Mgeni Rasmi katika Mkutano wa Wasambazaji wa Mafuta na Gesi hapa nchini,Jerry Silaa akizungumza machache wakati wa kufungua rasmi mkutano huo leo,kwenye Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Washauri wa Madini kutoka Wizara ya Nishati na Madini,Richard Kasesela akizungumza wakati akiwasilisha mada yake ya namna ya kupata leseni ya uwekezaji kwenye jamii hapa nchini.wakati wa Mkutano wa Wasambazaji wa Mafuta na Gesi hapa nchini unaofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Hyatt Regency,Dar es Salaam.Katika Mada yake hiyo,Pia Kasesela amesisitiza umuhimu wa Wawekezaji kuwa karibu na Jamii inayowazunguka ikiwa ni pamoja na kujenga makazi ya kudumu katika maeneo ya migodi yao.
Mwenyekiti wa Bodi ya Washauri wa Madini kutoka Wizara ya Nishati na Madini,Richard Kasesela akiendelea kuwasilisha mada yake ya namna ya kupata leseni ya kuweza uwekezaji kwenye jamii hapa nchini.wakati wa Mkutano wa Wasambazaji wa Mafuta na Gesi hapa nchini unaofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Hyatt Regency,Dar es Salaam.
Mhadhiri na Kiongozi wa Wanafunzi wa Kituo cha Mafunzo ya Takwimu Afrika Mashariki,Dkt. Camillus Kassala akiwasilisha mada yake iliyokuwa inahusu uwezekano wa Serikali za Mitaa zinavyoweza kushiriki kwenye Miradi Mikubwa wakati wa Mkutano wa Wasambazaji wa Mafuta na Gesi hapa nchini unaoendelea leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Hyatt Regency,Dar es Salaam.
Wadau mbali mbali wakifatilia kwa makini mada zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye Mkutano wa Wasambazaji wa Mafuta na Gesi hapa nchini unaoendelea leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Hyatt Regency,Dar es Salaam.