Familia ya Mzee Shilatu wa Mbagala wanasikitika kutangaza kifo cha Baba yao Mpendwa JOHN SHILATU kilichotokea katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili tarehe 23/07/2013 saa 10 jioni kutokana na shinikizo la damu.
Habari ziwafikie Ndugu, Jamaa, Marafiki, Viongozi, Wanasiasa wote wanaomfahamu vyema Marehemu popote pale walipo.
Mipango ya mazishi inafanyika Nyumbani kwa Marehemu Mbagala. Kwa mawasiliano zaidi juu ya msiba piga simu namba 0717 488622
Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe.
Amen!!