reach of the national electricity grid. The Tanzanian government estimates that about half of the country’s rural population could be served by off-grid options in a cost-effective manner. Mini-grids could provide access to electricity for 9.1 million people in Tanzania. 

  Lutengano Mwakahesya, Director General of Tanzania’s Rural Energy Agency said, “We have an urgent task ahead of us to increase energy access in Tanzania. Mini-grids are a key part of the solution, so this program with IFC is an essential step to improve the quality of life of households, demonstrating the role of the private sector.” 

  Tanzania’s Ministry of Energy and Minerals was closely involved in developing the mini grids program, and was represented at the event by the Assistant Commissioner, Mr. Edward Ishengoma. 

  Dan Kasirye, IFC’s Resident Representative for Tanzania, said “IFC aims to help develop a robust mini-grid market in Tanzania, which will create investment opportunities in the renewables sector and help fill the country’s energy gap. We plan to mobilize the financial resources and expertise of the private sector to expand energy services to low-income communities.”

  IFC, a leader in renewable energy finance, helps developing countries transition to a low carbon future. Over the past three years, IFC has financed close to $3.5 billion in renewable energy projects worldwide, including biomass, geothermal, hydro, solar, and wind.

  About IFC
  IFC, a member of the World Bank Group, is the largest global development institution focused on the private sector in emerging markets. Working with more than 2,000 businesses worldwide, we use our capital, expertise, and influence, to create opportunity where it’s needed most. In FY15, our long-term investments in developing countries rose to nearly $18 billion, helping the private sector play an essential role in the global effort to end extreme poverty and boost shared prosperity.

  0 0

   Mkurugenzi  wa Mipango na Maendeleo ya Biashara, Mhandisi Kato Kabaka (aliyesimama), kutoka Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania akitoa elimu kwa wananchi wa kata ya Kisaki wilaya ya Morogoro Vijijini namna ya kutafiti nishati ya Jotoardhi hadi hatua ya kuzalisha umeme na jinsi itakavyoweza kubadili maisha ya wananchi wa kata hiyo.
  Wananchi wa kata ya Kisaki, Morogoro Vijijini wakimsikiliza kwa makini Bi. Eva Nyantori, Afisa Sayansi ya Jamii kutoka Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania alipokuwa akiwaelimisha juu ya fursa ambazo watazipata kupitia mradi wa Jotoardhi.

  (Picha Na: Lilian Lundo – Maelezo)


  0 0

  The former president Hon. Ally Hassan Mwinyi giving the medal to the winner of the Marathon on mens side, Emmanuel Ginmiki during  Rotary Dar Marathon which took place in Dar es salaam on the Nyerere Day. Rotary Dar Marathon is taking place every year being organised by the Rotary Clubs in partnership with Bank M.Looking on is the Bank M's Deputy CEO Ms. Jacqueline Woiso and The Rotary District Governor Mr. Robert Waggwa Nsibirwa.
   The former president Hon. Ally Hassan Mwinyi flagging off the Rotary Dar Marathon 2015 which took place in Dar es salaam during Nyerere Day, right is the Bank M’s Deputy CEO Ms. Jacqueline Woiso (With the flag). Rotary Dar Marathon is taking place every year being organised by the Rotary Clubs in partnership with Bank M.
  Winners of the Rotary Dar Marathon 2015 on men’s runners side, Emmanuel Ginmiki (Winner), Ismail Juma (2ndplace) and Joseph Toefil (3rd Place) posing for a photo after receiving their prizes which were handed over by the former Tanzanian president Hon. Ally Hassan Mwinyi (standing in the middle).Others from right are Ms. Agnes Batengas, The Rotary Dar Marathon committee chair, Ms. Sharmila Bhatt, rotary Board chair, Mr. Robert Waggwa Nsibirwa, The Rotary District Governor, Ms. Jacqueline Woiso, Deputy CEO Bank M and Vikash Shah, The Rotary Dar Marathon 2015 committee member.

