Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 110189

AZAM FC YAANZA TAMBO KUELEKEA MCHEZO DHIDI YA NDANDA

$
0
0
Na Agness Francis, Globu ya Jamii 
MABINGWA wa Afrika Mashariki na Kati Azam Fc  wanatarajia kushuka dimbani kesho kuumana na  Wanakuchere NdandaFc katika mchezo wao wa marudiao raundi ya pili, Ligi kuu Tanzania Bara utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari AzamFc  Jaffary Iddy Maganga, amesema katika mtanange huo utakaoanza saa 10 jioni, kikosi chake kitawakosa wachezaji wake mahiri 5.

Amewataja wachezaji hao ni Himidi Mau, Waziri Junior, Joseph Mahundi, Joseph Kimwaga na Aboubakar Salum  maarufu  kama (Sure Boy) anayetumikia adhabu ya kadi Nyekundu aliyoipata wakati wa mechi dhidi ya Mabingwa watetezi Tanzania Bara  Yanga SC. 

"Licha ya kuwakosa wachezaji hao, tuko vizuri na kikosi chetu ni kipana chenye uwezo mkubwa, tutahakikisha tunapambana vikali dhidi ya Wanakuchere ili tunachukue pointi 3,"amesema Jaffary Maganga. 

Kwa upande wake Kocha Mkuu wa Azam Fc  Aristica Cioaba amesema kuwa wamejiandaa vema kwa mchezo huo kiakili, kimwili huku akitamba kuwa kikosi chake kiko kwenye mazingira mazuri.
Afisa Habari AzamFc,  Jaffary Iddy Maganga akizungumza na waandishi wa habari katika kuelekea   Mtanange  wa patashika nguo kuchanika pale Uwanja  wa Azam Complex Chamazi wakiwa wenyeji wa NdandaFc  katika kuuchapa mchezo  wao wa Marudiao raundi ya 2 Ligi kuu Tanzania Bara.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 110189

Latest Images

Trending Articles



Latest Images