Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115013

kutoka bungeni dodoma leo

$
0
0
Mbunge wa kuteuliwa kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi, Bw. James Mbatia, aliwasilisha hoja binafsi bungeni mjini Dodoma iliyoainisha suala zima la udhaifu uliopo katika sekta ya elimu nchini. 

 Katika hoja hiyo, Bw. Mbatia alisema kukosekana kwa mitaala katika shule za msingi na sekondari, kunachangia wanafunzi kufanya vibaya. 

 Alisema hali hiyo inachangiwa na utendaji mbovu wa kitengo cha kuandaa mitaala hiyo ambacho kimeshindwa kufanya kazi zake ipasavyo na kusababisha usambazaji vitabu kunuka rushwa. 

 Hoja hiyo iliibua mvutano mkali kwa wabunge ambao baadhi yao walishauri iundwe Kamati Teule ya Bunge kuchukuza udhaifu huo na wengine wakitaka hoja hiyo ifanyiwe kazi na Serikali.
 Mbunge wa Kuteuliwa (NCCR- Mageuzi Mhe James Mbatia (kushoto) akiongea na waandishi wa habari  katika Ukumbi wa Msekwa mjini Dodoma baada ya kuambiwa aondoe hoja yake ambako alikataa.(Mwengine), ni  Mnadhimu Mkuu wa Upinzani Mhe Tundu Lissu

 Naibu Waziri wa Fedha Mhe Janet Mbene(kushoto) akisalimiana na Mbunge  Khalifa Suleiman Khalifa (Gando) kat[ka viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma
 Wabunge wa Upinzani Mjini Dodoma leo walipokutana na waandishi wa habari na kutoa taarifa ya msimamo wao baada ya Mbunge wa Kuteuliwa (NCCR – Mageuzi) Joseph Mbatia kuambiwa aondoe hoja yake Bungeni  na kukataa
Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai (kulia) akisalimiana na Mbunge wa Kuteuliwa (NCCR-Magaeuzi) James Mbatia katika viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma. Picha zote na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO
Kwa habari kamili BOFYA HAPA

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115013

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>