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi kutoka China (ZHEJING UNIVESITY  OF MEDIA&COMMUNICATIONS) Rrof.Dk.Peng Shaojian wakati alipofika Ikulu mjini Zanzibar akiwa na ujumbe aliofuatana nao leo.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Ujumbe kutoka nchini China katika Chuo cha (ZHEJING UNIVESITY  OF MEDIA&COMMUNICATIONS) chini ya kiongozi wake Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi  Rrof.Dk.Peng Shaojian (katikati) wakati alipofika Ikulu mjini Zanzibar akiwa na ujumbe aliofuatana nao leo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na mgeni wake Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi  Rrof.Dk.Peng Shaojian kutoka Chuo cha (ZHEJING UNIVESITY  OF MEDIA&COMMUNICATIONS) nchini China baada ya mazungumzo na Ujumbe  aliofuatana nao walipofika  Ikulu mjini Zanzibar leo,[Picha na Ikulu.]

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, Waziri wa Mawasiliano wa Vietnam,Nguyen Bac Son, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mtandao mpya wa simu za Halotel Tanzania, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, jana usiku Okt 15, 2015.
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (katikati) akiwaongoza viongozi wenzake kupiga ngoma kama ishara ya uzinduzi rasmi wa Mtandao mpya wa mawasiliano wa Halotel Tanzania, wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, jana usiku Okt 15, 2015. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (katikati) akigonganisha glasi na baadhi ya viongozi wa Vietnam kama ishara ya furaha baada ya uzinduzi rasmi wa Mtandao mpya wa mawasiliano wa Halotel Tanzania, wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, jana usiku Okt 15, 2015.

  0 0
 • 10/16/15--05:00: Maisha ni Siasa

 • 0 0

   


  Mbunge wa Ludewa Mhe Deogratias Haule Filikunjombe (chini) amefariki dunia katia ajali ya Chopa katika hifadhi ya wanyama ya Selous, pamoja na rubani Kepteni William Silaa (juu kulia), mfanyakazi wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa na ndugu yake Marehemu Filikunjombe ambao majina  hayajapatikana mara moja.
  Mhe. Deo Filikunjombe, rubani na  na abiria wengine walipata matatizo ya engine ya chopa namba  5Y-DKK jana jioni wakitokea Dar kuelekea Ludewa.

  Kwa mujibu wa Meya wa Ilala aliyemaliza muda wake Mhe Jerry Silaa, ambaye ni mtoto wa rubani, hakuna mtu aliyenusurika katika ajali hiyo ya Chopa. 
  "Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa rasmi kutoka kwa timu ya uokoaji kuwa imefanikiwa kufika eneo la ajali na kukuta abiria wote na rubani wamepoteza maisha.
  "Ni mepoteza Baba na rubani mzuri wa nchi yetu Capt. William Silaa. Nimepoteza rafiki na kiongozi wangu Mhe. Deo Filikunjombe. Nawapa pole wote waliopoteza ndugu zao. Nawaombea marehemu mapumziko ya Amani. Nawashukuru wote walioshirikiana na familia kusaidia uokozi", amesema Mhe Jerry Silaa katika kurasa zake za mitandaoni.
  tangia jana habari za kuanguka kwa nchopa hiyo zilitapakaa kila kona na katika mitandao, na kuendelea hadi leo tangia asubuhi hadi baada ya ujumbe wa Jerry Silaa kupatikana mchana huu.


  0 0


  0 0

  Pichani Kulia ni Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akimnadi aliyekuwa Mgombea Ubunge wa jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe (enzi za uhai wake),wakati Dkt Mgufuli alipopita kwenye jimbo hilo wakati wa kampeni
   
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amepokea kwa mshtuko na huzuni nyingi taarifa za vifo vya Mbunge wa Jimbo la Ludewa, mkoani Njombe Ndugu Deo Filikunjombe Haule, Kepteni William Silaa pamoja na abiria wengine wawili ambao wameaga dunia jana, Alhamisi, Oktoba 15, 2015 kwa ajali ya helkopta iliyotokea katika eneo la Hifadhi ya Selous mkoani Morogoro.

  Katika salamu za rambirambi ambazo amewatumia Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Ndugu Deo Sanga, na Meya wa Manispaa ya Ilala Mstahiki Jerry Silaa, Dkt. Magufuli amesema: “Kwa hakika, nimeshtushwa na kuhuzunishwa mno na taarifa za vifo vya Ndugu Filikunjombe na Ndugu Silaa ambavyo nimetaarifiwa kuwa vimetokea kwa ajali ya helkopta aliyokuwa akiitumia Ndugu Filikunjombe kwa Kampeni zake za Ubunge katika jimbo hilo la Ludewa.

