Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 110202

WATU 10 WAFARIKI DUNIA KIGOMA BAADA YA BASI KUGONGANA NA TRENI

$
0
0
*Kamanda wa Polisi Kigoma aelezea hatua kwa hatua namna ilivyotokea

 Na Ripota Wetu, Kigoma

WATU 10 wamefariki dunia na wengine 26 wamejeruhiwa baada  ya basi la Hamida Trans lenye namba za usajili T 885 DLD iliyokuwa ikitokea Kigoma kwenda Tabora kuligonga treni. 

Akizungumzia ajali hiyo leo Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Kigoma Martine Otieno amesema  imetokea eneo la kivuko Bungo Relini mkoani humo.Amefafanua dereva wa  basi licha ya kupigiwa honi na  treni hakusimama eneo la kivuko na hivyo akagongwa. 

Ameongeza baada ya kutokea ajali hiyo  abiri 10 wamepoteza maisha wakiwamo saba waliofariki eneo la tukio na wengine watatu walifariki dunia wakiwa hospitali wakiendelea kupatiwa matibabu. 

Kamanda Otieno amesema ndani ya basi kulikuwa na jumla ya abiria 18 pamoja na dereva na utingo wake na kufanya jumla ya idadi waliokuwamo kufikia 20.Ameeleza kiss kati ya  hao waliofariki dunia wanaume ni saba na wanawake watatu. 

Pia amesema baada ya basi holiday kugonga treni liliburuzwa umbali wa mitambo 100 na hivyo kusababisha majeruhi wengine 17 waliokuwamo pembezoni mwa reli. "Katika ajali  hiyo waliokuwamo ndani ya basi ni watu 20,waliopoteza maisha ni 10,maheruhi tisa na mmoja amenusurika na majeruhi wengine 17 hawa waliokuwamo pembezoni mwa reli.

"Hivyo idadi ya  majeruhi wote ni 26 na chanzo cha ajali  ni uzembe wa dereva wa  basi ambaye aliamini atawahi kuvuka kivuko cha reli na matokeo yake amesababisha kutokea kwa ajali hiyo, "amesema Kamanda Otieno.
 Baadhi ya majeruhi wa ajali wakiendelea na matibabu katika hospitali  ya mkoa wa kigoma.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 110202

Latest Images

Trending Articles





Latest Images