Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 116996

SEKRETARIETI YA CCM YATEMBELEA MRADI WA DARAJA LA MAlAGARAsI MKOANI KIGOMA LEO

$
0
0

Ujumbe wa Sekretarieti ya CCM,ukiongozwa na Katibu Mkuu,Ndg. Abdulrahman Kinana,Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye ukiwa katika matembezi ya kuangalia maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Malagarasi na Ujenzi wa Barabara ya kutoka Kidawe mpaka Uvinza kwa kiwango cha lami leo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana (kushoto) akizungumza na Meneja wa Kampuni ya HANIL ambao ni Wakandarasi wa ujenzi wa Daraja hilo,Bw. Jung-Sik You kutoka nchini Korea.
Meneja wa Kampuni ya HANIL ambao ni Wakandarasi wa Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Malagarasi na Ujenzi wa Barabara ya kutoka Kidawe mpaka Uvinza kwa kiwango cha lami,Bw. Jung-Sik You (kushoto) akitoa maelezo machache juu ya maendeleo ya ujenzi wa Daraja hilo kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana na kuahidi kuwa mpaka ifikikapo mwezi Septemba ama Oktoba,Daraja hilo litakuwa limeshakamilika na kulikabidhi kwa Serikali.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nguruka,Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma leo,waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza na pia kusikiliza shida zao wakati alipofanya ziara ya kutembelea vijiji viwili vya Wilaya hiyo ya Uvinza.
Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akiwasalimia wananchi wa Kijiji cha Nguruka,Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma leo.
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Uvinza,Wilayani Uvinza mkoani Kigoma leo.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Viewing all articles
Browse latest Browse all 116996

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>