  Katika salamu zake hizo za rambirambi Dkt. Magufuli ameongeza kuwa: “Kama unavyojua, namfahamu vizuri Ndugu Filikunjombe. Alikuwa Mbunge mwenzangu katika Bunge lililomaliza muda wake mwaka huu. Nimefanya kazi naye  kwa karibu na kwa miaka mitano ndani ya bunge letu. 

  Alikuwa mtumishi hodari, mtumishi mwaminifu na mwadilifu kwa wananchi wa Tanzania, na hasa wananchi wa Jimbo la Ludewa, ambao aliwawakilisha kwa miaka mitano iliyopita akiwa Mbunge wao. Hata nilipofanya ziara ya kampeni katika jimbo lake la Ludewa mwezi uliopita nililala nyumbani kwake, hiyo inaonesha nilivyokuwa karibu naye. Tutakosa utumishi wake mahiri sana.”

  Salamu zake za rambirambi  kwa Mstahiki Meya Jerry Silaa, Dkt. Magufuli amesema: “Nimesikitishwa sana na taarifa ya kifo cha Baba yako Kepteni William Silaa, kwani ni tukio lisilozoeleka. Ni jana tu nimeshiriki nawe katika kampeni kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa 2015 katika jimbo unalogombea Ubunge, jimbo la Ukonga, naungana nawe katika kipindi hiki kigumu cha msiba mkubwa. Nakupa pole wewe binafsi, familia yenu, ndugu, jamaa na marafiki wote”.

  Aidha aliongeza “Nakutumia wewe Ndugu Sanga, Mwenyekiti wetu wa CCM mkoa wa Njombe salamu za rambirambi za dhati ya moyo wangu kuomboleza kifo cha Ndugu Filikunjombe na abiria hao wengine. Aidha, kupitia kwako namtumia rambirambi nyingi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Anna Semamba Makinda na Wabunge wote kwa kuondokewa na mwenzao.”

  Dkt. Magufuli ameongeza “Nakuomba pia unifikishe salamu zangu za rambirambi kwa wananchi wa Jimbo na Wilaya ya Ludewa ambao wamepoteza Mbunge wao aliyewatumikia kwa ustadi mkubwa kwa kipindi chote. Aliwawakilisha vizuri na kujali sana maslahi yao. “Ametuma pia salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa Ndugu Filikunjombe kwa kuondokewa na mhimili wa familia na rafiki yao mpenzi.

  Amewaombea kwa Mwenyezi Mungu awape subira na nguvu ya uvumilivu katika kipindi hiki kigumu na cha majonzi. Pia naungana nao kumwomba Mwenyezi Mungu aziweke pema peponi roho ya Deo Filikunjombe Haule”. Amen.


  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano
  CCM Ofisi Ndogo, Lumumba
  DAR ES SALAAM.
  16 Oktoba, 2015

  0 0


  0 0

  Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Mohamed Shein akimnadi Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli mbele ya maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja,kisiwani Unguja jioni ya leo.

  Dkt Shein emebainisha wazi kwenye mkutano huo wa kampeni kuwa Dkt Magufuli ni mtu sahihi na anatosha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,amesema kuwa iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano atashirikiana nae kwa kila jambo kuhakikisha Tanzania inapiga hatua zaidi kimaendeleo.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja,kisiwani Unguja jioni ya leo.
  Sehemu ya umati wa wakazi wa Kisiwani Unguja na vitongoji vyake wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja mjini humo,ambapo Mgombea Urasi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufui aliwahutubia.
  Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Mohamed Shein akimsikiliza kwa makini Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli kabla ya kupanda jukwaani na kuwahutubia maelfu ya wakazi wa kisiwani Unguja kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja,kisiwani humo.
  Wananchi wa kiswani Unguja wakishangilia jambo kwenye mkutano huo wa kampeni.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja,kisiwani Unguja jioni ya leo.
  Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Mh Al Hassan Mwinyi  akiwahutubia Wananchi (hawapo pichani) ,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja,kisiwani Unguja jioni ya leo.  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini,Ndugu Boraafya Silima akizungumza machache kwenye mkutano wa kampeni kabla ya kumkaribisha Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kuwahutubia wananchi wa kisiwani Unguja.
  Nyomi la wakazi wa Kisiwani Unguja ndani ya mkutano wa kampeni.
  Sehemu ya umati wa wakazi wa kisiwani Unguja na vitongoji vyake wakiwa  wamekusanyika kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja,kisiwani Unguja jioni ya leo.

