Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115471

RUBADA yawataka vijana Makambako kuchangamkia kilimo

$
0
0
 Mmoja wa vijana wanaojishughulisha na kilimo cha mboga mboga katika Bonde la Mlowa katika Halmashauri ya Mji wa Makambako Mkoani Njombe, Saimon Mdee (kushoto) akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uendelezaji wa Bonde la Mto Rufiji (Rubada), Bw. Aloyce Masanja alipowatembelea vijana hao katika shamba la maparachichi na mbogamboga, ikiwa ni katika kuhamasisha kilimo kupitia Mpango wa Ukuaji wa Kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT).
Mkulima wa mboga mboga katika Bonde la Mlowa katika Halmashauri ya mji Makambako Mkoani Njombe, Bw. Joseph Chengula (Kulia) akimwonyesha ukubwa wa bonde la Mlowa, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uendelezaji wa Bonde la Mto Rufiji (RUBADA) Bw. Aloyce Masanja( katikati)  alipofanya ziara ya kutembelea kambi za vijana wanaojishughulisha na kilimo katika mji huo jana.  Mkurugenzi huyo alikua katika ziara ya kuhamasisha kilimo kupitia Mpango wa Ukuaji wa Kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT).  Kulia ni mkulima mwingine wa mbogamboga, Bw. Silas Martin.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115471

Trending Articles