Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 110192

TUSIIME YATESA TENA KIDATO CHA NNE

$
0
0
Shule ya Tusiime imeendelea kufanya vizuri katika matokeo ya kitaifa ya kidato cha nne kwa kufaulisha asilimia 100 ya watahiniwa wake wote 303.

Kwenye matokeo yaliyotangazwa jana na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), shule hiyo imeendelea kufaulisha wanafunzi wake wote kwa ufaulu wa juu huku ikiwa na idadi kubwa ya wanafunzi kuliko shule zote 100 bora kitaifa.Shule hiyo ilikuwa na wanafunzi 303 waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana, kati ya hao, wanafunzi 59 wamepata daraja la kwanza, wanafunzi 161 daraja la pili na wanafunzi 62 daraja la tatu na 21 tu ndio wamepata daraja la nne.

Mkuu wa shule ya sekondari Tusiime, Emil Rugambwa, alifurahia sana matokeo hayo akisema ni mafanikio makubwa ikizingatiwa kuwa shule hiyo ilikuwa na idadi kubwa ya watahiniwa ambayo ni zaidi ya mara tatu ya watahiniwa wa baadhi ya shule zilizoingia kumi bora.

“Kwetu haya ni mafanikio makubwa sana kwani kufaulisha wanafunzi 212 kwa daraja la kwanza na la pili si jambo jepesi ni la kupongeza, nawapongeza walimu wangu na uongozi wa shule kwa matokeo haya mazuri, sisi tulikuwa na wanafunzi 303 na wamefaulu vizuri “ alisema Rugambwa.

“Shule yetu siyo ya vipaji maalum hivyo inachukua wanafunzi wenye uwezo wa kawaida sana kitaaluma na kuwajengea mazingira wezeshi ya kila mmoja kutimiza ndoto yake na mwisho wake wanafaulu mitihani yao ya kitaifa,” alisema

Naye Mkurugenzi wa shule hizo, Albert Katagira, alisema matokeo hayo mazuri yanatokana na dhamira waliyonayo kama taasisi kuhakikisha vijana wa Tanzania wanapata elimu bora katika mazingira yaliyo safi na salama.

“Napenda kuwathibitishia wazazi na wadau wote wa elimu kuwa shule za Tusiime zitaendelea kutoa elimu bora hapa nchini kama sehemu ya mchango wake kwa jamii ya watanzania kuandaa rasilimali watu wenye maarifa, ujuzi na weledi kwa manufaa yao, familia zao na taifa kwa ujumla,” alisema.

Alisema katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, shule hizo zimeweka mikakati mizuri iliyohakikisha kwamba kila mwanafunzi aliyejiunga na shule hizo anafaulu mitihani yake ya kitaifa.
Mkuu wa shule ya Tusiime, Emil Rugambwa, akimkabidhi zawadi ya kitabu mwanafunzi wa shule hiyo, Godson Ezekiel aliyepata daraja la 1.8 kwenye matokeo ya kidato cha nne. Wanafunzi 59 wamepata daraja la kwanza, wanafunzi 161 daraja la pili na wanafunzi 62 daraja la tatu na 21 tu ndio wamepata daraja la nne.
Mwanafunzi Godson Ezekiel wa shule ya Tusiime aliyepata daraja la kwanza 1.8 kwenye matokeo ya kidato cha nne akiwa na wenzake shuleni hapo mara baada ya kuzawadiwa kitabu na Mkuu wa shule hiyo. Emil Rugambwa. Wanafunzi 59 wa shule hiyo walipata daraja la kwanza, wanafunzi 161 daraja la pili na wanafunzi 62 daraja la tatu na 21 tu ndio wamepata daraja la nne
Mratibu wa kidato cha nne shule ya Tusiime, Mitala Innocent akiwasomea wanafunzi wa shule hiyo matokeo ya kidato cha nne shuleni hapo ambapo wanafunzi wa shule hiyo 59 wamepata daraja la kwanza, wanafunzi 161 daraja la pili na wanafunzi 62 daraja la tatu na 21 tu ndio wamepata daraja la nne.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 110192

Latest Images

Trending Articles





Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>