BARAZA la Sanaa la Taifa (Basata) limetoa kibali kwa ajili ya Tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika Machi 31 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana kuwa kutokana na kupata kibali hicho maandalizi rasmi sasa yameanza. “Nilikuwa Napata tabu hata kuanza kuhangaikia ukumbi ambao tutafanyia tamasha maana mwaka jana tulifanyia Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, sasa bado hatujaamua tutafanyia wapi kwa sababu ilikuwa hatuna kibali.
“Lakini hatua ya Basata kutupatia kibali inamaanisha tumepata baraka, hivyo tuendelee na mambo mengine ya maandalizi,” alisema Msama. Alisema wamepanga siku yenyewe ya Pasaka tamasha lifanyike Dar es Salaam na siku inayofuata bado wanaangalia wafanye wapi kwani mikoa mbalimbali imeomba ipewe uenyeji.
“Vipo vigezo tutaviangalia kwa wanaotaka tuwapelelekee, kama vitakuwa sawa basi tamasha litafanyika kwa watakaotimiza, lakini kwa sasa Jumatatu ya Pasaka bado hatujaamua wapi twende,” alisema Msama katika taarifa hiyo.
Tamasha la mwaka jana baadhi ya waimbaji mahiri waliokuwepo ni Rose Muhando, Rebecca Malope, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Atosha Kissava, Ephraim Sekeleti na kundi la Glorious Celebration.
Pia kwaya mahiri ya Kinondoni Revival, Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zilikuwa miongoni mwa burudani zilizokuwepo siku hiyo.
Pia kwaya mahiri ya Kinondoni Revival, Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zilikuwa miongoni mwa burudani zilizokuwepo siku hiyo.