Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115293

BALOZI WA TANZANIA NCHINI OMAN AANDAA HAFLA KUWAAGA WAJUMBE WA MKUTANO WA DIASPORA NCHINI OMAN

$
0
0
Mheshimiwa Ali Ahmed Saleh, Balozi wa Tanzania nchini Oman aliongoza Ubalozi wa Tanzania nchini Oman katika ya chakula alichoaandaa nyumbani kwake Shatti Al Qurum, mjini Muscat Oman kwa ajili ya kuwapongeza na kuwaaga wajumbe wa mkutano wa Diaspora uliofanyika mjini muscat kuanzia Alhamis tarehe 20 Disemba na kumalizika siku ya jumamosi tarehe 22 Disemba 2012 katika ukumbi wa Sindbad, Crowne Plaza Hotel Muscat.
 Katika hotuba yake ya kuwakaribisha wageni wake Mheshimiwa Balozi Ali Ahmed Saleh aliwapongeza wajumbe wote kutoka Tanzania kwa kazi nzuri waliyoifanya katika kukabili hoja na kero mbalimbali za wana diaspora, wafanya biashara na wawekezaji wa Oman kwa manufaa ya nchi ya Oman na Tanzania, michango yao na mahudhurio yao katika mkutano huu wa Diaspora ambao umefanyika kwa mafanikio makubwa.
 Pamoja na pongezi hizo Mheshimiwa Balozi Ali Saleh aliwasisitiza wajumbe hao kuendelea kufanya juhudi katika kufuatilia na kutekeleza yale yote yaliyokubaliwa katika vikao vya mikutano iliyofanyika. 
Aidha kwa upande Mheshimiwa Balozi aliwashukuru wana Diaspora kwa ushirikiano wao mkubwa na uvumilivu waliounyesha wakati wote wa mikutano hiyo. 
Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huu ulijumuisha wajumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi, Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu pamoja na taasisi kadhaa kutoka sekta ya umma na binafsi ikiwa ni pamoja Shirika la utangazaji Tanzania, Bodi ya Utalii, Benki yza CRDB, Azania Bank Corp, Bank of Africa, Benki ya Watu wa Zanzibar, Zanzibar Insurance, Zanzibar Social Security Fund, Zanzibar Chamber of Commerce, Tanzania Investment Centre, Zanzibar Investment Promotion Authority na Tanzania Private Sector Foundation, Dar Es Salaam Maritime Institute.
 Mheshimiwa Balozi Ali Saleh ( wa pili kutoka kushoto) akifunga kikao cha mwisho cha mkutano wa Diaspora nchini Oman . wa kwanza kushoto ni Mhe. Balozi, Bertha Somi, Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora, Wizara ya Mambo ya Nje
 Wajumbe wa mkutano
 Mheshimiwa Ali Ahmed Saleh, Balozi wa Tanzania nchini Oman ( aliesimamama ) akizungumza na ujumbe wa Tanzania na wana diaspora katika hafla ya chakula cha usiku

 Juu na chini ni Wajumbe wa mkutano wa Diaspora ya Oman wakimsikiliza Mheshimiwa Balozi wakati wa Sherehe ya kufunga mkutano


Viewing all articles
Browse latest Browse all 115293

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>