Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 110189

WAZIRI MHAGAMA: MUSWADA SHERIA MFUKO WA HIFADHI YA JAMII KUNUFAISHA WATUMISHI WA UMMA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema kupitishwa kwa muswada wa Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii utasaidia kuwanufaisha watumishi wa umma kwa kurahisisha utoaji wa huduma kwa wakati na wenye tija.

Amebainisha hayo wakati wa Mkutano wa Baraza Kuu la Taifa la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) walipokutana Mjini Dodoma katika warsha ya siku tano kuanzia Januari 29 hadi Februari 02, 2018 kujadili masuala ya wafanyakazi nchini.

Waziri Mhagama alieleza kuwa, kupitiswa kwa muswada ni moja ya utekelezaji wa takwa la Ibara ya 11 kifungu kidogo cha kwanza cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulipoona umuhimu wa kuweka mifumo ya hifadhi ili Watanzania wapate manufaa hasa siku za uzeeni.

“Maamuzi ya kuwa na Muswada huu umezingatia taratibu zote za kisheria ikiwemo Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Sera ya Hifadhi ya Jamii, Mkataba wa Shirika la Kazi Duniani unaoongoza katika maswala ya Hifadhi ya Jamii”.Alisisitiza Mhagama.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza jambo wakati wa Mkutano wa Baraza Kuu la Taifa la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Rayal Village Dodoma Februari 01, 2018.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiimba wimbo wa Umoja na Mshikamano wakati wa Mkutano wa Baraza Kuu la Taifa la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Dodoma.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Erick Shitindi akionesha ishara ya umoja na mshikamano wakati wa Mkutano wa Baraza Kuu la Taifa la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) uliofanyika Dodoma.
 Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa Baraza Kuu la Taifa la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) wakifuatilia ujumbe kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) aliowasilisha katika mkutano huo.
 Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) Bw. Suleiman Kikingo akichangia hoja wakati wa Mkutano wa Baraza Kuu la Taifa la chama hicho uliofanyika Ukumbi wa Royal Village Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa Baraza Kuu la Taifa uliofanyika Dodoma.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Viewing all articles
Browse latest Browse all 110189

Latest Images

Trending Articles





Latest Images