Na Mariam Mkamba, Tabora
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, amewataka Watanzania kuendelea kuiheshimu amani ya nchi kwani urithi wa kizazi hadi kizazi, huku akisisitiza kuwa wale wanaochochea uvunjifu wa amani iliyopo hawajui wanachokifanya.
Akizungumza wilayani Urambo mkoani Tabora ambako anaendelea na ziara yake ya kikazi ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu 2020-2025 , Wasira amesema baada ya uhuru, Tanzania imeendelea kuwa yenye amani na utulivu na amani hiyo inqpaswa kulindwa na kila mmoja Wetu.
Pia amesema kuwa tangu CCM imekuwa madarakani imefanya mambo mengi ya maendeleo na katika kipindi cha miaka 60 ya uhuru Watanzania maisha yao yameendelea kuwa bora zaidi ukilinganisha na miaka 70 ambayo Wakoloni walikuwa wametawala.
“Tumefanya maendeleo makubwa sana katika nchi yetu,maisha ya wananchi yamekuwa bora zaidi na kazi hiyo inaendelea maana maendeleo hayana mwisho.Wapo wanaosema hatujafanya chochote hao wanaosema hivyo tuwasamehe maana hawajui chochote.Nawaombeq msamaha.”
Kuhusu Ujenzi wa miundombinu ya huduma mbalimbali ,Wasira amesema kuwa chini ya uongozi wa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kuna kazi kubwa imefanya katika sekta mbalimbali.
Aidha, aligusia mafanikio katika sekta ya afya kwa kueleza kuwa enzi za nyuma wazazi walizaa kwa tabu kutokana na ukosefu wa vituo vya afya na huduma bora za matibabu tofauti na sasa ambapo huduma hizo zimeimarishwa na vifo vya watoto vimepungua kwa kiasi kikubwa.
Wasira pia alieleza Serikali ya CCM imeendelea kuboresha miundombinu nchini ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), daraja la Urambo linalotarajiwa kuanza kazi hivi karibuni pamoja na maboresho ya sekta za elimu na afya.
“Sera za CCM ni kazi iendelee kama kauli mbiu ya Mwenyekiti wetu, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Tunaona matokeo yake katika kila kona ya nchi,” amesema.
Kuhusu wakulima wa tumbaku mkoani Tabora Wasira aliwahakikishia wananchi kuwa atazungumza na wahusika kuhakikisha malipo yao yanapatikana haraka ili kuwaondolea kero zinazowakabili.
Image may be NSFW.
Clik here to view.

.jpeg)
Image may be NSFW.
Clik here to view.
.jpeg)
Image may be NSFW.
Clik here to view.

Clik here to view.

Image may be NSFW.
Clik here to view.
.jpeg)
Image may be NSFW.
Clik here to view.