Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama akizungumza na Mkuu wa Shule ya Sekondari Ndama ya Wilayani Karagwe Mwl. Emmanuel Muganyizi kuhusiana na umuhimu wa wanfunzi wa shule yake kuanzisha Vilabu vya Umoja wa Mataifa na faida zake.
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama akizungumza na walimu wa shule ya Sekondari Ndama na kuwapa hamasa ya kuwa walezi wazuri wa vilabu hivyo vitavyoanzishwa shuleni hapo ikiwa ni kama somo la ziada kwa wanafunzi wao ili wasipate muda wa kushiriki matendo ya ajabu na yasiyo na maadili.
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama akizungumza na vijana wa shule za sekondari Ndama wilayani Karagwe mkoani Kagera, kuwaelezea umuhimu wa kujiunga na vilabu vya Umoja wa Mataifa (UN Club) vinavyoanzishwa mashuleni kwa kuwa kwanza vitawasaidia kujitambua.
Amewaambia kwa vijana kama wao ambao tayari wameanzisha na kuendesha vilabu hivyo mashuleni kujiunga kwa wingi zaidi na kutawawezesha kujifunza shughuli za umoja wa mataifa duniani, kuhusishwa na mashirika mengine ya kimataifa, kushiriki katika mafunzo mbalimbali, warsha na mikutano ndani na nje ya nchi kama vile National Model UN, the Eastern Africa Model UN, the Africa Regional Model UN na mengineyo, ikiwemo kupata nafasi ya kuisaidia jamii zao kupitia program mbalimbali.
Bi. Usia pia amewafafanulia vijana kuwa katika klabu hizo wataweza kuwa na mtandao na vijana wengine kitaifa na kimataifa, kupata nafasi ya kufanya kazi za kujitolea.