Hapa ni Msasani Kwa Warioba katika barabara ya Old Bagamoyo Road ambayo kuanzia kesho itaitwa Barabara ya Mwai Kibaki Road kwa heshima aliyotunukiwa kiongozi huyo wa Kenya na Hlmashauri ya Wilaya ya Kinondoni kufuatia ziara yake ya kitaifa ya siku mbili itayoanza kesho jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadik, barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 10.1 ni kuaniza kwenye mataa ya Moroccco karibu na makao makuu ya Airtel hadi mzunguko wa kuelekea Africana kule Mbezi Beach, mkabara na uwanja wa kulenga shabaha wa JWTZ.
Akiongea usiku huu, Mkuu huyo wa Mkoa amesema Rais Kibaki anatarajiwa kuwasili kesho saa 9 alasiri na kupkewa na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ambapo usiku atamwandalia dhifa ya kitaifa Ikulu. Keshokutwa. Alhamisi, Rais Kibaki ataongea na wazee wa Dar es salaam katika ukumbi wa PTA ulioko viwanja vya SabaSaba barabara ya Kilwa Road. Pia atatembelea sehemu mbalimbali atazopangiwa katika ziara yake hiyo ambayo pia ataitumia kuwaaga Watanzania kwani muhula wake wa uongozi utafikia kikomo baadaye mwaka huu.