Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala Za Mikoa na Serikali za Mitaa Aggrey Mwanri akihutubia hafla ya uzinduzi wa mfumo mpya wa menejimenti ya taarifa za bima kwa ajili ya Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa (CHF Iliyoboreshwa) mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja wa Mradi wa HSPP Madfred Stroemer watekelezaji wa mfumo huo mpya kwa ufadhili mkuu wa Serikali ya Uswisi na Vodacom(katika mawasiliano).
Naibu Waziri Mwanri akipokea kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi kadi ya uanachama wa mfuko wa Afya ya Jamii Ulioboreshwa - CHF muda mfupi baada ya kuzindua mfumo mpya wa nmenejimenti ya taarifa za bima kwa ajili ya mfuko huo utakaowezesha uandikishaji, ukusanyaji na uwasilihaji madai ya malipo kwa wato huduma na ufuatiliaji wa taarifa za wanachama kwa njia rahisi ya kielekrtoniki kutumia mtandao wa Vodacom mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.