Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 110192

SERIKALI YAIPONGEZA COCA-COLA KWA KUWEKEZA KATIKA MASHINDANO YA UMISSETA

$
0
0
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Seleman Jafo,ameipongeza kampuni ya Coca-Cola kwa kuwekeza kudhamini mashindano ya Shule za Sekondari nchini ya UMISSETA kwa kipindi kingine mwaka huu na kuahidi kuwa serikali nayo pia itaendelea kuiunga mkono. 

 Akifungua semina elekezi ya maofisa wa michezo kutoka mikoa 26 ya hapa nchini iliyofanyika mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki,ambapo pia aliambatana na Naibu Waziri wake, Joseph Kakunda, Waziri Jafo, alisema serikali inatambua mchango mkubwa wa kampuni ya Coca-cola wa kukuza vipaji vya michezo kwa vijana. 

 “Nimevutiwa sana na maandalizi na usimamizi wa mashindano ya michezo ya UMMISETA ulivyokuwa mwaka jana,kwa hili nawashukuru Coca-Cola,nafahamu kuwa mkataba wao ulikuwa wa kudhamini mashindano haya kuanzia mwaka 2015 hadi 2018,natoa wito kwao kuangalia uwezekano wa kuongeza muda wa udhamini ikibidi hata kuwa na haki ya kuyasimamia moja kwa moja,”alisema Jafo.  
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Seleman Jafo, akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina elekezi ya maofisa michezo ilifanyika katika Chuo Cha Mipango cha Dodoma. Semina hiyo ilihudhuriwa na maofisa michezo wa mikoa kutoka mikoa 26 ikiwemo na  Zanzibar.
Baadhi ya maofisa michezo walioshiriki semina elekezi wakifuatilia hotoba ya Waziri Jafo
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Seleman Jafo, (Kushoto) akisalimiana na Meneja wa Chapa ya Cola-Cola nchini, Sialouise Shayo. Wengine pichani ni Maofisa wa Coca-Cola na Maofisa Michezo.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 110192

Latest Images

Trending Articles





Latest Images