

Moto mkubwa umezuka na unakiunguza kiwanda cha vipodozi cha ChemiCotex kilichopo huko Africana njia ya Tegeta jijini Dar es Salaam.
Chanzo cha moto huo hakijafahamika ingawaje inahisiwa kuwa huenda ni hitilafu iliyotokana na fundi aliyekuwa akichomelea kitu ndani ya kiwanda hicho.
Wahusika wakuu wa kiwanda hicho hawakuwa katika eneo husika ili kutoa maelezo zaidi. Taarifa zinasema kuwa magari ya kikosi cha zima-moto yalipowasili, watu walianza kuyarushia mawe kiasi cha kutishia usalama wa watu wengine ambao waliamua kuondoka kutoka katika eneo la tukio.
Jitihada za kumtafuta kamanda wa polisi wa kanda maalum ya Dar es Salaam Suelein Kova bado zinaendelea baada ya simu yake kuita bila kupokelewa