Nakala ya hukumu ni haki yako ikiwa ulikuwa mhusika katika kesi au shauri. Unakuwa mhusika katika kesi au shauri pale unapokuwa mshitaki au mshitakiwa, mlalamikaji au mlalamikiwa, au mhusika mwingine mwenye maslahi. Hapa ndipo unapohesabika kuwa mhusika katika kesi au shauri na hapa ndipo unapokuwa na haki ya kuomba kupatiwa nakala ya hukumu.
Makala yaliyopita yalieleza kuwa nakala ya hukumu ni muhimu hasa ukitaka kukata rufaa au kuchukua hatua zaidi , lakini pia ni muhimu kama nyaraka ya kumbukumbu kwa ajili ya kesho, pia ni muhimu kwa ajili ya utekelezaji wa kile kilichoamuliwa. Leo tuone mfano halisi wa barua ya maombi ya nakala ya hukumu
kama ulivyo hapa chini ;-
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, 24 / 5 / 2018
S.L.P..............................
Dar es salaam.
YAH ; MAOMBI YA KUPATIWA NAKALA YA HUKUMU.
Nilikuwa mlalamikiwa katika shauri namba 13 la mwaka 2018, ambalo limetolewa hukumu tarehe 22 / 3 / 2018, mbele ya Mhe. Kijana Mponela. Ninaomba kupatiwa nakala ya hukumu kwa kumbukumbu au hatua zaidi.
Wako
Mti Mkavu
( Aliyekuwa mlalamikiwa ).
0717600900
Sahihi...............................
KUSOMA ZAIDI sheriayakub.blogspot.com