Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 110189

KAMATI YA BUNGE YA MAADILI YAMHOJI MHE. KUBENEA MJINI DODOMA

$
0
0
Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, imemhoji Mbunge wa Ubungo Mheshimiwa Saed Kubenea kwa kosa la kutoa kauli ya kudharau Bunge.

Akizungumza mara baada ya kumhoji Mbunge huyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mheshimiwa Almasi Athuman Maige (Mb) alisema, Mheshimiwa Kubenea amefikishwa mbele ya Kamati hiyo kujibu tuhuma inayomkabili kutokana na kauli aliyotoa kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 26 (e) na 34 (1) (a) ya Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge, Sura ya 296. 

Mheshimiwa Maige alisema mahojiano hayo yamefanyika leo baada ya kuahirishwa mara mbili kutokana na Mheshimiwa Kubenea kutokua katika hali nzuri kiafya na hivyo kuomba mahojiano yaahirishwe. 

Mheshimiwa Maige aliongeza kuwa baada ya kumsikiliza Mhe. Kubenea itaandaa Taarifa yake na kuiwasilisha kwa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai kwa hatua zaidi.

“Kanuni zimeweka masharti kuwa shughuli za Kamati hii zinazofanywa zitabakia kuwa ni siri hadi hapo itakapomaliza kazi yake na kuwasilisha taarifa Bungeni,” alisema.
Mwenyekiti Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Mhe. Almasi Athuman Maige (Mb), akiongoza kikao cha Kamati hiyo kilichokutana kumhoji Mhe. Saed Kubenea (Mb) kwa kosa la kutoa kauli ya kudharau Bunge kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 26 (e) na 34 (1) (a) ya Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge, Sura ya 296. Mhe. Kubenea alifika mbele ya Kamati hiyo leo ikiwa ni mara ya tatu baada ya kuomba mahojiano yake yaahirishwe mara mbili kutokana na kutokuwa katika hali nzuri kiafya.
Mbunge wa Ubungo, Mhe. Saed Kubenea (Mb) akijieleza mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa kosa la kutoa kauli ya kudharau Bunge kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 26 (e) na 34 (1) (a) ya Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge, Sura ya 296. Mhe. Kubenea amefika mbele ya Kamati hiyo leo kwa mara ya tatu baada ya kuomba mahojiano hayo yaahirishwe mara mbili kutokana na kutokuwa katika hali nzuri kiafya.PICHA NA BUNGE

Viewing all articles
Browse latest Browse all 110189

Latest Images

Trending Articles



Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>