Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Taarifa za kinatharia Kupitia Vyombo vya Habari

$
0
0

Kama jibu  kwa taarifa za kupotosha za hivi karibuni kutoka kwa vyombo vya habari, Bodi ya fastjet ingependa kuchukua fursa hii kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa zisizo za kweli na za kuchafua zilizotolewa na Don Smith wa fly540 Kenya.

Kampuni, kwa msisitizo mkubwa, inakataa madai yaliyotolewa na Don Smith kuhusu  wazo la ununuzi wa hisa ndani ya Fly540 Kenya pamoja na madai mengine mengi yaliyofanywa kupitia vyombo vya habari katika majuma ya hivi karibuni.

Akitoa kauli kuhusu madai ya hivi karibuni, mweyekiti wa fastjet David Lenigas alisema:

 “fastjet imenuia kufanya biashara zake katika hali ya uwazi, isiyofichika na ya kihalali kwa ujumla wake, kupitia itifaki zinazotakiwa. Kampuni hii haina nia ya kuendelea kukanusha madai ya uongo kupitia vyombo vya habari lakini itachukua hatua za kisheria kuhusu madai mengine zaidi kama hayo.”

“fastjet imemlipa Don Smith na wenzake zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 6 kwa ajili ya hisa zake kwenye  Fly540 na nembo nyingine za kibiashara zinazohusiana na hiyo, na sasa kwa ari kubwa itachukua hatua kuhakikisha kuwa mikataba yake imetekelezwa.”

“Kampuni haitavumilia mikakati yoyote ya ulaghai na isiyo ya wazi. Masuala yaliyotungwa na Don Smith nchini Kenya hayatadhuru mpango wa jumla wa fastjet wa kuwa kampuni ya kwanza ya safari za ndege kwa Afrika nzima yenye gharama za chini”

 “Nafasi ya kampuni nchini Kenya, ambayo ni  sehemu ndogo tu ya upanuaji wetu, imeshawekwa salama kupitia mkataba wa makubaliano na Jetlink uliotangazwa wiki iliyopita. Tunahisi kuwa Jetlink, ambayo tayari ina ithibati ya  IOSA, ni mshirika mzuri zaidi wa fastjet ukizingatia viwango vyetu vya usalama na uaminikaji. Baada ya kufanya mapitio ya kina, tulitambua kuwa Jetlink itaweza kuipa fastjet msingi wa kudumu wa kuanzia kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa miundombinu na ithibati yake ya kiwango cha kutoa huduma na kusimamia ndege nyingi kubwa za kisasa”
“Afrika ina karibu asilimia 4% ya abiria wa safari za anga duniani lakini kwa bahati mbaya kwa sasa ndiyo yenye asilimia 25% ya ajali za ndege duniani. Dhima yetu ya kuleta usafiri salama kwa watu wa Afrika inahitaji viwango vya juu na uzingatiaji wa kila mara kuhakikisha kuwa haya yanatekelezwa.”

Mkurugenzi mkuu wa fastjet Ed Winter aliongeza: 
 “Pale ambapo madeni ya kihistoria yaliyoendelea kuongezwa na Don Smith na Fly540 yamekuja kuwa wazi baada ya umiliki, fastjet inafanya kazi kwa karibu na wadai wake ili kufikia muafaka unaoridhisha kwa pande zote zinazohusika. Hatukubaliani na viwango vya gharama ambavyo vimekuwa vikitamkwa katika vyombo vya habari hivi karibuni, na pale viwango vinavyodaiwa vinapotambulika, msivichukulie kwa umakini kuhusiana na biashara kwa ujumla. Masuala haya yaliyojitenga hayadhuru utendaji wa siku hadi siku wa fastjet au utendaji wowote wetu katika Angola au Ghana ambao wanasafirisha chini ya nembo nyingine ya Afrika ya Fly540”

 “fastjet itachukua hatua kurejesha madeni haya ambayo hayawekwi wazi na mengine yoyote yaliyomo chini ya waranti zilizotolewa na Don Smith na wenzake katika makubaliano yao ya kuuza hisa zao ndani ya Fly 540 Kenya na kuiuzia fastjet mwezi Juni mwaka jana”

Timu ya menejimenti ya fastjet inabaki kuwa ya wanaharakati wakubwa wa maendeleo ya kampuni, kujenga mafanikio yake Tanzania na ukuaji kuelekea kuweka demokrasia katika usafiri wa anga wa Afrika na kuwa shirika la kwanza  la usafiri wa anga barani Africa lenye gharama za chini

 “Kwa sasa, tunaendelea kufanya kazi na mamlaka zinazohusika katika mataifa mengine Afrika kupanua mtandao wa fastjet”


kuhusu utata wa Leseni ya Nembo na takwimu BOFYA HAPA



Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>