Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

POLISI LINDI YAZUIA MAANDAMANO YA GESI YALIYOANDALIWA NA VYAMA VYA SIASA

$
0
0
Na Mwandishi wetu,Lindi

JESHI la Polisi mkoani Lindi,limezuia kufanyika kwa maandamano ya kuunga mkono majirani zao wa Mtwara,kupinga kusafirishwa kwa njia ya bomba la gesi asilia,kutoka mkoani humo kupelekwa Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kufufua umeme utokanao kwa rasilimali hiyo.

Kwa mujibu wa barua kutoka Ofisi ya Jeshi hilo,ambayo inaonyesha kukosewa kwa mwezi na mwaka,yenye kumbukumbu LND/271/VOL.1/17 ya Decemba 17/2012,na mwandishi wa habari hizi kupata nakala yake,na kusainiwa na Kamanda George Mwakajinga,imepelekwa kwa vyama vinne vya siasa.

Vyama vilivyopelekewa barua za zuio la maandamano hayo ni pamoja na Chama cha mapinduzi (CCM), (CUF), CHADEMA na NCCR-MAGEUZI.

Kwa mujibu wa barua hiyo,inawataka viongozi wa vyama hivyo vinne vya siasa kuchukua hatua mapema ya kuwasihi na kuwaelimisha wanachama wao kwanza, kwa ujumbe wa gesi kama ulivyotolewa na wananchi wa mkoa wa Mtwara.

“Napenda kuchukuwa nafasi hii kuwaandikia kuwakumbusha tarehe kuwa 04/01/2013,siku ya Ijumaa mkuu wa mkoa wa Lindi,Ludovick Mwananzila alipata fursa ya kuwaalika wadau wote,wazee wa mji wa Lindi,viongozi wa madhehebu ya dini na vyama vya siasa,alizungumzia na kufafanua mwelekeo na msimamo wa Serikali katika suala la gesi na jinsi mkoa unavyochangia pato la Taifa kwa gesi ya Songosongo na jinsi anavyojiandaa kwa ugunduzi mpya kwenye kina kirefu cha bahari ya Hindi wilaya ya Kilwa”Imeeleza sehemu ya barua hiyo.

Aidha,barua hiyo imeeleza kwamba Jeshi hilo la Polisi,lisingependa kukwaruzana na jamii katika maandamano hayo ya barabarani kwa hoja za kisera za kiuchumi ambazo ni za ki-Taifa, zinazoweza kuzungumzika katika mifumo mingine ya kiutawala kama vile katika vikao vya Bunge.

“Tunaomba ushirikiano na ushirikishwaji wa Jamii katika utii wa sheria bila Shuruti katika kudumisha amani na utulivu ndani ya mkoa wa Lindi”Imeeleza barua hiyo.

Baadhi ya viongozi na wanachama wa vyama vilivyopelekewa barua hizo,wamemuomba kamanda huyo wa Polisi mkoani hapa,George Mwakajinga,kutoupotosha umma juu kauli yake,kwani maandamano yanayotarajiwa kufanywa ni kuunga mkono jirani zao wa Mtwara katika kutetea gesi iliyogunduliwa huko kutopelekwa nje ya mkoa huo kwa njia ya Bomba,na sio kupinga kauli ya mkuu wa mkoa wa Lindi.

“Sisi tunawaunga mkono jirani zetu wa Mtwara, juu ya kuondolewa gesi kupelekwa Dar es salaam,kwani huo ni uonevu na unyang’anyi mkubwa unaofanywa na hawa viongozi wetu waliopo madarakani”

“Kwani sisi watu wa mikoa ya kusini tumeikosea nini hii Serikali,kama ni gesi tumewapa kutoka Songosongo Kilwa,licha ya wenzetu kuizuia kwa njia ya kiustaarabu,yaani kuifikisha mahakamani,lakini tuliwaachia na Kilwa kukosa kiwanda cha mbolea kama ilivyokuwa imepangwa,sasa leo wanataka kuihamisha ya Mtwara tuendelee kuwa masikini”Walisema viongozi na wanachama hao.

Januari 04 mwaka huu,viongozi wa Chama cha wananchi (CUF) mkoani Lindi, wakiwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja vya Sera,Manispaa ya Lindi,Walitoa wito kwa wananchi kushiriki katika maandamano yatakayofanyika Februari 23 mwaka huu,ili kuwaunga mkono jirani zao wa mkoa wa Mtwara,kupinga uamuzi wa Serikali kusafirisha gesi kwa njia ya bomba na kuipeleka Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuongeza upatikanaji wa nishati ya umeme.

Mambo mengine yaliyotajwa na viongozi hao ni pamoja na kuwepo kwa mfumo wa ununuzi wa mazao kwa utaratibu wa mfumo wa Stakabadhi ghalani, kwa maelezo kwamba umekuwa hauwasaidii walengwa (wakulima) na badala yake umekuwa ukiwasaidia wachache

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>