Mdau Sara Ali Aboud akitembea kwa madaha kwenye stage mara baada ya kulamba Nondoz yake ya BSc in Mathematics (Financial IT ),katika Chuo Kikuu cha Brunell University nchini Uingereza.
Mdau wa Globu ya Jamii,Sara Aboud (kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na mama yake mzazi Bi Mariam Kilumanga (Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake UK -TAWA) na mdogo wake Samie Aboud wote wakiwa ni wenye furaha sana baada ya Sara kulamba Nondozz yake hiyo.
Mdau Sara Ali akiwa katika pozi na anti yake,Bi Mariam Mungula a.k.a Katibu CCM UK / TAWA UK .
Siku isingekamilika iwapo Mdau Sara Ali asingepata picha Ukumbusho na Mkuu wa Chuo "Vice Chancellor " wa Brunell University.
GLOBU YA JAMII INAMPA HONGERA SANA MDAU SARA ABOUD KWA KUKAMILISHA MASOMO YAKE HAYO, NA HONGERA SANA KWA MZAZI WA SARA KWA KAZI NZURI YA KUMSOMESHA BINTI ILI AJE KUWA MSAADA MKUBWA KWA TAIFA LETU HAPO BAADAE.