Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115475

Washindi watano waibuka na Milioni 10 kwenye Promosheni ya 'Cheka Plus' ya Vodacom

$
0
0
Ofisa wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini,Bw.Humud Abdulhussein(kulia)akihakiki namba ya mmoja ya washindi watano wa Sh Milioni Mbili wa promosheni ya Cheka Plus kutoka kwa Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu.Promosheni hiyo inaendeshwa kila mwezi na Vodacom.
Ofisa wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini,Bw.Humud Abdulhussein(kulia)akimshuhudia Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kushoto)akiongea na mmoja wa washindi wa Promosheni ya Cheka Plus ambapo washindi watano walijishindia shilingi milioni mbilimbili kila mmoja kupitia Promosheni hiyo kubwa ya mwezi.

Kampuni ya Vodacom Tanzania imeendelea kuboresha maisha ya Watanzania kwa kuwawezesha kujishindia kitita cha Shilingi Milioni 10 kupitia promosheni ya 'Cheka Plus.'

Kitita hicho cha Shilingi Milioni 10 kimenyakuliwa na washindi watano (5) ambapo kila mmoja amejishindia kiasi cha Shilingi Milioni 2 kila mmoja kupitia Promosheni ya 'Cheka Plus' iliyofanyika tarehe 20 mwezi huu. 

Washindi hao ni pamoja na; Musa Hussein Ellmy ambaye ni mkazi wa (Karatu - Arusha), Vumi Joshua Mteru (Kilimanjaro), Joseph Godfrey Kyando (Tunduma, Mbeya), Anatori Emmanuel Chogolo (Dar es Salaam), na Amina Joseph Mmbaga (Arusha).

Meneja Uhusiano wa Umma wa Kampuni hiyo Bw. Matina Nkurlu, alisema kuwa zaidi ya wateja 6,000 wamefaidika na ofa hiyo kabambe inayoendelea hivi sasa nchi nzima ambapo zaidi ya Shilingi Milioni 100 zilikabidhiwa kwa wateja mbalimbali walioshinda kupitia Promosheni ya 'Cheka Plus.'

Nkurlu alisema kuwa hadi hivi sasa, tayari wateja mbalimbali nchini wameweza kujishindia kiasi kinachofikia zaidi ya Shilingi milioni 100 "Tumekuwa tukipata washindi 100 kila siku ambapo wamekuwa wakijishindia shilingi 10,000 kila mmoja na washindi wengine 10 wakijinyakulia shilingi 50,000 kila siku, sambamba na droo kubwa ya mwezi ambapo katika washindi watano(5) kila mmoja wao amekuwa akijinyakulia kitita cha shilingi milioni mbili.

Hivyo toka uzinduzi wa promosheni hii ya 'Cheka Plus,' wateja takribani 10 wameweza kujishindia kiasi cha shilingi milioni mbili mbili kila mwezi," alisema Nkurlu nakuongeza kuwa "promosheni hiyo bado inaendelea hivyo ninapenda kuwasihi wateja wa mtandao wa Vodacom kuendelea kufaidika na huduma zetu ikiwemo promosheni ya "Cheka Plus" na kuweza kujishindia zawadi kemkem sambamba na kuendelea kuwasiliana na wapendwa wao."

Kampuni hiyo kupitia mpango wake wa Promosheni ya 'Cheka Plus,' umewezesha wateja kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi wa maneno (SMS), na kuperuzi kwenye mtandao wa intaneti bila hofu.

Ili kuweza kujiunga na huduma ya Cheka Plus, wateja wanashauriwa kupiga *149*01 # na kuchagua kifurushi wanachokitaka. Promosheni ya Cheka Plus inawezesha wateja kutuma SMS na kupiga simu katika kiwango cha bei nafuu kabisa.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115475

Trending Articles