Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115299

UFUNGUZI WA VISIMA 30 KATIKA MAENEO YA WILAYA 6 KAME TANZANIA VILIVYOCHIMBWA KWA MSAADA WA SERIKALI YA MISRI WAFANYIKA WILAYANI MASWA

$
0
0
Waziri wa Maji na Umwagiliaji  Profesa Jumanne Maghembe (katikati) akishirikiana na Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Serikali ya Misri Prof. Dr. Mohamed Bahaa El-Din Ahmed (kulia) kukata utepe kuashiria ufunguzi wa visima 30 katika maeneo ya wilaya sita kame, Tanzania vilivyochimbwa kwa msaada wa serikali ya Misri uliofanyika jana katika kijiji cha Mwanang'ombe wilayani Maswa mkoani Simiyu. Kushoto kabisa ni Mhe. Pascal Mabiti ambaye ni mkuu wa mkoa wa Simiyu.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Serikali ya Misri Prof. Dr. Mohamed Bahaa El-Din Ahmed akionja ladha ya maji toka kwenye bomba kuu la chanzo cha maji yanayoelekezwa kwenye bomba la utekaji maji kijiji cha Mwanang'ombe wilayani Maswa mkoani Simiyu ikiwa ni moja kati ya hatua za serikali ya Tanzania kusaidia wananchi wake kukabiliana na tatizo la upatikanaji wa maji salama.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Serikali ya Tanzania Jumanne Maghembe naye akionja ladha ya maji toka kwenye bomba kuu la chanzo cha maji yanayoelekezwa kwenye bomba la utekaji maji kijiji cha Mwanang'ombe wilayani Maswa mkoani Simiyu ikiwa ni moja kati ya hatua za serikali ya Tanzania kusaidia wananchi wake kukabiliana na tatizo la upatikanaji wa maji salama.

Mbunge wa jimbo la Busega mkoani Simiyu  Titus Kamani naye akionja ladha ya maji toka kwenye bomba kuu la chanzo cha maji yanayoelekezwa kwenye bomba la utekaji maji kijiji cha Mwanang'ombe wilayani Maswa mkoani Simiyu ikiwa ni moja kati ya hatua za serikali ya Tanzania kusaidia wananchi wake kukabiliana na tatizo la upatikanaji wa maji salama.

Mama Maria akiondoka kwenye eneo la bomba kuu la kutekea maji mara baada ya kutwishwa ndoo na Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Serikali ya Misri Prof. Dr. Mohamed Bahaa El-Din Ahmed huku wananchi wengine wakipiga makofi kuashiria kufurahia tukio hilo lililofanyika katika kijiji cha Mwanang'ombe wilayani Maswa mkoani Simiyu.Picha kwa hisani ya Gsengo Blog.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115299

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>