Makumbusho ya Taifa Tanzania ipo katika maandalizi ya kuwaenzi wanamichezo mbali mbali walio ipatia sifa Tanzania kutokana na juhudi mbali mbali walizo zionesha kupitia nafasi zao za uwanamichezo ndani nan je ya Nchi na kuifanya Tanzania ifahamike kimataifa.
Hayo yamesemwa na Kahimu Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho Tanzania Bi Eliwasa Maro pale alipo kuwa akifungua Mkutano ulio wajumuisha wadau wa ndani wa Makumbusho na wale wa kutoka katika taasisi za hapa nchini, uliofanyika katika Ukumbi mdogo wa Mikutano wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
Bi Maro aliongeza kuwa umefikia wakati sasa watanzania wakawaenzi wa wanamichezo wazamani na wa sasa ambao wameinyanyua vyema bendera ya Tanzania nje ya mipaka yetu kwani kwa kufanya hivyo tutatoa hamasa kwa wanamichezo wanao chipukia katika nyanja tofauti tofauti za michezo.
Akizungumzia lengo la Onesho hilo, Bw, Fredrick Mwakalebela ambae ndie Mratibu wa onesho hilo alisema kuwa onesho limelenga kuifanyia kazi wito wa Mh Jakaya M. Kikwete Rais wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania alio utoa Mkakumbusho ya Taifa mwaka 20012 alipo ya zindua majengo ya Mradi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam wa Makumbusho kuwa na onesho la wanamichezo walio tukuka na walio ipatia sifa Taifa letu kwa lengo la kutunza kumbu kumbu zao.
Bw Mwakalebela ametoa wito kwa vyama vya Michezo/Taasisi na Mashirika mbali mbali kujitoleza katika kufanikisha zeozi hili muhimu kwa maslahi ya Taifa letu hasa katika tasnia ya Michezo nchini.
Bi Flower Manase na Bi Irene Mville waandalizi wa onesho hili na ni wahifadhi wa Makubusho ya Taifa, wamesema kuwa maandalizi yanakwenda vizuri na kwa hatua ya sasa ni ushirikishwaji wa wadau wa michezo nchini ili kupata mawazo ya kulifanikisha onesho hilo linalo tarajiwa kuzinduliwa rasmi mwezi March 2013
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho Tanzania (wa pili kushoto),Bi Eliwasa Maro akifungua Mkutano wa Wadau wa Michezo Nchini katika kujadili namna ya kufanikisha onesho la Wanamichezo Tanzania, linalo andaliwa na Makumbusho ya Taifa.
Bw, Chance Ezekiel akitoa maoni yake mbeli ya wajumbe wa Mkutano wa ufanikishaji wa Onesho la Wanamichezo wa Tanzania.
baadhi ya wajumbe wakifuatilia kwa karibu maoni ya wajumbe katika kujadili namna ya kufanikisha onesho la wachezaji linalo andaliwa na Makumbusho ya Taifa.