Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 110193

WAKULIMA ZAO LA KARAFUU WILAYA YA MKINGA WAISHAURI SERIKALI KUWATAFUTIA KUPATA SOKO

$
0
0
Na David John, Tanga

WAKULIMA wa zao la Karafuu wilayani Mkinga mkoani Tanga wameishauri Serikali kusimamia zao hilo kama wanavyofanya katika mazao ikiwa pamoja na kupata soko la uhakika huku pia itambulike hata wakazi wa  wilayani hapa wanalima kwa wingi zao hilo.

Wakulima hao wamefafanua Serikali yenyewe inatambua karafuu inapatikana tu visiwani Zanzibar lakini ukweli ni kwmba nao wanalima kwa wingi zao hilo pamoja na mazao mengine.Akizungumza leo Mwenyekiti wa Kijiji cha Mhesambia kilichopo Kata ya Kigongoi Mashariki Stephano Banda amesema kijiji chao  kinachounda na vitongoji zaidi ya vitatu wanalima kwa wingi zao la karafuu lakini changamoto kubwa wanayokabiliana nayo ni soko la zao hilo.

Amesema kuna wakulima wanamiliki mashamba makubwa ya karafuu na ndio zao kuu kwao lakini mara zote wamekosekana wawekezaji au wafanyabiashara wakubwa wa kununua zao hilo na kusababisha wakulima wake kukata tamaa ya kilimo hicho."Nataka nikuwahakikishie wananchi wa huku wanalima sana zao la Karafuu lakini changamoto kubwa ni soko , hivyo ni vema Serikali 
wakaweka nguvu kama ambavyo inafanya kwenye mazao mengine,"amesema.

Ameongeza Kijiji cha Mhesambia ni kikubwa mno katika wilaya ya Mkinga na kimsingi wananchi wake ni wakulima na zao kubwa ukiondoa mazao mengine kama mpunga, pilipili na mengineyo lakini Karafuu lakini akasisitiza changamoto ni soko.Mkazi wa Kijiji hicho Agustino Hassan amesema changamoto hizo katika eneo hilo ni  barabara, kukosa soko la uhakika , maji na umeme na hivyo iwapo zitaondolewa wananchi watapiga hatua kibwa kimaendeleo.

Amesema wananchi wanajitahidi kulima  na kuzalisha mazao lakini mvua ikinyesha tu kwa wingi ni shida kwani miundombinu ya barabara inakuwa haipitiki hasa kutoka Maramba hadi Daruni na kupanda Hemsambia.Akizungumzia changamoto za wakulima Diwani wa Kata hiyo ya Kigongoi Mashariki  A Mary Semhunge amesema miudombinu ya barabara inakwamisha wananchi kufanya kazi zao za kilimo kwa uhakika.

"Kuhusu zao la karafuu ni kweli wakulima wanalima kwa wingi na tayari tumekaa na Mbunge kuona namna gani panakuwepo na mkakati wa kuwa na kiwanda kidogo cha kuchenjua na kufungasha 
zao hili ambapo kipekee kuna pia pilipili manga, mdalasini, "amesema Semhunge Kuhusu mkakati wa maji amesema wananchi wapo tayari kwenye mpango wa kuchimba bwawa kubwa na hivi sasa wanamsubiri mhandisi ili kuona mahala sahihi pakuchimba.

Akizungumzia umeme amesema katika umeme wa awamu ya tatu kata hiyo hasa kijiji  cha Kigongoi Mashariki A huku akiwataka wananchi kuendelea kushirikiana nao.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 110193

Latest Images

Trending Articles





Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>