Kikosi cha Timu ya Taifa (Taifa Stars) kikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Entebe nchini Uganda jioni ya leo,tayari kwa mtanange wa marudiano na timu ya Taifa ya nchi hiyo utakaopigwa mwishoni mwa wiki hii.
Kikosi cha Taifa Stars kikiwa uwanja wa ndege wa Mwanza kikisubiri usafiri kilikutana na Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambaye naye alitua hapo kwa muda akielekea Bukoba kwa ziara ya siku sita mkoani Kagera
Rais Kikwete akisalimiana na wachezaji wa Taifa Stars jijini Mwanza
Rais Kikwete akiwatakia Taifa Stars kila la heri katika mchezo wao wa marudiano