  PICHA NA MICHUZI JR-KISIWANI UNGUJA

  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Familia ya Michael na Teddy pamoja na Mngodo wote, tunapenda kuwakaribisha ndugu, jamaa na marafiki zetu kwenye ibada maalumu ya shukurani, na kusherehekea maisha ya Marehemu Baba yetu Mzee GODFREY MBIU MNGODO, (pichani) itakayofanyika siku ya Jumamosi 10/31/2015 kuanzia saa kumi jioni hadi saa tatu usiku ..

  Mahali ni:
  35 E.STANTON AVE, 
  COLUMBUS OH 43214. 

  Karibuni sana na Mungu awabariki.

  Kwa maelezo zaidi na maelekezo
  Michael Godfrey Mngodo: 614 446 5565. Teresia Teddy Ngeleja Mngodo: 614 772 1591. Kwetukia Joseph Mngodo: 614 316 5092   Vickie Tungaraza: 614 288 8103

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kulia) akizungumza na uongozi na watendaji wa Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma alipofanya ziara wilayani humo kwa ajili ya kukagua Kambi ya Nduta wilayani humo pamoja na Kambi za Mtendeli na Karago wilayani Kakonko ambazo zipo katika maandalizi ya kuwapokea wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa kwa muda katika Kambi ya Nyarugusu mkaoni humo. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Ruth Msafiri.
  Mhandisi wa Maji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Msafiri Mtyaule akitoa maelezo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (wa pili kulia) kuhusu kisima ambacho kitasambaza maji kwa ajili ya wakimbizi kutoka Burundi ambao watahifadhiwa katika Kambi ya Mtendeli wakitokea Kambi ya Nyarugusu ambapo wanahifadhiwa kwa muda.
  Mkuu wa Kambi ya Wakimbizi ya Nduta, Fred Nisajile akimuonyesha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (wa pili kulia) moja wapo ya madarasa yatakayotumiwa na wakimbizi watakaohamishiwa katika Kambi ya Karago kutoka Kambi ya Nyarugusu wanapohifadhiwa kwa muda. Ubaoni ni picha na maandishi yaliyoachwa na wakimbizi walioishi katika kambi hiyo kabla ya kufungwa mwaka 2007.

  Baadhi ya Wakimbizi kutoka Burundi wakipokelewa katika Kambi ya Wakimbizi ya Nduta. Idadi ya wakimbizi kutoka nchini humo inazidi kuongezeka siku hadi siku.
  Askari Polisi wanaosimamia usalama katika Kambi ya Wakimbizi ya Nduta wakikagua mizigo ya wakimbizi kutoka Burundi wanaopokelewa katika kambi hiyo ili kuhakikisha usalama wa mizigo yao.
  Watoto wa Wakimbizi kutoka Burundi wakiwa katika Kambi ya Wakimbizi ya Nduta ambapo wanahifadhiwa.
  Baadhi ya mahema yanayojengwa katika Kambi ya Wakimbizi ya Nduta wilayani Kibondo mkoani Kigoma ambayo yatatumika kuwahifadhi wakimbizi kutoka Burundi wanaoendelea kuwahamishiwa kambini hapo kutoka Kambi ya Nyarugusu ambapo walikuwa wamehifadhiwa kwa muda.  
  Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

   Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Azania ya jijini Dar-es-Salaam akizima moto kwa kutumia kizimia moto cha aina ya dry powder baada ya kupewa mafunzo ya kukabiliana na majanga ya moto kutoka Jeshi la Zimamoto na Ukoaji mkoa wa Ilala.

   Wanafunzi wa shule ya Secondari Azania ya jijini Dar-es-Salaam wakizimamoto kwa kutumia blanketi ya kuzimia moto baada ya kupewa mafunzo ya kukabiliana na majanga ya moto kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Ilala jana tarehe 15 Oct, 15.

  ‘’Tayari tumeuzima’’ walisikika wanafunzi wa shule ya Sekondari Azania jijini Dar-es-Salaam baada ya kufanikiwa kuuzima moto kwa kuufunika kwa kutumia blanketi maalumu, huku wakishangiliwa mafunzo hayo utolewa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini bila malipo yoyote. (Picha na FC Godfrey Peter).


