Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115279

POLISI MKOANI KATAVI WALALAMIKIWA KUTOA SIRI ZA WATOA TAARIFA

$
0
0
Na Willy Sumia, Katavi

JESHI la polisi mkoani Katavi limetakiwa kubadili utendaji kazi wake ili kujenga imani ya ushirikiano baina ya jeshi hilo na wananchi katika juhudi za kuutokomeza uhalifu mkoani humo.

Hayo yalibainishwa jana na wananchi wa kata ya Kawajense katika mkutano wa hadhara wa polisi jamii uliofanyika katika eneo la Bar ya Web Site iliyoko jirani na shule ya msingi Nyerere katika kata hiyo mjini Mpanda ambapo Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi alikuwa akitoa elimu ya polisi jamii kwa wananchi.

Wananchi hao walilalamikia vitendo vya baadhi ya askari wa jeshi hilo kutoa siri ya watoa taarifa kwa wahalifu na hivyo kujenga chuki na kuhatarisha usalama wa watoa taarifa na hivyo kudhoofisha juhudi za kupambana na uhalifu mkoani humo.

Wakizungumza wananchi hao waliwasihi viongozi wa jeshi hilo ngazi ya wilaya kuiga utendaji kazi wa aliyekuwa mkuu wa polisi wa wilaya hiyo na baadaye kupelekwa mkoani kuwa aliweza kupambana na uhalifu hadi akafanikiwa kuondoa wimbi la ujambazi lililokuwa limeota mizizi wilayani Mpanda.

Akizungumza katika mkutano huo kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari aliwasihi wananchi kutokukata tamaa kwa changamoto ndogo ambazo zinaweza kutatuliwa na yeye mwenyewe tena kwa muda mfupi sana, wanachopaswa kufanya kuanzia sasa ni kumpa taarifa ni askari gani anafanya huo mchezo mchafu wa kiuaji.

Alisema anachoomba kwa wananchi ni kumpa taarifa kwa njia ya simu kwa namba alizozitoa au kumuona popote watakapokutana naye kuhusu matukio ya kuvujisha siri wanazotoa kwa jeshi la polisi ili aweze kuchukua hatua haraka na kwa wakati ili Katavi iendelee kuwa salama bila majambazi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115279

Trending Articles