Naibu Waziri wa Fedha, Bi. Saada Mkuya Salum (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Bi. Mizinga Melu (kushoto kwake) wakichukua mlo wa futari pamoja na baadhi ya wateja wa benki hiyo katika hafla ya futari iliyoandaliwa na NBC kwa wateja wake jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Naibu Waziri wa Fedha, Bi. Saada Mkuya Salum (kushoto) akizungumza na Mjumbe wa Bodi ya Benki ya NBC, Dk Kassim Hussein (kulia) wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na NBC kwa wateja wake jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bi. Mizinga Melu na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, Bi. Mwinda Kiula Mfugale.
Mkuu wa Huduma za Kibenki kwa kufuata kanuni za Kiislamu wa Benki ya NBC, Yassir Masoud (wa pili kushoto) pamoja na baadhi ya wateja wa benki hiyo, wakichukua mlo wa futari katika hafla ya futari iliyoandaliwa na NBC kwa wateja wake jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Bi. Mizinga Melu (kulia) akimsilikiliza Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Bi. Mwinda Kiula Mfugale (kushoto) katika wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Huduma za Kibenki kwa kufuata kanuni za Kiislamu wa Benki ya NBC, Yassir Masoud (katikati) akiteta jambo na Meneja Uhusiano wa benki hiyo, Eddie Mhina wakati wa hafla ya futari waliyoiandaa kwa wateja wao jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mjumbe wa Bodi ya NBC, Dk. Kassim Hussein.
Baadhi ya wateja wa benki ya NBC, wakila futari waliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.