  0 0

  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura akizungumza katika hafla fupi iliyowakutanisha baadhi ya wateja wa kampuni hiyo na maofisa wa TTCL kubadilishana uzoefu na kupata maoni ya wateja wao jana jijini Dar es Salaam Double Tree by Hilton Hotel. Tukio hili ni mwendelezo wa Wiki ya Huduma kwa wateja wa Kampuni ya simu ya TTCL iliyozinduliwa hivi karibuni.
  Baadhi ya wateja, wafanyakazi wa TTCL wakibadilishana mawazo kwenye  hafla fupi iliyowakutanisha baadhi ya wateja wa kampuni hiyo na maofisa wa TTCL kupata maoni juu ya huduma wanazopatiwa na kampuni hiyo.
  Baadhi ya wateja, wafanyakazi wa TTCL wakibadilishana mawazo kwenye  hafla fupi iliyowakutanisha baadhi ya wateja wa kampuni hiyo na maofisa wa TTCL kupata maoni juu ya huduma wanazopatiwa na kampuni hiyo.
  Baadhi ya wateja, wafanyakazi wa TTCL wakibadilishana mawazo kwenye  hafla fupi iliyowakutanisha baadhi ya wateja wa kampuni hiyo na maofisa wa TTCL kupata maoni juu ya huduma wanazopatiwa na kampuni hiyo.
  Meneja wa Kitengo cha Habari na Mausiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Thomas Mushi akizungumza kwenye hafla hiyo iliyokutanisha baadhi ya wateja na maofisa wa TTCL kubadilishana uzoefu jana jijini Dar es Salaam Double Tree by Hilton Hotel.
  Mmoja wa wateja wa TTCL akitoa maoni yake juu ya huduma zinazotolewa na kampuni hiyo kwa wateja wake.
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kulia) akigonganisha glasi ya mvinyo na baadhi ya wageni waalikwa kwenye hafla fupi ya baadhi ya wateja wa kampuni hiyo na maofisa wa TTCL kubadilishana uzoefu na kupata maoni ya wateja wao jana jijini Dar es Salaam.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

  Jana Ijumaa ya Octoba 16,2015 Baraza Kuu la Waislamu Mkoa wa Mwanza liliungana na Waislamu wengine kuadhimisha mwaka mpya wa Kiislamu ambao ni 1437. 
  Kwa kalenda ya Kiislamu sherehe hizo zilifanyika jana tarehe mbili, mwezi Muharamu mwaka wa 1437 (02.01.1437) ikiwa maadhimisho yanayoambatana na kumbukumbu ya Kuhama kwa Mtume Muhammad kutoka Mji wa Macca kwenda Madina.

  Katika kuadhimisha sherehe hizo, Baraza hilo kupitia kwa Katibu wake Mkoani Mwanza Sheikh Mohamed Balla (Kulia Pichani) alitoa tamko kwa niaba ya Waislamu wote Mkoani Mwanza kutokana na kauli inayoelezwa kutolewa na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima kwamba ana ndoto ya Misikiti yote nchini kugezwa kuwa Sunday School na Masheikh watakwenda kuangukia katika misalaba. 

  Alisema kauli za namna hiyo si njema kwa mstakabali wa Taifa ambapo alisema kuwa Waislamu wote Mkoani Mwanza wanalaani na kukemea kauli hiyo na nyingine zote za aina hiyo na wale wanaozitoa.

  Aliwataka Watanzania kuungana kwa pamoja hususani katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu na kwamba Wamchague kiongozi muadilifu, Mchapakazi na anaechukia rushwa ambae ataendelea kuwaunganisha watanania wote. 
  Imam wa Msikiti Khadija Jijini Mwanza Mohammed Awadhi akisoma Ibada ya Quran katika Sherehe za Mwaka mpya wa Kiislamu ulioadhimishwa jana katika Uwanja wa Mbugani Jijini Mwanza na kuambatana na ibada mbalimbali ikiwemo kuliombea taifa amani.

  Sheikh Mahamood Khasan akisoma ibada ya kuliombea taifa amani katika Sherehe za Mwaka mpya wa Kiislamu ulioadhimishwa jana katika Uwanja wa Mbugani Jijini Mwanza na kuambatana na ibada mbalimbali ikiwemo kuliombea taifa amani.

older | 1 | .... | 1000 | 1001 | (Page 1002) | 1003 | 1004 | .... | 3284 | newer