Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

WANANCHI WAHAMASISHWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUCHANGIA DAMU KWA HIARI KUOKOA MAISHA

$
0
0
Mpango wa Taifa wa damu salama kwa kushirikiana na asasi ya Evidence of action” umezindua kampeni ya kuokoa maisha ya mama na mtoto “ MAMA YE” tarehe 17/01/2013 jijini Arusha kwa kutoa elimu juu ya uchangiaji damu na kuendesha zoezi la uchangiaji damu.


Akiongea katika uzinduzi huo Meneja wa mpango wa taifa wa damu salama Dr Effesper Nkya alitoa shukrani za dhati kwa mtu mmoja mmoja na Taasisi mbalimbali ambazo zimekuwa zinashirikiana na Mpango kuhakikisha upatikanaji wa damu salama katika hosipitali zetu.

Dr Nkya katika hotuba yake alihamasisha wananchi juu ya umuhimu wa kuchangia damu kwa hiari mara kwa mara ili kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji huduma ya kuongezewa damu pia aliwashauri wananchi watunze usalama wa damu iliyomo mwilini mwao ili wanapochangia, iweze kusaidia wenye upungufu wa damu. Jumla ya chupa za damu 1040 zilikusanywa katika kipindi cha siku 5 ( tarehe13 mpaka 17 januari)

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>