Tunaukaribisha mwaka 2013 kwa kuwaletea ubao mpya wa malumbano ya hoja:
Filosofa Forum (http://www.filosofaforum.com/)
Katika fani hii ya mawasiliano, iwe kwa blog za jamii, barua pepe, magazeti, tovuti na aina nyingine nyingi, jambo moja ambalo baadhi yetu wadau wa malumbano ya hoja tungependa kuweka juhudi kulibadilisha katika mwaka huu mpya 2013, ni jukwaa la habari, mipasho (malumbano) ya kisiasa, kimichezo, na utani wa kikabila, wenye ustaarabu na maadili yaliyopevuka bila kudhihaki jinsia, dini, maumbile au kabila la mtanzania yeyote.
Awe mtoto, kijana, mzee, mvulana, msichana, mwanaume au mwanamke, Filosofa Forum inaamini sisi sote ni matokeo ya uumbaji wa mwenyezi mungu.
Hivyo basi kama unaamini kwa dhati kuwa huu ndo mwelekeo unaostahili katika malumbano ya hoja bila vioja, hapa ndio mahali muafaka ambapo mijadala ya aina zote itazingatia maadili , uwazi, na kuheshimu tofauti za kiitikadi, dini , na tamaduni zote za mtanzania.
KARIBUNI SANA UELIMIKE NA KUELIMISHA WENGINE
Happy New Year 2013
By Filosofa Forum team.