Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 116996

MICHUANO YA KINONDONI MEYA CUP YASHIKA KASI

$
0
0
Manispaa ya Kinondoni ni moja ya wateja wakubwa wa NMB lakini pia Manispa ya kinondoni inaongoza kwakua na wakazi wengi zaidi ya manispaa nyinginezo. Hivyo basi kwa kulizingatia hili na kuendelea kuimarisha mahusiano mazuri kati ya NMB na Manispaa ya Kinondoni NMB imedhamini mashindano yanayoendelea katika wilaya ya kinondoni . Mashindano ambayo yanawahamisisha vijana katika kuimarisha ulinzi na usafi.Michuano hii ambayo inazinduliwa katika awamu tatu tofauti na katika sehemu tatu tofauti, mwishoni mwa wiki ikiwa ndio uzinduzi wa pili ulishirikisha kata ya Mzimuni na Ndugumbi ambapo Ndugumbi waliibuka kidedea kwa 1-0

Mheshimiwa Iddi Azan Mbunge wa Jimbo la kinondoni akikagua vikosi vya mpira wa miguu kata ya Ndugumbi na Mzimuni mwishoni mwa wiki ambao wapo katika michuano ya kinyang’anyiro cha Kinondoni Meya Cup 2013 inayoendelea katika kata tofauti wilayani humo.Mashindano haya yakiwa na kusudi la kuhamasisha Usafi na ulinzi Benki ya NMB ikiwa ndio wafadhiri wakuu na TVS King watatoa zawadi ya pikipiki ya miguu mitatu kwa mshindi wa kwanza

Mchezaji Abdul Hussein wa timu ya Ndugumbi akiwakabili vilivyo wachezaji wa timu ya Mzimuni katika michuano ya kuwania kombe la meya wa kinondoni 2013 katika mechi zinazoendelea kwenye wilaya ya kinondoni Katika mechi zilizochezwa mwishini mwa wiki Ndugumbi waliibuka kidedea kwa 1-0

Viewing all articles
Browse latest Browse all 116996

Trending Articles