Quantcast
Viewing latest article 13
Browse Latest Browse All 118179

Vodacom Wadhamini Wakuu Matembezi ya TWENDE BUTIAMA 2025.

 

Na Jane Edward, Arusha 

Vijana wa baiskeli wenye kampeni ya TWENDE BUTIAMA wakishirikiana na Kampuni ya Mtandao wa simu ya Vodacom imeanza mchakato rasmi wa maandalizi kuelekea Butiama ikiwa ni muendelezo wa kumuenzi Baba wa Taifa Mwl Julias Kambarage Nyerere.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti vijana hao wakiongozwa na mwenyekiti wa zoezi hilo Gabriel Landa amesema wameamua kwa mwaka huu kuanza matembezi hayo mapema ili kupisha uchaguzi mkuu ambao utafanyika mwishoni mwa mwaka huu wa 2025.


Aidha Kwa kutumia baiskeli zao, vijana kutoka mikoa mbalimbali wanapita vijiji na miji, wakibeba ujumbe mmoja muhimu wa uzalendo wa kweli bado upo, na unaishi ndani ya kizazi kipya.

"Twende Butiama si tu kumbukumbu ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere. Ni mwamko Ni sauti ya mshikamano, afya ya jamii, na maendeleo ya vijana kupitia michezo na usafiri"Alisema


Amesema Katika kila mtaa wanaopita, vijana hawa wanakutana na wenzao wanabadilishana mawazo, wanahamasishana,juu ya yote, wanakumbusha umuhimu wa kuenzi historia na misingi ya taifa.

Zuweina Farah ni Mkurugenzi wa Vodacom Foundation ambapo Kampeni hii imepata sapoti kubwa kutoka sekta binafsi, huku Vodacom Tanzania ikiongoza kama mdhamini mkuu kwa awamu tatu.


Amesema kuwa kwa sasa matembezi hayo yataanzia rasmi Mkoa wa Arusha tofauti na kipindi cha nyuma ambapo matembezi hayo hufanyika katika mikoa mingine.

"Tunaowadau wengine ambao wameshirikiana na sisi na kwamba ipo misaada itakayotolewa ikiwemo baiskeli kwa watoto wenye uhitaji ili kupamba matembezi hayo kuelekea makazi ya hayati Baba wa Taifa Mwl Julias Kambarage Nyerere "alisema

Kadri safari inavyoendelea, na kila kilomita inapopungua, ujumbe wa Twende Butiama unazidi kugusa mioyo ya Watanzania.






Viewing latest article 13
Browse Latest Browse All 118179

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>