Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage akifafanua jambo wakati wa Mkutano Mkuu wa Simba wa kujadili maendeleo ya klabu hiyo ulioanza saa nne kamili na kumalizika saa tano kamili katika Bwalo la Maofisa wa Polisi jijini Dar es Salaam leo, ambapo wanachama zaidi ya 700 walihudhuria mkutano huo.
Mwanachama wa Simba kutoka Iringa akiuliza swali katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali (kushoto) akifuatilia mkutano huo.
Baadhi ya wanachama wa Simba wakiwa katika mkutano huo.