Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba amesema maambukizi ya virusi vya ukimwi yamepungua kwenye Wilaya ya Tandahimba na amewataka wananchi kujiepusha na maambukizi mapya
Ameyasema hayo leo asubuhi wakati akitoa taarifa kwa kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru Mzee Mkongea Ally katika Kijiji cha Nanyhanga
Mwenge wa Uhuru umepitia miradi ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Bil 1.7 Wilayani humo na yote imeridhiwa.