Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akiwahutubia watu wenye walemavu walioalikwa katika hafla ya cha mchana kilicho andaliwa na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Bw. Reginald Mengi ikiwa ni katika kukaribisha mwaka mpya wa 2013 wa Walemavu hao.Waziri Mkuu alikuwa mgeni rasimi katika hafla hiyo.
Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akiasalimiana na Bi. Regina Mengi mtoto wa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Bw. Reginald Mengi wakati wa hafla ya watu wenye Ulemavu iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akisalimiana na Redd's Miss Tanzania,Brigit Alfred ambaye alikuwa ni miongoni mwa wageni waalikwa katika kushiriki chakula hicho cha mchana na watu walemavu kilichoandaliwa na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Bw. Reginald Mengi.
Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akimsalimia mtoto Abrahamu Omari (miezi 3) aliyebebwa na mama yake ambaye ni mlemavu wa ngozi anaitwae Amina Fadhili wakati wa hafla ya Chakula cha Mchana iliyoandaliwa na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Bw. Reginald Mengi (nyuma ya Waziri Mkuu) ikiwa ni katika kuukaribisha mwaka mpya 2013.Picha na Chris Mfinanga.