Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 110202

TaESA WAKANUSHA TAARIFA YA TANGAZO LA AJIRA LINALOSAMBAA MTANDAONI

$
0
0
WAKALA wa Huduma za Ajira Tanzania(TaEsa) umesema umesikitishwa na taarifa potofu ambazo zinasambazwa kupitia tangazo la ajira .

Imefahamika taarifa hiyo inayosambaa kupitia tangazo hilo inasomeka ‘’CHINI YA MH:RAIS WETU DKT JOHN POMBE MAGUFULI KUPITIA SHERIA YA UANDIKISHAJI VIZAZI NA VIFO SURA 108 YA MWAKA 2000’’ kwamba tunatangaza ajira kwa vijana wote waliomaliza mafunzo ya uwalimu ngazi ya cheti,stashahada na waliosoma vyuo vya utumishi wa umma ngazi ya cheti.

Taarifa hiyo ya upotoshaji inaendelea kueleza mchakato wa usajili ajira linaratibiwa na RITA kwa kushirikiana na TaESA na kwamba maombi yameanza kupokelewa Mei 5 mwaka 2018 hadi Julai 7 mwaka 2018 na hivyo waombaji wote watume maombi yao kupitia barua pepe, taesa.ritarecruitment.go.tz@outlook.com.

Taarifa ya TaESA imesema leo jijini Dar es Salaam imefafanua tangazo hilo ni uzushi na utapeli wa wazi kwani RITA haina utaratibu wa kutangaza ajira kupitia utaratibu huo ulioainishwa hapo juu.

Imefafanuliwa badala yake ajira zote zinatangazwa kwa kufuata taratibu zilizowekwa na kusimamiwa na Sekretarieti ya Ajira na siyo TaESA.Aidha wamesena wanachukua fursa hiyo kuwatahadharisha wananchi kuhusu watu wanaojifanya kuwa ni Mawakala wa RITA chini ya Kampuni yao ya Mtema Brokers Limited ambao wanafanya kazi za usajili wa vizazi na vifo katika Mikoa mbalimbali Tanzania Bara.

TaESA imeelezwa watu hao ni matapeli hivyo yeyote mwenye taarifa sahihi afike kituo cha Polisi kilichopo karibu naye au awapigie kwa namba za simu hapo juu.Kampuni hiyo imeshawatapeli wananchi katika maeneo ya Kipunguni B,Temeke,Kinondoni,Kigamboni Sinza Jijini Dar es salaam na Mlandizi mkoani Pwani ambapo zaidi ya wananchi 1000 wametapeliwa fedha zao.
 Afisa habari wa TaESA, Jamila Mbarouk akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo  jijini Dar es Salaam , kuhusu kukanusha na kuwaomba wananchi wasitume fedha katika Kampuni ya  Mtema Brokers Limited watatapeliwa pesa zao.
 Afisa habari wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA),Jafari Hamadi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kukanusha taarifa zilizo enea katika mitandao ya kijamii na kubandikwa katika semu mbalimbali unaosema kwamba wametangaza ajira, Tangazo hilo ni uzushi na utapeli wa wazi kwani RITA haina utaratibu wa kutangaza ajira kupitia utaratibu huo.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Mkutano ukiendelea.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 110202

Latest Images

Trending Articles





Latest Images