Onyesho kubwa la kimataifa "International African Festival Tubingen 2013,linatalajiwa kuanza tarehe 8 hadi 11.Augost 2013,mjini Tübingen, jirani na Stuttgart huko Ujerumani. Maonyesho hayo ya aina yake yanatarajiwa kuhudhuriwa na watu zaidi ya 100,000 kutoka sehemu mbali mbali duniani.
wanasanii zaidi 600 zikiwemo bendi za muziki za kiafrika zitatumbuiza katika maonyesho hayo makubwa ya kiafrika barani ulaya.
Bidhaa na sanaa kutoka nchi mbali mbali za kiafrika ndizo zitakaonyeshwa katika maonyesho hayo,kutakuwa na mikutano katika ya wafanyibiashara wa kiafrika na wa Ujerumani kwa lengo la kukuza uhusiano wa kibiashara.
Onyesho hilo pia litaudhuriwa na mabalozi na wawakilishi wa nchi za kiafrika nchini Ujerumani,pamoja na viongozi wa jumuiya za kiafrika nchi ujerumani.
Maonyesho ya "International African Festival Tubingen " yanayo andaliwa na shirika lisilo la kiserekali Afrikaktiv e.V, chini ya mkurugenzi wake Madam Susan Enih Tatah,maonyesho hayo yanakuwa kwa kasi kubwa na kuwa na mvuto wa maelfu ya watazamaji.
Kwa wale wanao shiriki au kuhudhuria maonyesho hayo wanaweza kuwasiliana at Susan Enih Tatah – Founder & CEO
AFRIKAKTIV e.V
Call:+49(0)15210910374
kontakt@afrikafestival.net