Mheshimiwa Mathias Chikawe (Mb), Waziri wa Katiba na Sheria leo amekutana na viongozi mbalimbali kwa nyakati tofauti na kufanya nao mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ambayo Wizara ya Katiba na Sheria inashughulika nao.
Mheshimiwa Chikawe pia amefanya mazungumzo na Balozi wa Denmark hapa Nchini Bw Johnny Flentoe ambaye alimtembelea Waziri Ofisini kwake. Katika mazungumzo yao wameongelea ziara wa Waziri Mkuu wa Denmark itakayofanyika hivi karibuni na kuongelea mahusiano ya Denmark na Serikali katika nyanja mbalimbali. Mhe Chikawe aliishukuru Serikali ya Kifalme ya Denmark kwa kuwa mdau Mkubwa wa Sekta ya Sheria Nchini na kwa misaada yao kupitia Shirika lake la Maendeleo ya Kimataifa la DANIDA katika Programu ya Maboresho ya Sekta ya Sheria Nchini. Misaada yao imefanikisha kuboresha miundombinu ya taasisi za kisheria na kujenga mifumo imara ya sheria na kupanua wigo wa fursa za wananchi kupata haki.
Mhe. Chikawe akiwa kwenye picha ya pamoja na Lord Dholakia (kushoto) na Bw Julian Chandler (Naibu Balozi wa Uingereza Nchini) mara baada ya kufanya mazungumzo ofisini kwa Waziri
Mheshimiwa Chikawe amefanya mazungumzo na Lord Navnit Dholakia ambaye ni Naibu Kiongozi wa chama cha Liberal Democrats cha Uingereza na mjumbe wa All Party Parliamentary Group ambalo linajihusisha na kufutwa kwa adhabu ya kifo. Lord Dholakia yuko nchini kwa ziara ya kikazi na moja ya mambo aliyozungumza na Mhe. Chikawe ni mustakabali wa adhabu ya kifo Nchini na kushauri kuwa wakati umefika kwa Serikali ya Tanzania kuangalia umuhimu wa kuwepo au kutowepo kwa adhabu ya kifo na ameshauri uwezekano wa adhabu hiyo kufutwa. Kwa upande wake pamoja na mambo mengine Mhe Chikawe amemuhakikishaia Lord Dholakia kuwa kupitia
Mhe Chikawe akiwa kwenye mazungumzo na Bw. Bongani Majola ambaye ni Msajili wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari (ICTR
Waziri Chikawe pia amefanya mazungumzo na Msajili wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) Bw. Bongani Majola ambaye alimtembelea Ofisini kwake leo, lengo likiwa ni kujitambulisha na na kuongelea shughuli mbalimbali za Mahakama, mafanikio na changamoto za Mahakama hiyo. Mhe Chikawe amemuhakikishia Msajili huyo kuwa Tanzania itaendeleza ushirikiano wake na Mahakama hiyo na kumuomba wawe tayari kusaidia pale ambapo sekta ya sheria itaona inahitaji msaada. Picha na Charles Joseph Mmbando