Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 110202

TANTRADE YAZUNGUMZIA KUKAMILIKA MAANDALIZI MAONESHA YA BIASHARA SABASABA, KUANZA ASUBUHI HADI SAA TATU USIKU, WASHIIKI WAONGEZEKA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii 

MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara(TanTrade) imesema tayari maandalizi ya Maonesho ya biashara yamekamilika huku idadi ya washiriki ikiongezeka kwa kiwango kikubwa. Pia imesema mwaka huu wameongeza muda wa maonesho kwa lengo la kutoa nafasi kwa wananchi wengi zaidi kuyashuhudia,hivyo yataanza Juni 28 hadi Julai 13 mwaka huu. 

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TanTrade Injinia Christopher Chiza baada ya kukagua na kisha kujiridhisha na maandalizi ya maonesho hayo ya biashaara."Nimefurahishwa na maandalizi ya maonesho ya mwaka huu. 

"Hata hivyo nieleze kuwa tumetekeleza agizo la Rais Dk.John Magufuli ambapo alitutaka tuongeze muda wa kufanya maonesho haya na hivyo mwaka huu tumeongeza muda.Tutaanza Juni 28 na tutamaliza rasmi Julai 13 mwaka huu. "Cha kufurahisha zaidi idadi ya kampuni za nje zimeongezeka kutoka 30 mwaka jana hadi kampuni 33.Na kwa hapa nchini kutakuwa na 2900,"amesema. 

Pia amehoji kwanini watu wanapenda maonesho ya biashara , ambapo jibu ni kwamba kauli mbiu ya maonesho ya mwaka huu inasema Ukuzaji wa biashara kwa Maendeleo ya viwanda, hivyo uwepo wa viwanda lazima uendane na biashara na ndio maana washiriki wameongezeka. 

Amefafanua kwenye maonesho kama hayo ndiko ambako teknolojia wengi waniona na ni njia mojawapo ya kukuza biashara.Pia ametoa rai kwa Watanzania kupenda bidhaa zinazozalisha nchini kwani zina ubora wa kiwango kikubwa. Mhandisi Chiza amezungumzia pia mchakato wa eneo la TanTrade kuendelea kutumika kibiashara hata baada ya maonesho ya Sabasaba kumalizika na watazungumza rasmi wakikamilisha hatua zote. 

Amesema wanataka kulifanya eneo hilo kuendelea kutumika kwa biashara wakati wote.Hiyo itatoa nafasi ya wananchi kuendelea kulitumia eneo hilo kibiashara lakini mchakato wa mazungumzo unaendelea. 

Kwa upande wake Mkurugezi Mkuu wa TanTrade Edwin Ntagaruka amesema wananchi wajitokeze kwa wingi kwenye maonesho hayo kutakuwa na shughuli za aina mbalimbali za kibiashara. Pia amesema wanatambua kuwa wakati maonesho yakiendelea kuna michuano ya kombe la Dunia inaendelea nchini Urusi, hivyo licha ya muda wa kumaliza ni saa 12 jioni ,wameamua kuongeza hadi saa tatu usiku.

Kuhusu maandalizi amesisitiza yamekamilika na wanachojivunia kutakuwa na mambo mengi ya kuvutia kwa mwaka huu. Pia amesema TanTrade imekuwa ikitoa mafunzo ya mara kwa mara kwa wafanyabishara na mwaka huu wanatarajia kuzindua kliniki ya biashara ambayo jukumu lake itakuwa ni kuwasaidia wafanyabiashara nchini. Amesema kwenye kliniki hiyo ya biashara kutakuwa na madaktari bingwa wa kutibu magonjwa ya biashara na hiyo itasaidia katika kutatua changamoto zinazojitokeza. 
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TanTrade Injinia Christopher Chiza (kushoto),akizungumzia maandalizi ya Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa yanayotarajia kuanza Juni 28 mwaka huu hadi Julai 13 katika Viwanja vya Sabasaba.
Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Edwin Rutageruka akifafanua jambo kuhusu maonesho ya Biashara ya Kimataifa yanayotarajia kuanza Juni 28 mwaka huu katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam

Viewing all articles
Browse latest Browse all 110202

Latest Images

Trending Articles



Latest Images