Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 110192

WAJASIRIAMALI WANAWAKE 200 MKOANI KIGOMA WAPATIWA MAFUNZO KUWAIMARISHA KIUCHUMI

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel, Kigoma

WANAWAKE 200 ambao ni wajasiriamali mkoani Kigoma wanataraja kupata mafunzo yatakayosaidia kuwaimarisha kiuchumi na lengo ni kuhakikisha wanapata maendeleo katika mkoa huo na Taifa kwa ujumla hasa kipindi hiki cha kutekeleza sera ya Tanzania ya viwanda.

Awali akifungua rasmi mafunzo hayo jana mkoani humo na yanatarajiwa kudumu kwa siku 10 katika halmashauri zote mkoani hapa Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Kigoma Gaden Machunda ametoa msisitizo kwa akina mama kujikita katika ujenzi wa viwanda.

Aidha Machunda amewataka akina mama kuzingatia misingi ya ujasiriamali pamoja na kuwa na nidhamu na biashara wanazozifanya huku akiwataka wauzaji wa hoteli na migawa kuwa nadhifu ili kuwavutia wateja.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya AJ General Company amesema lengo la mradi huo ni kuwawezesha wanawake na kusaidia kutekeleza Ilani ya Serikali ya awamu ya 5  kuelekea ujenzi wa Tanzania ya viwanda.Ambapo amesema wanawake watainuka kiuchumi kupitia mpango huu na wanawake watapata mikopo isiyokuwa na masharti kama ilivyokuwa hapo awali lakini pia kuwezesha bidhaa zinazozalishwa mkoani hapa kupata soko nje ya nchi.

Katibu wa Umoja wa Wanawake mkoani Kigoma (UWT) Edina Kuguru amesema wao kama viongozi wa wanawake wamejipanga kuhakikisha wanawake wote mkoani hapa wanaondokana na mfumo wa kuwategemea wanaume.Amesema mikakati waliyonayo ni kutoa elimu ya ujasiriama na jinsi ya kutumia fedha wanazopewe zinatumika ipasavyo na kuwatafutia masoko kwani wana mipango ya kuanzisha viwanda vya mihogo kwa kuwa zao hilo linalimwa sana mkoani Kigoma.

Mmoja wa wajasiriamali wa Mkoa wa Kigoa Maisala Barakabise amesema wanawake wa mkoa huo wanajitahidi kufanya biashara kwa kutumia mitaji yao na wao ndio walezi wa familia na ni wathubutu.Hivyo wakiwezeshwa wanaweza zaidi na kuongeza wamekuwa wakiibua fursa nyingi.

Amesema changamoto wanazokumbana nazo katika kutafuta kipato na kujiondoa katika dimbwi la umasikini ni mitaji modogo.Mjasiriamali mwingine Sakina Kabeza amesema wanawake wa Kigoma ni wachapakazi na wanajituma na kufafanua kipindi cha nyuma fursa zilikuwa ni chache lakini kwa sasa Awamu ya tano imejipanga kikamilifu kutoa fursa kwa wanawake wote.

"Na endapo wanawake wa Kigoma wakipatiwa elimu na mitaji wanaouwezo wa kufanya vitu vya tofauti na wanao uwezo wa kuchangamkia fursa kujikwamua kimaisha,"amesema.Aidha ameipongeza taasisi hiyo iliyojitokeza na kutoa elimu na mikopo kwa wanawake mkoani Kigoma.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 110192

Latest Images

Trending Articles





Latest Images